Monday, March 28, 2016

Ajali ya Helicopter yaua watu 12 Algeria



Ajali ya Helicopter yaua watu 12 Algeria
Watu wasiopungua 12 wamepoteza maisha Algeria kufuatia ajali ya helikopta wakati ikilinda doria katika eneo la jangwa la Sahara nchini humo.
Wizara ya Ulinzi ya Algeria imetoa taarifa na kusema helikopta hiyo ilianguka Jumapili kutokana na matatizo ya kiufundi. Taarifa hiyo imesema tukio hilo lilijiri wakati helikopta hiyo ilipokuwa ikiruka baina ya miji ya Adrar na Reggan katika eneo la Tamanrasset.  Uchunguzi umeanzishwa na jeshi la nchi hiyo kuhusu ajali hiyo. Algeria imekuwa ikipambana na magaidi wa Kitakfiri hasa kundi la kigaidi la Al Qaeda katika eneo la Maghreb AQIM.
Jumapili iliyopita, jeshi la Algeria liliua magaidi wanne na kuwajeruhi wengine watatu katika eneo la jangwani wakati magaidi hao waliposhambulia kituo cha kuzalisha gesi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment