mbunge wa Kilolo mkoani Iringa Bw Venance Mwamoto akisalimiana na wananchi wa Ilula waliokuwa wakisubiri maji
Mwamoto akizungumza na meneja wa maji mji mdogo wa Ilula Bi Mvungi
Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto (kushoto) akisalimiana na mmoja kati ya wazee wa mji wa Ilula aliyetoka kuchota maji
Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto akisaidia kufungulia maji
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto ameahidi kuongozana na wazee wa mji wa Ilula kwenda Dodoma kuonana na waziri mkuu Kassim Majaliwa ili kumfikishia ahadi ya maji ya Rais Dr John Magufuli kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula .
Huku akiwataka wananchi wa Ilula na Nyalumbu kutomchagua mwaka 2020 iwapo atashindwa kutekeleza ahadi ya maji katika mji huo wa Ilula ndani ya miaka yake mitano ya ubunge.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Nyalumbu na Ilula wakati wa mikutano yake ya hadhara ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo la Kilolo jana ,Mwamoto alisema kuwa kero ya maji katika mji wa Ilula imekuwa ya muda murefu jambo ambalo hatataka kuona wananchi hao wakiendelea kutabika.
Alisema kuwa kero hiyo ya maji imeanza kuwasumbua wananchi hao toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 hadi leo wapo katika mahangaiko ya maji na baadhi ya viongozi wameendelea kufanya udanganyifu wa mradi huo kama ambavyo mwaka 2010 viongozi walivyomdanganya aliyekuwa makamu wa Rais Dr Alli Mohamed Shein kwa kupelekwa kufungua mradi wa maji ambao viongozi walimdanganya kwa kujaza maji katika tanki hilo ili azindue mradi huo.
Hivyo alisema udanganyifu huo hautapewa nafasi katika uongozi wake wa miaka mitano lazima kero hiyo imalizike na wananchi hao waweze kupata maji vinginevyo yupo tayari kuongoza wananchi wake kumzuia waziri wa maji kupita Ilula kwenda jimboni kwake Njombe iwapo wananchi hao hawatatimiziwa ahadi yao ya maji safi na salama .
Mbunge huyo alisema katika kikao kijacho cha bunge kinachoanza mwezi ujao ataomba wananchi wa Ilula na Nyalumbu kumteulia wazee watatu ama wanne ili kwenda nao bungeni Dodoma kukutana na waziri mkuu ili kwa ajili ya kumkumbusha ahadi ya Rais ya maji katika mji huo wa Ilula
Pia aliagiza mamlaka ya maji ya mji mdogo wa Ilula kuchunguza vema mradi wa maji uliopo kama umejengwa kwa kiwango ama chini ya kiwango maana amesema mradi mdogo uliopo kwa sasa bado umekuwa na kero kubwa ikiwa
ni pamoja na baadhi ya maeneo kuvujisha maji huku akiwataka wananchi kwa upande wao kutunza miundombinu ya maji.
ni pamoja na baadhi ya maeneo kuvujisha maji huku akiwataka wananchi kwa upande wao kutunza miundombinu ya maji.
Katika hatua nyingine mbunge Mwamoto alimshauri meneja wa maji wa IRUWASA katika mji wa Ilula Teodolah Mvungi kuangalia uwezekano wa kuboresha kituo cha maji eneo la Ilula ili kiweze kunufaisha wananchi wengi na kuwa iwapo wataanza uboreshaji kwa upande wake ataunga mkono .(P.T)
No comments:
Post a Comment