Sunday, June 26, 2016

SIMBA YAJIBU MAPIGO YA YANGA




Haji Manara-Afisa habari Simba SC
Haji Manara-Afisa habari Simba SC
Awali ya yote klabu inaendelea kutoa pongezi kwa ndugu zetu Waislaam wanaoendelea kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani tunaamini Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kwa ibada hiyo muhimu.
Ndugu wanahabari katika siku za karibuni hususan kuelekea mchezo wa Yanga na klabu kutoka Congo DRC  TP Mazembe Englebert kumekuwa na maneno mengi kutoka klabu ya Yanga yakiishutumu klabu yetu kuhusiana na kutokutoa ruhusa kwa mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ na pia kuhusiana na namna mashabiki watakavyokaa majukwaani siku ya mchezo huo Jumanne ya wiki hii.
Klabu ya Simba kwa maksudi kabisa inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na mambo hayo mawili yanayoleta sintofahamu miongoni mwa wadau wa mchezo huu murua wa kandanda.
Hakuna barua yoyote ambayo klabu ya Yanga imetuandikia kuhusiana na suala la mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ pia hakuna hata mazungumzo yaliyofanyika baina ya viongozi wa vilabu hivi ili kutuomba walau kwa mdomo kama taratibu zinavyotaka.
Ikumbukwe Simba huwa haina tatizo kuruhusu matakwa binafsi ya mchezaji na nyote mnajua utamaduni huo wa klabu yetu.
Kwa wasiofahamu mwaka 1998 klabu ya Simba iliwaazima wachezaji watatu Yanga ili wacheze hatua ya makundi kama hii ya klabu bingwa Afrika wachezaji hao ni Shaban Ramadhani Monja Liseki na Alphonse Modest sasa jiulize kama tuliweza kuwaazima wachezaji vipi tushindwe kumruhusu mchezaji waliyemsaini? Pamoja na maneno yao ya kuudhi Simba ni waungwana wa kutosha na wao wasitumie ukimya wetu kuwapotosha wanachama na washabiki wao eti tumewakatalia kuwajibu barua ya Hassan Ramadhani ‘Kessy’
Msimamo wetu kuhusiana na jambo hili inategemea uungwana wao tu.
Pia Yanga kupitia msemaji wao wamenukuliwa kuwa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe watakaa kwenye majukwaa yote hata yale ambayo kwa utamaduni wa uwanja wa taifa hukaliwa na mashabiki wa klabu yetu.
Tunafahamu kuwa kauli hii ina nia ya kuchochea vurugu kubwa kwenye mchezo huo na sote tunajua athari ya vurugu michezoni tunawashauri Yanga wasijaribu kuleta mashabiki wao kwenye majukwaa wanayokaa washabiki wa Simba ili kuleta amani siku hyo ya mchezo.matarajio yetu vyombo vinavyohusika vitasimamia kwa ukaribu jambo hilo.
Mwisho ingawa si kwa umuhimu klabu haimzuii yoyote kushangilia timu yoyote siku ya mchezo huo kama zilivyo desturi ya wao Yanga kushangilia klabu yoyote inayocheza na Simba hususan wageni toka nje.kama ilivyokuwa miaka michache nyuma ambapo walishangilia na kuvaa jezi za TP Mazembe.
Waarabu wana msemo wao maarufu “KAMA TUDINI TUDANI” kama ulivyofanya na wewe utafanyiwa hivyohivyo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Waethiopia 19 wapoteza maisha ndani ya lori la wasafirishaji haramu wa watu:IOM


Wakimbizi wa kutoka Ethiopia na Eritrea amabo wanaokolewa na wafanya kazi wa IOM.(Picha:© IOM 2015)
Takribani Waethiopia 19 wamekutwa wamekufa ndani ya lori nchini Zambia baada ya kukosa hewa . Lori hilo linasadikiwa kuwa ni la mtandao wa usafirishaji haramu wa binadamu na lilikuwa likielekea Afrika ya Kusini.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM , wahanga hao walikutwa baada ya manusura kugongagonga kontena walimokuwa wakihitaji msaada. Msemaji wa IOM Joel Millman amesema tukio hilo ni baya sana kulishuhudia.
(SAUTI YA JOEL MILLMAN)
"Hili ni kubwakabisa tunalolifahamu, lakini kumekuwa na visa vingine vya kutisha kwatika safari hizo siku za nyuma.Nadhani ilikuwa mwaka jana au miwili iliyopita kulikuwa na tukio la wahamiaji kuzama, ambao walishuhudiwa wakiliwa na mamba, lakini hatujawahi kuona vifo vya kukosa hewa kwenye kontena kama hivi"
Kwa mujibu wa IOM manusura 76 waliojumuisha watoto, wamepelekwa kwenye makazi ya dharura.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Ban ahuzunishwa na mapigano Sudan Kusini


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Sudan SPLA na vikundi vyenye silaha mjini Wau,  na maeneo jirani  nchini Sudan Kusini.
Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu akisema kuwa amesikitishwa na taarifa za vifo kufuatia machafuko hayo.
Amevitaka vikosi kinzani kusitisha uhasama hima, kuruhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kufika katika maeneo hayo na kushirikiana na wadau wa misaada ya kibinadamu ili kuwezesha ufikishwaji wa misaada.
Ban amezitaka pande hizo kukubali majadiliano ili kutatua mizozo yao ya kisiasa huku pia akipongeza UNMISS na timu ya misaada ya kibinadamu nchini humo kwa hatua za kulinda raia wanoakimbia mjini Wau.
UNMISS iko katika mchakato wa kutuma vikosi zaidi ili kukabiliana na dharura
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Umuhimu wa mabaharia utambuliwe : IOM


Baharini kwa wote ni kauli mbiu inayotumika kwa ajili ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya mabaharia leo Juni 25, 2016.
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, linaadhimisha siku hii kwa mara ya sita kwa kuangazia umuhimu wa mabaharia katika bahari duniani ambapo Katibu Mkuu wa IOM Kitack Lim amekaririwa akisema mabaharia hawatambuliwi huku wakitimiza jukumu muhimu la kuisongesha dunia.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wa kuadhimisha siku hii amesema mabaharia wanalisha dunia, huvalisha na kuihifadhi.

Ban amesema wana umuhimu katika kukuza uchumi jumuishi na aunaojali mazingira.
Sherehe za siku ya mabaharia zitafanyika rasmi Septemba 29 ambayo ni siku ya kimataifa ya masuala ya bahari,ambapo umuhimu wa dhana hiyo utamulikwa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Habari za wiki Hapa na pale Vipindi Taarifa maalumu Kuhusu Idhaa Hati ya mtumiaji 25/06/2016 Jumuiya ya Ulaya chondechonde wathaminini wakimbizi,wahamiaji: Ban


Ban Ki-moon akiwatia moyo wakimbizi nchini Ugiriki. Picha na Rick Bajornas wa UMAkiwa ziarani nchini Ufaransa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisisitiza kuwa uamuzi wa Uingereza kujitoa katika jumuiya ya Ulaya EU, haupasiwi kuwa mzigo kwa wakimbizi, wahamiaji na wasaka hifadhi barani humo.
Akizungumza na vyombo vya habari akiwa ameambatana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande, Ban amesema anatarajia nchi za Ulaya zitaheshimu sheria za  kimataifa na kuonyesha ubinadamu kwa makundi hayo yasiyo na hatia.
Akitolea mfano Katibu Mkuu amesema juma lililopita alitembelea kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki ambapo alikutana na kushuhudia madhila ya wakimbizi kutoka Syria, na Iraq.
Amesema wakimbizi hao ambao waliosafiri safari zisizo salama za muda mrefu ni wachovu na wanachotaka ni uslama na watoto wao, elimu na ajira ili waweze kushiriki katika maendeleo
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mke wa Rais Obama ziarani barani Afrika


 media
Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi barani Afrika, Jumapili hii, akiambatana na watoto wake, Sasha na Malia, ziara ambayo ni sehemu ya juhudi zake za kuhamasisha elimu kwa mtoto wa kike.
Ziara hii ya siku sita barani Afrika, itashuhudia mke wa rais Obama, akisafiri kwenye nchi za Morocco na Liberia, ambapo pia atasafiri hadi Hispania.
Ziara ya Michelle Obama imebeba ujumbe wa "Waache wasichana wasome", ilizinduliwa na Serikali ya Marekani kupitia rais Barack Obama na mkewe mwenyewe mwaka 2015.
Mradi huu ni sehemu ya Serikali ya Marekani katika juhudi zake za kueneza elimu na kuondoa vikwazo ambavyo vinawazuia zaidi ya wasichana milioni 62 duniani kutokwenda shule.
Kwenye ziara hiyo, Michelle atasindikizwa na muigizaji, Meryl Streep na Freida Pinto nchini Morocco, ambako watazungumza na wasichana wadogo kuhusu changamoto zinazowakabili kupata elimu, ilisema taarifa ya ofisi ya mke wa rais.
Akiwa nchini Liberia, atatembelea kituo cha Marekani cha wafanyakazi wa Marekani wanaojitolea, pamoja na shule moja ya wasichana akiambatana na rais wa Liberia, Ellen Johansson Sirleaf, mwanamke wa kwanza Rais aliyechaguliwa kidemokrasia na mshindi wa tuzo la Nobel.
Nia ya Michelle Obama kuwasaidia wasichana kupata elimu, ilizidi baadaya tukio la kutekwa nyara kwa wasichana zaidi ya 200 wa Chibok kaskazini mwa Nigeria, mwezi Aprili mwaka 2014, ambapo aliandika kwenye mtandao wake #BringBackOurGirls.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Watu 11 wauawa katika shambulizi la Al Shabab mjini Mogadishu



media Shambulizi katika Hoteli ya Naasa Hablood mjini Mogadishu Somalia 25 06 2016 REUTERS/Feisal Omar
Takriban watu 11 wameuawa jana Jumamosi katika shambulizi kwenye hoteli ya mjini Mogadishu nchini Somalia ambalo linadaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab.
Shambulizi hilo ambalo ni la karibuni katika mfululizo wa mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la Al Shabab kulenga hoteli na migahawa, lilianza wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alipolipua bomu lililokuwa limetegwa garini nje ya jengo la hoteli.
Watu wenye silaha walivamia hoteli iitwayo Naasa Hablood na milio ya risasi ilisikika kwa saa kadhaa, mashahidi wamesema, kabla ya mamlaka kutangaza mashambulizi kumalizika.
Vikosi maalum vya usalama vimekomesha shambulizi hilo baada ya kuwaua washambuliaji watatu ndani ya hoteli.
Msemaji wa wizara ya usalama Abdi Kamil Shukri, amewaambia waandishi wa habari kuwa raia kumi na mmoja, wawili kati yao madaktari, wameuawa katika shambulio hilo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Maswali matano kwa Uingereza na EU baada ya kujitoa


Waingereza walipiga kura ya maoni Alhamis (23.06.2016)kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya. Yafuatayo ni majibu kwa maswali muhimu juu ya kitu gani kitatokea baadaye katika uhusiano kati ya Uingereza na kundi hilo la mataifa.
Euromaxx Brexit Großbritannien Bendera ya Uingereza
Umoja wa Ulaya umo katika mshituko na unaingia katika neo ambalo bado hailijui. Hakuna mwanachama ambaye aliwahi kujitoa na kifungu cha 50 cha mkataba wa Ulaya, ambao unaweka utaratibu wa nchi kujitoa, unatoa maelezo machache.
Licha ya kuwa unatoa maelezo ya juu juu ya kisheria kwa kipindi cha miaka miwili cha kujiondoa, wengi wanaamini itachukumua muda mrefu kuweza kuweka uhusiano mpya wa kibiashara kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya na baadhi wanahofia kuwa hatua hizo zitakuwa ngumu, zitakazoleta mvurugiko wa uchumi na masuala ya Ulaya kwa pande zote.
Brexit Nigel Farage Mwanaharakati aliyefanya kampeni ya kijitoa Nigel Farage
David Cameron alisema atajiuzulu ifikapo Oktoba mwaka huu na kumwachia mrithi wake kuwa kiongozi wa chama cha Conservative kuufahamisha Umoja wa Ulaya kwamba Uingereza inajitoa kupitia maelekezo ya kifungu cha 50.
Hali hiyo itauweka muda wa miaka miwili wa kukimbizana, na Umoja wa Ulaya wenyewe hauwezi wanaamini maafisa, kuanzisha hatua hiyo wenyewe. Baadhi katika Umoja wa Ulaya wanataka mchakato kuanza hata haraka zaidi wakati Cameron akizungumza na viongozi wa Umoja wa Ulaya katika mkutano siku ya Jumanne wiki ijayo, na wana wasiwasi juu ya taarifa kutoka kwa waliofanya kampeni ya kujitoa kwamba wangependelea kuanzisha majadiliano mapya kabla ya kufikia kifungu 50 cha kujitoa.
Infografik Brexit Wahl nach Altersgruppen Russisch Jinsi watu walivyopiga kura kulingana na umri nchini Uingereza
Mrithi mtarajiwa
Mrithi mtarajiwa wa Cameron, Boris Johnson alisema haoni sababu yoyote kuanza mchakato huo na kwamba hakuna kinachohitajika kubadilika katika kipindi hiki kifupi.
Makubaliano aliyoyapata Cameron na viongozi wa Umoja wa Ulaya mwezi Februari kudhibiti uhamiaji, kulinda maslahi ya kifedha ya Uingereza kutoka kanda ya euro na kujitoa kutoka katika "umoja wa karibu zaidi" yamekufa kutokana na matokeo ya kura hiyo ya maoni na viongozi wa Umoja wa Ulaya wameondoa uwezekano wa mazungumzo mapya katika utaratibu mpya wa uanachama wa Uingereza katika Umoja wa Ulaya "kuondoka maana yake kuondoka."
Wengi wanataka kuvunjika kwa haraka kwa ndoa katika muda wa miaka miwili, wakati majadiliano kuhusiana na masharti kwa ajili ya hali ya baadaye ya uhusiano wa mbali huenda yakachukua muda mrefu zaidi.
Kipindi cha mpito
Hata hivyo, Ujerumani, hususan ina nia ya kuona utaratibu mzuri wa kipindi cha mpito kuwa na uwezekano wa uhusiano mpya.
Brexit Angela Merkel Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akilihutubia taifa baada ya kura nchini Uingereza
Hii itahusisha majadiliano mapya ya kifungu 50, ambacho mkataba unasema , kinapaswa "kuchukuliwa maanani" kuhusiana na uhusiano kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya, ukirefushwa kupindukia miaka miwili ili kuruhusu muda zaidi wa kupatikana makubaliano mapana zaidi.
Urefushwaji wa aina hiyo unahitaji ridhaa ya mataifa 28 wanachama, na kufikia kauli hiyo ya pamoja inaweza kuwa na matatizo.
Pamoja na hayo, wanasheria wa Umoja wa Ulaya na wanasiasa wanatambulika kwa kutokuwa wakweli. Afisa mmoja wa Umoja wa Ulaya alisema kwamba mkataba wa kuvunja ndoa unahitaji wingi mdogo tu na makubaliano yanaweza kufikiwa kwa muda wa miaka miwili lakini kuanza rasmi ni baada tu ya makubaliano ya pili kuanzisha uhusiano mpya yatakapokamilika.
Brexit Reaktionen Geert Wilders Kiongozi wa siasa za mrengo mkali wa kulia Geert Wilders wa Uholanzi akifurahia matokeo ya kura ya maoni Uingereza
Kuna idadi kubwa ya njia zilizowazi kwa Uingereza , ikiwa ni pamoja na kuendelea na matumizi ya soko la Umoja wa Ulaya katika utaratibu kama wa Uswisi na Norway, licha ya kuwa viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesema gharama ya hali hiyo inaweza kuruhusu uhamiaji huru katika Umoja wa Ulaya na kukubali sheria nyingine za Umoja wa Ulaya ambapo wapiga kura wa Uingereza wamezikataa katika kura ya maoni.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Vita vyaendelea Sudan Kusini



Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Monn anasema ana wai wasi mkuwa kufuatia kuendelea kwa mapigano nchini Sudan Kusini.
Kumeripitiwa mapigano nje na ndani ya mji wa Wau, kati ya wanajeshi ya serikalia na makundi yaliyojihami tangu Ijumaa.
Haijulikani wapiganaji hao ni akina nani.
Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa maelfu ya raia wamekimbia na pia kuna ripoti za uporaji na vifo.
Hali ni tete nchini Sudan Kusini licha ya kuundwa kwa serikali ya umoja, yenye lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 2013.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mrithi wa Cameron nani na lini ?


Uamuzi wa waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kujiuzulu baada ya kushindwa katika kampeni ya kuibakisha Uingereza katika Umoja wa Ulaya umezusha mchuano wa kuwania wadhifa huo katika chama cha Conservative.
Brexit David Cameron Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
Mchakato umeshanza wa kumtafuta mrithi wake na mshindi atachukua nafasi yake katika mtaa wa Downing namba 10.
Tayari Cameron amekwisha sema kwamba atajiuzulu kabla ya uchaguzi ujao mwaka 2020, na wabunge kadhaa wa chama cha Conservative wamejiweka tayari kuwa warithi wake.
Großbritannien London Demonstration gegen Brexit Maandamano ya kuunga mkono Umoja wa ulaya Uingereza
Waziri mkuu ajaye wa Uingereza atakuwa na jukumu la kufanya majadiliano ya kuitoa nchi hiyo kutoka Umoja wa Ulaya.
Hizi ndio hatua muhimu zinazofuatia kujiuzulu kwake.
Cameron aliitisha kura ya maoni na kufanya kampeni kwa nguvu zote ya "kubakia" katika kura ya maoni iliyofanyika siku ya Alhamis, kwa hiyo kuondoka kwake kulikuwa hakuzuiliki, lakini ni mwisho wenye kudhalilisha katika muda wake wa kazi.
Cameron mwenye umri wa miaka 49 alikuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo kabisa nchini Uingereza mwaka 2010 , katika muda wa miaka 200 iliyopita, na mwaka jana alichaguliwa tena kwa wingi mkubwa wa chama cha Conservative.
Brexit Boris Johnson Boris Johnson meya wa zamani wa London
Cameron atakabidhi uongozi na funguo ya nyumba ya mtaa wa Downing utakapofanyika mkutano wa chama hicho mwezi Oktoba.
Anakiacha chama kikiwa kimegawanyika mno, ambapo sita kati ya mawaziri wake na wabunge 128 kati ya wabunge 330 wa chama chake cha kihafidhina wakiwa wameunga mkono kujitoa.
Kamati ya wabunge waandamizi
Kamati ya wabunge waandamizi wa chama hicho cha kihafidhina watakutana Jumatatu kuanza rasmi mchakato wa kumpata kiongozi.
Britischer Bildungsminister Michael Gove Michael Gove waziri wa sheria wa Uingereza
Watu wanaotarajiwa kuwania wadhifa huo ni hawa.
Boris Johnson, ambaye aliongoza kampeni ya kujitoa, ndie aliyetia nguvu zaidi kampeni ya kujitoa. Meya huyo wa zamani wa mji wa London mwenye umri wa miaka 52 amejijengea umaarufu kwa watu wengi wenye shaka na Umoja wa Ulaya miongoni mwa wapiga kura wa chama cha Conservative.
Michael Gove: Ni waziri wa sheria na rafiki mkubwa wa David Cameron na uamuzi wake wa kumkana na kufanya kampeni ya kujitoa ilikuwa ni pigo kwa waziri mkuu.
Theresa May, ni waziri wa mambo ya ndani na aliepuka vita vya ndani ambavyo viligubika kampeni hiyo, na hatua hiyo inampa nafasi adimu kuwa mmoja kati ya wale wanaoweza kumrithi Cameron.
Großbritannien Theresa May Theresa May waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza
George Osborne, ni waziri wa fedha ,na mshirika wa karibu wa Cameron , na amekuwa kwa muda mrefu akitajwa kuwa na uwezekano wa kumrithi waziri mkuu, lakini uungaji wake mkono kura ya "kubakia" umewakasirisha wengi wa wapiga kura wa chama hicho.
Merkel atuliza mzuka
Wengine wanaoangaliwa kuwa na uwezekano wa kumrithi Cameron ni pamoja na mawaziri wawili wanaopendelea Umoja wa Ulaya , Nicky Morgan, waziri wa elimu na Stephen Crabb, waziri wa kazi na mafao ya uzeeni.
Nchini Uingereza wapiga kura wanakichagua chama na sio waziri mkuu, kwa hiyo mabadiliko ya juu ya uongozi hayahitaji kuitishwa uchaguzi mpya.
Brexit Angela Merkel Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Wakati huo huo kansela wa Ujerumani Angela Merkel alijaribu jana Jumamosi (25.06.2016) kupunguza mbinyo kutoka Paris, Brussels na serikali yake kuilazimisha Uingereza kuingia katika mazungumzo haraka ya kuvunja ndoa kati ya Umoja wa ulaya na Uingereza, licha ya onyo kwamba kusitasita kutasababisha hisia za kizalendo kuota mizizi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mawaziri wa Leba kujiuzulu Uingereza



Image caption Jeremy Corbyn
Hali ya wasiwasi iliyoanzishwa na upigaji kura wa Uingereza kuondoka Jumuiya ya Ulaya (EU) imekumba chama kikubwa cha upinzani cha Leba.
Nusu ya Baraza la Mawaziri la upinzani linatarajiwa kujiuzulu hii leo likilalamikia jinsi kiongozi wao Jeremy Corbyn alivyoongoza kampeni ya kura za maoni.
Wa kwanza kuondoka alikuwa Waziri wa Afya, Heidi Alexander, aliyesema kuwa Bwana Corbyn hana kipaji cha kushughulikia matatizo yanayokumba Uingereza kwa wakati huu.
Awali, Waziri wa upinzani wa Mashauri ya Kigeni, Hilary Benn, aliachishwa kazi kwa kile Bwana Corbyn alidai kuwachochea wenzake waondoke katika baraza hilo iwapo Bwana Corbyn, atakataa kuheshimu mswada wa kutokuwa na imani kwake.
Wafuasi wengi wa Leba walipiga kura kwa Uingereza kujiondoa katika Jumuiya ya Ulaya.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Belle 9 Feat. Izzo Bizness, Jux, G Nako, Mr Blue, Maua Sama - Burger Movie Selfie RMX (Official VIDEO)


Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mr Blue Ft Alikiba - Mboga Saba (Video)


Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Breaking News: Orodha Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Ufundi Kwa Mwaka 2016



OR-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. 

Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. 

Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. 


Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI


Tumia link hii kupata matokeo Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya June 26




Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Friday, June 24, 2016

Tanzania kutengeneza ndege aina ya helikopta


Image caption Ndege aina ya helikopta
Raia nchini Tanzania wameamkia habari za kushangaza kwamba taifa hilo linaunda ndege.
Gazeti la Tanzania la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa barani Afrika kwa kasi.
Gazeti la Zambia, Observer linasema kuwa lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana na matatizo ya uchukuzi nchini humo.
Huku gazeti la Cameron, Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka.
Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania kulingana na Daily News
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Trump apongeza kuondoka kwa Uingereza


Image caption Donald Trump
Mgombea kiti cha urais nchini Marekani Donald Trump amepongeza hatua ya raia wa Uingereza kujiondoa katika muungano wa Ulaya akisema "wamekomboa nchi yao".
Amesema hayo alipowasili Trump Turnberry kwa ufunguzi wa mgahawa wa Ayrshire na ukumbi wa gofu,baada ya kufanyiwa ukarabati.
Kuna madai kuwa alinunua Hoteli hiyo kwa kima cha pesa ambazo hazikutajwa mwaka 2014.
Ufungamano wa kibiashara baina ya Scotland na bilionea huyo wa Marekani ulianza muongo mmoja uliopita alipoahidi kudumisha urithi wa mamake Mary MacLeod, aliyezaliwa Stornoway mwendo mfupi kutoka eneo la Hebrides.
Bwana Trump ambaye anasifika kwa kumiliki hoteli nyingi za kifahari pamoja na nyanja za gofu nchini Marekani pia alifungua moja ya Hoteli hizo nchini Uingereza katika jimbo la Menie mjini Aberdeenshire,mwaka 2012 baada ya mzozo juu ya mipango na masuala ya mazingira ambayo yalipingwa na wenyeji waliokataa kuhama.
Maandamano dhidi mgombea huyo wa urais wa Marekani wa chama cha Republican yanatarajiwa, kutoka kwa wale wanaomlaumu kwa ubaguzi wa rangi.
 
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Waziri mkuu wa Uingereza ajiuzulu



Image caption Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.
Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.
Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.
Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Bwana Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Image caption Bwana Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Sauti yake iliibua hisia hasa aliposena naipenda saana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda huo wote.
Bwana Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.
Cameron akiwa ameandamana na mkewe amesema bila shaka sasa utawala mpya unahitajika utakaoweza kutathmini mbinu na mkataba wa kujiondoa kutoka kwa muungano huo wa bara Ulaya
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Kama ni mtumiaji wa YouTube katika simu, wametangaza maboresho mapya


Kama wewe ni mmoja kati ya watumiaji wa mitandao kwa kutumia smartphone yako, basi mtandao wa YouTube umetangaza maboresho katika application yao kwa watumiaji wa simu za mkononi.
YouTube wametangaza kuboresha application yao ya YouTube inayotumika katika smartphone, sasa unaweza kuweka video za YouTube live streaming kupitia simu ya mkononi, unachotakiwa kufanya ni kubonyeza button katika simu yako na video unayorekodi moja kwa moja itaenda YouTube.
YouTubeConnect1-Cropped
Maboresho hayo ya YouTube kwa application za simu za mkononi, unaweza ukaifananisha na ile application ya mtandao wa Periscope na itakuwa na option ya viewers kuweka comment zao kama kawaida. Mfumo huo wa live streaming kwa simu za mkononi wa YouTube unaitwa ‘YouTube Connect’
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

AUDIO: Wimbo wa Papa Wemba ft Diamond Platnumz umeachiwa leo June 24 2016


Legend wa muziki wa dansi Afrika Papa Wemba daima hawezi kusahaulika, licha ya kuwa tayari alishatangulia mbele za haki, Diamond Platnumz ni moja kati ya wasanii waliopata bahati ya kufanya wimbo na Papa Wemba miezi michache kabla ya kufariki, wimbo wao umetoka leo Papa Wemba ft Diamond ‘Chacun Pour Soi’
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Thursday, June 23, 2016

Rais Magufuli kaeleza hizi sababu za kusitisha ajira mpya


June 22 2016 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amehutubia katika Jubilei ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliyofanyika katika ukumbi wa Benki hiyo, mtaa wa Mirambo Jijini Dar es salaam.
Katika hotuba yake Rais  Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda mfupi usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa…..
>>>’lengo lake ni kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya haitazidi miezi miwili hatutaajiri mtumishi yeyote serikalini pia hatutatoa promosheni ili tufanye ukaguzi wote ili kusudi ndani ya serikali tuondoe hili tatizo la wafanyakazi hewa’
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.



Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali ombi la kumuachia huru mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel 10 mkoani humo, Daudi mwangosi na badala yake imesema ana kesi ya kujibu.

Akitoa uamuzi wa ombi hilo mahakamani hapo jana, Jaji Paulo Kihwelo, alisema mahakama imeona mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu na anatakiwa  kupeleka mashahidi makamanani.
 
Akizungumzia uamuzi huo, wakili wa upande wa utetezi, Rwezaura Kaijage, alisema wameridhika na watatoa ushahidi wakiwa na shahidi mmoja ambaye ni mtuhumiwa mwenyewe.
 
“Utetezi tumeridhika na uamuzi wa mahakama, shahidi atakuwa mmoja na ni mtuhumiwa mwenyewe, lakini tunaiomba mahakama yako tukufu ushahidi huo utolewe kwa njia ya kiapo,” alisema.
 
Kaijage aliomba utetezi huo utolewe leo kuanzia saa 3: 00 asubuhi. Kwa upande wa wakili wa Jamhuri, Ladislaus Komanya na mwenzake Sunday Hyera, walisema hawana pingamizi lolote la ombi hilo kuwa utetezi utolewe leo.
 
Ulinzi Mkali Mahakamani
Kabla ya Jaji kuingia kwenye chumba cha mahakama, ulinzi mkali wa polisi ulitawala nje na ndani ya mahakama, wakiwamo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuzingira eneo hilo.
 
Aidha, waandishi wa habari walipata wakati mgumu kutekeleza kazi yao baada kunyimwa kuingia ndani ya chumba cha mahakama kwa kisingizio kuwa kesi haijaanza, hali iliyolazimu Msajili wa Mahakama hiyo, Ruth Massam, kuingilia kati na kuwataka polisi kuacha lakini hawakumsikiliza.
 
Baada ya mvutano huo, waandishi walikaguliwa na kisha kuruhusiwa kuingia, lakini hali iliendelea kuwa ngumu ndani ya chumba cha mahakama kiasi cha kutishiwa kuvunjiwa vitendea kazi vyao na baadhi ya polisi.
 
Hata hivyo, waaandishi waliendelea kutekeleza majukumu yao hadi kesi ilipoanza.
 
Baada ya Jaji Kihwelo kuahirisha kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani kimgongo mgongo ili asionekane sura, huku askari wenzake wakimfunika kwa kitambaa na kitenge kichwani, pamoja na bahasha ya kaki. Askari zaidi ya 30 walimzingira ili asipigwe picha.
 
Mwangosi aliuawa Septemba 2, 2012 kwenye ufunguzi wa matawi ya Chadema katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova Aagwa...... Aomba kazi Tena Polisi


Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, ameliomba jeshi hilo kumpa kitengo cha masoko ili aweze kulitangaza na kuliunganisha na wananchi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maboresho ndani ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.

Kova alitoa ombi hilo jana mjini Moshi katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Shule ya Polisi Moshi (MPA).

Alisema jeshi hilo linaelekea kuzindua mpango wake wa matokeo makubwa sasa (BRN) ,ambao unahitaji msukumo wa jamii katika kusaidia kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali ukiwamo wa mtandaoni na dawa ya kulevya.

Kova alisema kutokana na utumishi wake wa zaidi ya miaka 40 kwa kushirikiana na wastaafu wengine, wanaweza kusaidia na kuwa kiunganishi baina ya polisi na raia kama njia bora ya kukabiliana na uhalifu kwa kutumia kitengo cha masoko.

“Nimekuwa mtumishi ndani ya polisi kwa miaka 40, ninaweza kutumika hata na Shule ya Polisi Moshi kufundisha na hata kutoa uzoefu wangu ambao utalisaidia jeshi katika kukabili uhalifu, kama mnavyoniona ninazo nguvu za kutosha na ninalipenda Jeshi la Polisi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kova aliiomba serikali kuliboresha zaidi jeshi la polisi kwa vifaa, mbinu na teknolojia za hali ya juu ili kukabiliana na matukio ya uhalifu wa aina mbalimbali unaokuwa kulingana na ukuaji wa teknolojia duniani.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.