Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani Papa Francis amezungumzia dhidi ya "kukataliwa" kwa wahamiaji na wakimbizi katika ujumbe wake wa Pasaka, wakati huu Ulaya ikikabiliana na wimbi kubwa kabisa la mgogoro wa wakimbizi tangu kumalizia kwa Vita ya Pili ya Dunia. Papa alisikika akisema "Ujumbe wa Pasaka kwa Kristo aliyefufuka...unatualika sote tusisahahu wale wote, wake kwa waume wanaotafuta maisha bora ya baadae, na zaidi umma wa wahamiaji na wakimbizi wanaokimbia vita, njaa, umasikini na kutokuwepo kwa haki za kijamii". Papa alikuwa akiizungumzia Syria, mgogoro wa muda mrefu, uliogubikwa na vifo, ukiukwaji wa haki za binaadamu, na kusisitiza kuwa ana matumani mazungumzo ya amani ambayo yamepangwa kuanza tena mwezi ujao kati ya serikali na upande wa upinzani yatazaa matunda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment