Monday, March 28, 2016

Ban awasili Tunisia kwa ziara ya siku mbili


Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwasili Tunisia, Machi 28 2016/Picha: UNIC Tunis
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewasili mjini Tunis, Tunisia kwa ziara ya siku mbili, ambapo anatarajiwa kukutana na rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi, na maafisa wengine wa ngazi ya juu serikalini.
Ban anatarajiwa kumpongeza rais wa Tunisia kwa hatua ambazo nchi yake imepiga katika kukuza demokrasia, na kwa juhudi zake katika kukabiliana na tifauti za kitanaka kijamii na kiuchumi.
Akiwa Tunisia, Katibu Mkuu anatarajiwa kukutana na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, wakiwemo wafanyakazi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya wanaokaa Tunisia.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment