Thursday, April 7, 2016

Sanaa ya muziki


Sanaa ya muziki
Sevda Elekberzade, ni mwanamuziki wa miondoko ya Jazz aliezaliwa mwaka 1977 mjini Baku nchini Azerbaijan.
Mwanamuziki huyo alianza kujihusisha na muziki wa jazz akiwa bado na umri mdogo.
Mwaka 1988 alianza kujihusisha na masomo ya muziki katika chuo kikuu cha İncesenet ambacho ni chuo kikuu cha serikali ambapo alipa mafunzo ya classic music na kubobea.
Baada ya kuwa mtaalamu wa muziki alijiunga na kundi la Aypar na kuwa mpicharaza gita hodari katika kundi hilo mwaka 1991.
Kundi hilo liliwavutia wapenzi wa muziki kwa kupiga miondoko tofauti ikiwemo miondoko ya kigeni.
Mwaka 2001 aliachana na kundi hilo baada ya kumaliza masomo yake ya muziki wa Jazz.
Sevda akishirikiana na mtunzi wa muziki Cemil Emirov walianzisha mradi wao wa kwanza uliojulikana kama “Deme ki ,Sevirem".
Mwaka 2002 alishiriki katika tamasha la muziki la kimataifa la Jazz na kuonesha ohodari wake.
Kwa jina la Şebi Hicran mwaka 2004 alianza tamasha akiwa pekee na kujitegemea ambapo alitumbuiza “Devlet Filarmoni" .
Mwaka 2005 pamoja na kundi la Bethoven walicharaza kibao kwa jina la “Sevinç Odası" ambacho kilitaarishwa kwa miondoko ya kiazeri na kutolewa kama zawadi.
Nchini Italia kulifanyika maonesho ya muziki wa kiazeri na baadae kuoneshwa nchni Ufaransa.
Katika shindano lililoandaliwa na kituo cha redio ya kimataifa ya Ur-faransa walijipatia ushindi kwa mindoko ya Rock na Pop.
Sevda alifanya tamasha pia mjini Jerusalem na baadae kuweza kuigiza katika filamu.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment