Thursday, March 31, 2016

Watuhumiwa watatu wafunguliwa mashtaka Brussels



Watu hao waliofunguliwa mashtaka wametajwa kuwa ni Yassine A. Mohamed B na Aboubaker O.
Msichana anawasha mshumaa katika eneo lililotokea mashambulizi ya mabomu Brussels.
Msichana anawasha mshumaa katika eneo lililotokea mashambulizi ya mabomu Brussels.
Waendesha mashtaka wa serikali kuu ya Brussels wamesema Jumatatu kwamba wamewafungulia mashtaka watu watatu kwa kuhusika kwao katika kundi moja la ugaidi.
Ukamataji huo unafuatia shambulizi la mabomu wiki iliyopita katika mji mkuu wa Ubelgiji ambalo liliuwa watu wasiopungua 35, wakiwemo raia wanne wa Marekani. Taarifa kutoka kwenye ofisi hiyo imesema kwamba mtu wa nne aliyekamatwa, aliachiwa Jumapili.
Kerry BrusselsKerry Brussels
Watu hao waliofunguliwa mashtaka wametajwa kuwa ni Yassine A. Mohamed B na Aboubaker O.
Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa na waendesha mashtaka hawakusema moja kwa moja kama washukiwa walihusika katika shambulizi la wiki iliyopita lililosababisa vifo.
Wakati huo huo rais wa Marekani Barack Obama alitoa rambi rambi zake Jumapili kwa njia ya simu kwa wazazi wa Justin na Stephanie Shults, wanafamilia ambao walifariki katika mashambulizi ya wiki iliyopita huko Brussels.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Yanga yafanikiwa kutinga nusu fainali kwa ushindi huu dhidi ya Ndanda FC (+Pichaz)


March 31 klabu ya Dar Es Salaam Young Africans inayojiandaa na mchezo wake wa klabu Bingwa barani Afrika dhidi ya klabu ya Al Ahly ya Misri, ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa robo fainali ya Kombe la FA.
Yanga ambayo ipo kambini kwa muda mrefu kujiandaa na mchezo wa klabu bingwa, ilifanikiwa kuiadhibu Ndanda FC katika mchezo wake wa robo fainali ya Kombe la FA,Yanga ilianza kufungwa goli na Atupele Green, lakini lilikataliwa na muamuzi wa mechi.
Baada ya Ndanda FC kuonesha jitihada za kutaka kupata goli, Yanga walilazimika kuongeza nguvu ya ziada na Paul Nonga dakika ya 26 akapachika goli la uongozi kwaYangaNdanda FC walifanya jitihada na dakika ya 57 nahodha wao Kigi Makasyakapachika goli la kusawazisha.
Uzoefu uliwafanya Yanga wafanikiwe kupata goli la pili na ushindi, kwani Ndanda FCwalifanya faulo katika eneo la hatari, na muamuzi wa mechi Jimmy Fanuel kutokaShinyanga akaamua ipigwe penati, Kelvin Yondani kazidi kudhihirisha umahiri wake katika upigaji wa penati kwa kuipachikia Yanga goli la ushindi na kuipeleka nusu fainali.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Watu 33 wapoteza maisha katika ghasia za kisiasa Uganda



Jeshi la Uganda la likiwa katika njia za Kampala baada ya uchaguzi.
Jeshi la Uganda la likiwa katika njia za Kampala baada ya uchaguzi.
Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni amelazimika kufanya ziara ya ghafla katika eneo la Rwenzori kwenye mpaka wa Uganda na Congo, ambako hali ya wasiwasi inaendelea kuongezeka, vyombo vya usalama vilitoa hesabu ya watu 33 kuuawa hadi sasa kutokana na makabiliano kati ya raia na polisi.
Museveni ametembelea eneo hilo, huku nyumba zikiwa tupu, watu wakitoroka makwao wakitafuta mahali salama licha ya mkuu wa Polisi wa Uganda Jenerali Kaye Kayihura kuamua kukita kambi katika eneo hilo ili kujaribu kumaliza hali ya uhasama kati ya raia na Polisi hao.
 Hii ni wiki ya tatu sasa idadi ya watu wanaouwawa kutoka na uhasama kati ya raia na Polisi inaendelea kuongezeka kutokana na ghasia hizo, uhasama huu ulianza pale Polisi walipouwa vijana saba waliokuwa wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa huku Polisi wakikanusha kwamba ghasa hizo ni za kijamii na sio vurugu za kisiasa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

MAGARI 5 YA TFF YAKAMATAWA NA TRA KWA KODI YA TSH BILIONI 1.118


jengo-la-TFF1Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala yake imeondoka na magari matano yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kiasi kikubwa cha kodi.TRA LOGO

TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao.

Richard Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyakamata magari hayo yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu zilizopelekea kufanya hivyo.

“Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanayotokana na deni la kodi ambalo TFF hawajalipa.

“Mpaka sasa tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu deni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano.”

Hii ni mara ya pili kwa TFF kupigiwa hodi na TRA ikilalamikiwa kulimbikiza madeni ya kodi, mara ya kwanza TRA ilizifunga account zote za TFF lakini safari hii wameamua kuyashikilia magari yao.

Kwa mujibu wa Kayombo, magari hayo yapo kwenye yard ya YONO likiwemo basi ambalo hutumiwa kuisafirisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Wanawake 14 wapokea tuzo ya Marekani ya Wanawake Shujaa


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani  John Kerry pamoja na Balozi wa masuala ya wanawake Cathy Russell wakipiga picha na washindi wa tunzo ya "Wanawake Shujaa" 2016.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry pamoja na Balozi wa masuala ya wanawake Cathy Russell wakipiga picha na washindi wa tunzo ya "Wanawake Shujaa" 2016.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, aliwakabidhi  wanawake kumi na wanne kutoka nchi mbali mbali za dunia tuzo ya Wanawake Shujaa, kwa kuonyesha uongozi katika kutetea haki, haki za binadam, demokrasia, usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.
Mmoja kati ya walopokea tuzo hiyo maarufu inayotolewa kila mwaka na Marekani,  ni mwanaharakati wa kichina, Ni Yulan, aliyezuiliwa na serikali yake kusafiri hadi Washington.
Miongoni mwa wanawake watatu kutoka Afrika ni Vicky Ntetema, Mtanzania aliyetunukiwa tuzo hiyo kwa jitihada zake za kufichua mbinu zinazotumika kuwauwa na kuwakata viungo watu wenye ulemavu wa ngozi – albino.
Waziri Kerry amesema, “Mwaka huu tunatambua kundi la wanawake walonesha ushujaa katika fani tatu muhimu. Kufichua na kupinga ghasia kwa misingi ya ngono, wanapambana na ulaji rushwa na kuimarisha utawala wa sheria na wanaohamasisha haki za kisheria na haki za binadamu kwa wote.”
Huu ni mwaka wa 10 tangu kuanzishwa kwa tunzo ya “Women of Courage”, ambapo hasi sasa wanawake 101 wamepokea tunzo hiyo kutokana na mafanikio yao.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

ZITTO KUWATAJA WATUMISHI HEWA WIZARA YA UJENZI




Mbunge wa Kigoma mjini kupitia ACT Wazalendo Zitto Kabwe, aitaka Serikali kuwabainisha wafanyakazi hewa kwenye Wizara, baada ya agizo la Rais la kuhakiki watumishi hewa kwenye Halmashauri kutekelezwa.

Zitto Kabwe ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook, na kuonesha kushangazwa kwa Wizara kutoweka wazi wafanyakazi hewa waliomo humo, huku akijitolea kubainisha wale wa kwenye wizara ya ujenzi.

“Watumishi hewa kwenye wizara mbona hatusikii? Wakuu wa mikoa wameagizwa kutambua watumishi hewa. Mawaziri hawakuagizwa. Ok ngoja nijitolee kutambua watumishi hewa wizara ya ujenzi kupitia ripoti za CAG 2010/2011 mpaka 2014/2015”, aliandika Zitto Kabwe.

Jana mikoa yote nchini imetekeleza agizo la kuhakiki wafanyakazi hewa walioko kwenye halmashauri zao, huku mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kuwa na wafanyakazi hewa 334.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Wazazi wa msichana anayedaiwa kujitoa muhanga Nigeria kumtambua



Girls who escaped from their Boko Haram captors arrive at the presidential villa in Abuja, July 22, 2014.
Girls who escaped from their Boko Haram captors arrive at the presidential villa in Abuja, July 22, 2014.

Wazazi wa wasichana wa shule waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram wamesema wanangoja kusafiri kuelekea Cameroon ili kuthibitisha iwapo msichana aliyetaka kujitoa muhanga aliyekamatwa na kutoka Chibok kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo wasichana 276 wa shule walitekwa karibu miaka miwili iliopita ni miongoni mwao.
Hata hivyo mvutano umeibuka kwa kuwa mtoto aliekamatwa Ijumaa akiwa na mkanda wenye vilipuzi anaonekana kuwa na umri wa takriban miaka 10. Mzazi Yakubu Nkeki kutoka Chibok amesema anaweza kudhibitisha iwapo atamuona msichana huyo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

PROFESSA J: NAHAMISHIA STUDIO YANGU MIKUMI



Jay-mwanalizombe

Joseph Haule a.k.a profesor Jay amesema atahamisha studio yake ya Mwanalizombe iliyopo Dar es salaam hadi jimboni kwake Mikumi mkoani Morogoro.

Akiongea hayo kupitia Clouds fm mbunge huyo wa Mikumi katoa sababu ya kuhamisha jimboni kwake lengo kuu kusaidia wananchi wa jimbo hilo kwani yawezekana kuna vipaji ili wajipatie ajira kupitia studio yake.

Amewaomba  watengenezaji wa muziki(producer) waje kutengeneza ngoma kupitia studio hiyo ili kutoa mchango wao kwa wananchi wa mkoa huo.

Profesor Jay amesema pia ataongeza na video shooting kwa ajili ya kutengeneza wigo mpana kwa wana kwaya au sherehe na shughuli zote zinazo husu video.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Korea Kaskazini yarusha tena makombora



North Korean leader Kim Jong Un salutes as he arrives to inspect a military drill at an unknown location.
North Korean leader Kim Jong Un salutes as he arrives to inspect a military drill at an unknown location.

Korea Kusini imesema kuwa Korea Kaskazini imerusha makombora ya masafa mafupi kwenye bahari karibu na ufukwe wake licha ya taifa hilo lililotengwa kuwekewa vikwazo vya kimataifa pamoja na zoezi la kijeshi linaloendelea kwa ushirikiano wa Marekani na Korea Kusini.
Wakuu wa kijeshi wa Korea Kusini wamesema kombora lilirushwa leo karibu na mji wa bandari wa Korea Kaskazini wa Wonan huku ikienda umbali wa kilomita 200 kabla ya kuanguka ardhini.
Pyongyang ilirusha makombora matano ya masafa mafupi jumatatu ya tarehe 21 Machi kwenye bahari ya mashariki kutoka kwenye mji wa Hamhung. Korea Kusini imekuwa ikitishia kurusha makombora ya nyuklia dhidi ya Washington na Seoul kama hatua ya kulalamikia zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Marekani yapata njia ya kutoa taarifa za simu za Apple



Joey Mink demonstrates outside the Apple store in New York protesting the FBI for obtaining a court order that requires Apple to make it easier to unlock an encrypted iPhone.
Joey Mink demonstrates outside the Apple store in New York protesting the FBI for obtaining a court order that requires Apple to make it easier to unlock an encrypted iPhone.
Hatimae Wizara ya Sheria ya Marekani imepata njia ya kutoa taarifa kwenye simu ya iPhone 5C iliotengenezwa na kampuni ya Apple kwa kutumia mbinu ambayo haijatolewa wa umaa.
Hatua hiyo imefikisha kikomo kesi iliokuwa ikiendelea kati ya Serikali na kampuni ya Apple kuhusiana na simu ya mshukiwa wa shambulizi la mwaka jana mjini San Bernardino, California.
Sasa swali lililobaki ni la viwango vya habari ambavyo Serikali inaweza kupata kutoka kwa raia wake na mbinu zinazotumika. Mjumbe wa baraza la Congress kutoka California, Darell Issa, ambae amekuwa akiongoza kampeni ya kulindwa kwa taarifa za kibinafsi, amesema ni bora kesi hiyo ilivyomalizika bila kuongoja uamuzi wa mahakama lakini swala la habari za kibinafsi lingali halijatatuliwa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Waziri mkuu wa India anaimani huyu mwigizaji anafaa kuwa rais wa India.



president
Mwana siasa Amar Singh amesema Waziri mkuu wa India Narendra Modi anampango wa kumpendekeza staa wa filamu kutoka Bollywood Amitabh Bachchan kuwa rais ajayo wa India.
amitabh-bachchan
Amar Singh amesema haya akifanyiwa mahojiano na 24X7 kuwa Amitabh Bachchan anaweza kutajwa kama watu wenye uwezo wa kuwa rais wa India. Amar Singh ndiye alimtambulisha Amitabh Bachchan kwa waziri mkuu Narendra Modi
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Tetesi,Mpenzi wa Tyga ‘Kylie Jenner’ anaujauzito.



kylie-jenner-tyga-king-cairo
Maneno mtaani yanasema mpenzi wa rapa Tyga ‘Kylie Jenner’ anaujauzito wa msanii huyu akiwa na miaka 18.
Huyu atakuwa mtoto wa kwanza kwneye mahusiano yao na wapili kwa Tyag ambaye ana mtoto wa kiume King Cairo, 3, kutoka kwenye mahusiano yake na Blac Chyna.
Uvumi huu umesambaa baada ya Kulie kuongezeka uzito hivi karibuni na muonekano wake kubadilika kabisa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mahakama ya Uganda yaidhinisha ushindi wa Museveni



Rais Yoweri Museveni wa Uganda
Rais Yoweri Museveni wa Uganda
Mahakama nchini Uganda imeidhinisha ushindi wa Yoweri Museveni kama Rais wa Uganda kwa mhula wa tano kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.
Jopo la majaji 9 lilitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Amama Mbabazi aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha upinzani cha Go Forward, ambaye alipinga ushindi wake Museveni, kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Taarifa kamili na mwandishi wa Sauti ya Amerika-VOA, Kennes Bwire kutoka kampala nchini Uganda.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Davido awapongeza D’banj na Banky W kwa mchezo wao wa ku***ga nje.




Davido
Staa wa muziki Nigeria amewapongeza wasanii wawili wakubwa ambao wamekuwa na wanawake wakali nje na ndani ya Nigeria ila hawajawahi kuwa na watoto au BABY MAMA.
Tofauti na 2Baba, Wizkid, Olamide, Flavour, Ice Prince, Duncan Mighty, Timaya wote hao wana watoto bila ndoa, D’banj na Banky W bado hawana watoto na ni nikutokana na mchezo wao wa PULL OUT GAME au KUMWAGA NJE.
Shabiki mmoja amemshauri Bank W kufanya wimbo wa MY PULLOUT GAME
.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mafanikio ya Magufuli yanahitaji mabadiliko ya sera-Mkumbo.



Profesa Kitila Mkumbo.
Profesa Kitila Mkumbo.
Kufuatia tamko la rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kupunguza mishahara ya wakuu wa taasisi na mashirika ya umma nchini Tanzania baadhi ya wachambuzi wamepokea kwa hisia tofauti nchini humo.
Mahojiano na Profesa Kitila Mkumbo

Uamuzi huo utaathiri mashirika mengi ya umma nchini humo ambapo baadhi ya wakuu wake wametajwa kupokea mshahara wa zaidi ya milioni 30 kwa mwezi .
Mchambuzi wa siasa nchini Tanzania na mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kitila Mkumbo, anasema kufanya kazi kwenye mashirika haya ni sehemu ya utumishi wa umma na akisistiza kwamba wakuu wa mashirika haya wasitarajie kulipwa kiasi kikubwa kupita kiasi akipinga wale wanaodai kwamba kupunguza mishahara hiyo kunaweza kupunguza utendaji au morali katika mashirika ya umma.
Pia akiongeza kwamba ili Rais Magufuli na chama chake wafanikiwe lazima wabadilishe mtazamo wa kisera, kiitikadi na kifalsafa bila hivyo mabadiliko hayatakuwa na msingi wowote wa kufanikiwa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Sudan Kusini: kundi la kwanza la waasi wa Riek Machar lawasili Juba



Kundi la kwanza la askari waasi wa Sudan Kusini waliwasili Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.

Hii ni hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mkataba wa amani uliosainiwa miezi saba iliyopita kati ya makundi hasimu katika vita vya wenyewe kwa wenyew nchini Sudan Kusini kwa zaidi ya miaka miwili, kundi la waangalizi wa kimataifa limetangaza.
Askari thelathini na tisa waasi wamewasili mjini Juba kwa jumla ya 1.370 wanonatarajiwa kama sehemu ya mkataba wa amani ulioafikiwa mwezi Agosti mwaka 2015, Tume ya ufuatiliaji na tathmini ya makubaliano (JMEC) imebaini. Tume hii iliundwa na jumuiya ya kikada ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD).
Waangalizi wa kimataifa piawamemtolea wito kiongozi wa waasi Riek Machar kushikilia nafasi ya Makamu wa Rais.
"Hakuna tena vikwazo kwa Makamu wa Rais alieteuliwa kurudi na uundwaji wa serikali mpya ya mpito ya umoja wa kitaifa," Festus Mogae, ambaye anaongoza JMEC, amesema.
Riek Machar aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais Februari 12 na hasimu wake Rais Salva Kiir, ikiwa inaonekana kama ishara ya maendeleo katika utekelezaji wa mkataba wa amani. Lakini mchakato wa kuundwa kwa serikali ya umoja na ya mpito badoumekwama, na mapigano yanaendelea katika nchini changa duniani.
Sudan Kusini ilitangaza uhuru wake mwezi Julai 2011, baada ya miongo kadhaa ya mgogoro na Khartoum, kabla ya kutumbukia tena miaka miwili na nusu baadaye katika vita kwa sababu ya kugawanyika kutokana na sababu za kisiasa na kikabila ndani ya jeshi, sababu zilizochochewa na uhasama kati ya Salva Kiir na Riek Machar.
Hayo yakijri, Umoja wa Mataifa, Jumanne hii, umeonya kuwa njaai mefikiwa katika kiwango cha "kutisha" nchini Sudan Kusini, ambapo bei za vyakula ni kubwa mno baada ya miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe viliokumbwa na mauaji na tuhuma za uhalifu wa kivita.
"Ripoti ya kutisha ya njaa, utapiamlo na viwango vya janga la uhaba wa chakula vimeshuhudiwa katika maeneo mengi yaliokumbwa na machafuko," shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Kilimo ( FAO) limesema katika taarifa yake.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Pentagon kutuma kikosi cha kudumu Ulaya ya Mashariki



Kifaru cha jeshi la Marekani kiitwacho Abrams kiliotumwa katika mji wa Riga, Latvia, Machi 9, 2015
Kifaru cha jeshi la Marekani kiitwacho Abrams kiliotumwa katika mji wa Riga, Latvia, Machi 9, 2015
AFP

Marekani inapania kutuma kikosi cha wanajeshi wa kudumu watakaokua wakibadilishwa kila mara katika Ulaya ya Mashariki ifikapo Februari 2017, kama sehemu ya jitihada zake za kuzuia uwezekano wa uchokozi kutoka Urusi, Pentagon imesema Jumatano hii.

"Askari wa kikosi hiki watakua wanabadilishwa kila mara, hivo kuruhusu uwepo wa kikosi cha kudumu chenye magari ya kivita na mafunzo yataboreshwa huku kukiwa na mazoezi pamoja na washirika " wa NATO, amesema Laura Seal, msemaji wa Pentagon.
Kutakuwa na "uwepo endelevu wa kikosi cha kudumu Ulaya ya Mashariki," Seal amebaini.
Pentagon na NATO walikua tayari wamejadili kupelekwa kikosi cha askari watakaokua wakibadilishwa kila mara katika Ulaya ya Mashariki, bila hata hivo kutoa ratiba iliyo wazi.
Mwezi Februari Washington ilitangaza nia yake ya kuongeza mara nne mwaka 2017, gharama zake hadi kufikia Dola bilioni 3.4 zitakazotumiwa kwa kuimarisha jeshi la Marekani barani Ulaya.
Pamoja na kikosi hiki chenye askari 4,200 ambao watakua na vifaa vya kivita ikiwa ni pamoja na vifaru na magari ya kivita), kitakuwa na vitengo vitatu vya kivita barani Ulaya.
Pamoja na vitengo vyote, jeshi la Marekani lina askari 62,000 barani Ulaya.
Moscow imekua ikionya mara kwa mara dhidi ya "uwepo wa askari wa kudumu" kutoa nchi washirika katika mpaka wake, ambapo inaona kuwa ni kinyume na sheria inayounda NATO-Urusi , iliyosainiwa mwaka 1997.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

François Hollande aachana na marekebisho ya katiba



Rais wa Ufaransa François Hollande.
Rais wa Ufaransa François Hollande.
REUTERS/Stephane de Sakutin/Pool

Baada ya miezi minne ya mijadala mikali, François Hollande Alhamisi hii, ameamua kuachana na marekebisho ya katiba ambayo alianzisha mwenyewe baada ya mashambulizi ya Novemba, na ambayo yalikwama kufuatia suala la kunyang'anywa uraia kwa Wafaransa wenye asili ya kigeni watakaojihusisha na ugaidi.

"Nimeamua, baada ya kuzungumza na marais wa Bunge na Seneti, kuhitimisha mjadala wa kikatiba," Rais Hollande ametangaza rasmi Jumatano hii katika Ikulu ya Elysee katika tangazo la dakika tano.
Miezi minne baada ya kupongezwa na karibu wabunge wote mjini Versailles, Rais Hollande "anaona leo kwamba Bunge na Seneti wameshindwa kuafikiana na maelewano yanaonekana kutofikia juu ya ufafanuzi wa kunyang'anywa uraia kwa magaidi. "
"Pia naona kwamba sehemu moja ya upinzani inapinga marekebisho yoyote ya kikatiba, ambayo yanahusu hali ya tahadhari au hata uhuru wa vyombo vya sheria. Ninasikitishwa na tabia hii. Kwa maana tunapaswa kufanya chochote kile katika mazingira tunayojua, na ya hatari, ili kuepuka mgawanyiko na kuzuia hali ya sintofahamu ambayo ingeliweza kutokea kwa wakati wowote", Rais Hollande ameeleza. Hata hivyo hakutaja mjadala ulioibua mgawanyiko katika chama cha mrengo wa kushoto na kusababisha kujiuzulu kwa Christiane Taubira, aliyekuwa Waziri wa Sheria.
Wiki iliyopita, Baraza la Seneti lenye wajumbe wengi kutoka mrengo wa kulia,, lilitupilia mbali hoja ya kunyang'anywa uraia kwa Wafaransa wenye asili ya kigeni pekee, ikibaini kwamba hali hiyo inaweza kuzua mkanganyiko na ubaguzi kwa wananchi wa Ufaransa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Obama apunguza adhabu za wafungwa 61



Rais wa Marekani Barack Obama akimsalimu mfungwa wa zamani mjini Washington, Machi 30, 2016.
Rais wa Marekani Barack Obama akimsalimu mfungwa wa zamani mjini Washington, Machi 30, 2016.
NICHOLAS KAMM/AF

Rais wa Marekani Barack Obama, Jumatano hii, amepunguza adhabu zilizokua zikiwakabili wafungwa 61 waliohukumiwa kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya. Hili ni tukio la kihistoria wakati ambapo amekua akishawishi wahusika katika sekta ya sheria kufanya mageuzi ya kijinai kuhusu makosa madogo madogo.

Obama amepunguza adhabu za wafungwa 61, waliokua wamehukumiwa kuanzia kifungo cha maisha hadi adhabu ndogo ndogo gerezani kwa kumiliki au kuuza madawa ya kulevya kama Crak au cocaine, Ikulu ya White House imetangaza.
Barack Obama, ambaye anafikia mwishoni wa muhula,amekua akizidisha juhudi kama hizi. Mwezi Desemba, alipunguza adhabu kwa wafungwa 95 wa Marekani.
Hivi karibuni alipunguza adhabu kwa wafungwa 248 waliohukumiwa, na baadhi yao walipewa msamaha, na Jumatano hii anatazamiwa kukutana na wafungwa wengine.
Rais wa Marekani, kwa muda mrefu, amekua akiomba mageuzi ya sheria za jinai, akilaani jinsi magereza yamekua yakijaa wafungwa na hivo kusababisha vitendo viovu sugu, kutokana na kuzuiliwa kwa kipindi kirefu katika magereza.
Bw Obama alitoa mfano wa ahadi yake ya mageuzi kwa kutembelea mwezi Julai katika jela moja nchini Marekani, ikiwa tukio la kwanza kuwahi kutokea kwa Rais aliye madarakani nchini Marekani.
Watu milioni 2.2 wanazuiliwa katika magereza tofauti nchini Marekani na Rais Obama amesema akisisitiza kwamba Wamarekani wanawakilisha "5% ya idadi ya watu duniani, lakini 25% ya watu wanaozuiliwa gerezani duniani", ikiwa ni pamoja na watu weusi na watu kutoka jamii ya Hispanics.
Miongoni mwa watu wanaozuiliwa gerezani nchini Marekani, zaidi ya nusu walihukumiwa kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya, imebaini mwezi Oktoba tathmini ya Idara ya Takwimu ya vyombo vya sheria iliyofanywa mwaka 2012 katika sampuli ya mahabusu 94,678
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

DRC: Moïse Katumbi atawazwa kuwa "mgombea wa urais"



Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga Moïse Katumbi katika mahojiano mjini Lubumbashi, Juni 2, 2015.
Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga Moïse Katumbi katika mahojiano mjini Lubumbashi, Juni 2, 2015.
AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kamati kuu ya muungano wa vyama 7 vya upinzani G7 imemteua rasmi Jumatano hii mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga, Moïse Katumbi kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais kwa tiketi ya muungano huo.

Vyama hivi vilioondolewa hivi karibuni katika muungano unaounga mkono chama tawala cha PPRD.
Bila ubishi wowote, Moïse Katumbi ameteuliwa rasmi kuwa mgombea wa G7 katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Tangazo hili limetolewa Jumatano Machi 30 baada ya mkutano wa kamati kuu ya muungano unaojumuisha vya saba vya upinzani vilioondolea serikalini, uliofanyika mjini Kinshasa. Vyama hivi viliondolewa katika muungano wa vyama vinavyokiunga mkono chama tawala cha PPRD, baada ya kuonyesha msimamo wao wa kupinga muhula wa tatu wa rais Joseph Kabila.
G7 imemuomba Moïse Katumbi kushiriki uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika Novemba 27.
Siku moja kabla ya uteuzi huo, mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga alikua amesha jiandaa kuwania katika kinyang'anyiro hicho, ambapo alikemea vikali mjini Lubumbashi, kusini mwa nchi hiyo "uchaguzi wa Wakuu wa Mikoa" ambao aliutaja kuwa "uligubikwa na kasoro nyingi".
Hata hivyo Katika mkoa huo mpya wa Katanga, muungano wa vyama vilio serikalini vilipata ushindi katika uchaguzi wa wakuu wa Mikoa uliofanyika Machi 26, huku wagombe wa muungano wa G7 wakibatilishwa na Tume Huru ya Uchaguzi, kwa "ombi la moja kwa moja" la muungano wa vyama vilio serikalini, jambo ambalo Moïse Katumbi, alikemea pia, akibaini kwamba hiyo ni moja ya dalili zinazoonyesha "jinsi gani sheria zinadidimizwa na demokrasia kotoendelea nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo".
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Libya: Tripoli katika hali ya taharuki baada ya kuwasili Waziri Mkuu



Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Machi 30, 2016.
Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli, Machi 30, 2016.
AFP


Nchini Libya, Waziri Mkuu aliyeteuliwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa hatimaye aliwasili Jumatano Machi 30 katika mji wa Tripoli.

Kuwasili kwa Fayez el-Sarraj kumesababisaha kuzorota kwa hali ya usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo. Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya, Marekani, Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa wamekaribisha ujio wa Waziri Mkuu wa Libya katika mji wa Tripoli.
Hata hivyo serikali hiyo inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, inapingwa na serikali mbili sambamba, zisiotambuliwa na jumuiya hiyo: serikali moja ina makao yake makuu katika mji wa Tripoli na nyingine katika mji wa Tobruk. Hali ya mvutano ilijitikeza Jumatano jioni kati ya wanamgambo baada ya kuwasili kwa kiongozi huyo mjini Tripoli kwa njia ya bahari.
Kulisikika milio ya risasi katika maeneo mbali mbali ya mji mkuu wa Libya, Tripoli baaada ya kuwasili kwa Waziri Mkuu Fayez Seraj pamoja na mafaasa wengine wa serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa.
Waziri huyo Mkuu wa Libya amekaribishwa na milio ya risasi, huku msafara wake ukikumbana na upinzani mkali kutoka kundi lililojitangazia madaraka linalodhibiti mji wa Tripoli likikidai kuja kwao ni jaribio la mapinduzi.
Serikali isiyotanbuliwa na jumuiya ya kimataifa katika mji mkuu wa Tripoli imekua ikibaini kwamba mipango inayofanywa na baraza la rais ni jaribio la mapinduzi. Baadhi ya mawaziri na maafisa wengine wa serikali hiyo wamesema watu hao wakamatwe.
Kituo cha televisheni cha libya Al Naab kimeshambuliwa na watu wenye silaha. Mpaka sasa kituo hicho kimefungwa na kimezuia kutangaza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault amewasihi wananchi wa Libya kuwa na umoja na kudumisha amani kwa maslahi ya taifa lao.
"Nchi zote katika ukanda huo wanatarajia hali mpya ya kisiasa nchini Libya kwa sababu ni suala muhimu, ni suala la usalama, vinginevyo kundi la Islamic State linaendelea kujidhatiti," Bw Ayrault amesema.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.