Thursday, April 7, 2016

Mustakhbali wa UNAMID Darfur kuangaziwa wiki ijayo


Mkuu wa Idara ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous.(Picha:UM/ Eskinder Debebe)
Hali ya usalama kwenye eneo la Jebel Marra huko Sudan ikizidi kuzorota kutokana na mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi, mustakhbali wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID utaangaziwa tena wiki ijayo. Priscilla Lecomte na taarifa kamili.
(Taarifa ya Priscilla)
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za ulinzi wa amani, Herve Ladsous amesema hayo wakati akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya UAMID.
Amesema raia wanazidi kukumbwa na zahma, huku UNAMID ikipata vikwazo kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuwafikia wahitaji huko Jebel Marra.
Amesema AU, Umoja wa mataifa na Sudan watakutana wiki ijayo kujadili mpango wa UNAMID kuondoka ambapo..
(Sauti ya Ladsous)
"Hatua muhimu kwenye mchakato huo itakuwa kuandaa vigezo vitakavyokubaliwa kwa kupima maendeleo kwa kuzingatia viwango vya UNAMID kama ilivyoainishwa na azimio la baraza lako namba 2228 na taarifa za Muungano wa Afrika za 22 Juni na 21 Julai 2015."
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment