Wednesday, April 13, 2016

Wananchi wa Syria wajitokeza kushiriki uchaguzi wa Bunge


Wananchi wa Syria wajitokeza kushiriki uchaguzi wa Bunge
Wananchi wa Syria waliotimiza mashari ya kupiga kura wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura mapema leo, kushiriki uchaguzi wa Bunge la nchi hiyo.
Shirika rasmi la habari Syria SANA limeripoti kuwa, vituo vya kupiga kura vimefunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za nchi hiyo na vinatazamiwa kufungwa saa moja jioni hii leo. Hata hivyo Tume ya Uchaguzi nchini humo imesema huenda muda wa kupiga kura ukasogezwa mbele kwa masaa matano iwapo idadi kubwa ya wapiga kura itajitokeza kushiriki zoezi hilo. Wananchi wanatazamiwa kuchagua Wabunge 250, kati ya wagombea 3,500 waliojitokeza kuwania nafasi hizo.
Kuna vituo zaidi ya 7,300 vya kupiga kura katika maeneo ambayo yanadhibitiwa na serikali nchini humo.
Rais Bashar al-Assad wa Syria amekuwa akisisitiza kuwa, mgogoro wa Syria utatatuliwa na wananchi wenyewe na kwamba uchaguzi huu ni moja ya mikakati ya kuupatia ufumbuzi mzozo huo. Kadhalika Rais Assad ameonya kuwa, mpango wowote wa kuifanya nchi hiyo iwe chini ya uongozi wa kifederali hautakuwa na tija kwa taifa hilo. Kwa muda mrefu sasa serikali ya Syria imekuwa ikisisitiza kuwa magaidi nchini humo wanapata misaada ya fedha na silaha kutoka kwa nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifaki wake katika eneo hili ambao ni Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala haramu wa Israel.
Karibu watu nusu milioni wameshapoteza maisha tokea magaidi waanzishe kampeni ya kumuondoa madarakani Rais Bashar al Assad wa Syria mwaka 2011.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment