Saturday, April 2, 2016

SERIKALI YAITANGAZIA NEEMA TTCL



SERIKALI imetangaza azma ya kuifanyia maboresho na mageuzi makubwa kampuni ya simu nchini (TTCL) ili iweze kuendesha kwa ubia mkongo wa mawasiliano ya Taifa. Na kwamba hatua hiyo itaifanya TTCL kuwa moja ya kampuni kubwa za mawasiliano nchini ambayo itatoa huduma zake kwa ufanisi na tija kubwa kwa wateja wa kampuni hiyo.ttclWaziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, aliyasema hayo jana katika maeneo tofauti akiwa kwenye ziara ya kiserikali mkoani Kigoma. Alisema kuwa moja ya maboresho hayo ni mazungumzo yanayoendelea ya kuona namna ya kuipa nafasi kampuni hiyo kuendesha sehemu ya huduma za mkongo huo.

Alisema kuwa kwa sasa hudumu nyingine za kampuni zinaonekana kupoteza wateja wake. Kikubwa alisema kampuni hiyo itafanyiwa maboresho ya kiteknolojia na uendeshaji ili kuendana na zama hizi za sayansi na teknolojia na kwamba maboresho hayo yatairudisha kampuni hiyo kuaminiwa na kutoa huduma zake kwa tija kwa Watanzania na watu wote watakaotumia huduma za kampuni hiyo.

Profesa Mbarawa alisema kuwa miongoni mwa maboresho yatakayofanywa ni kuiongezea masafa kampuni hiyo na kwamba kwa mwaka huu inatarajia kuongezewa masafa 800 ambayo yatakuwa chachu ya kuifanya kampuni hiyo iongeze wateja na huduma zake kuwafikia watu wengi na kwa uhakika.

Awali akitembelea ofisi za kampuni hiyo mjini Kigoma, Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema kuwa nia njema ya serikali kutaka kuimilikisha TTCL sehemu ya uendeshaji wa Mkongo wa Taifa ni jambo lenye tija kibiashara kwa kampuni hiyo

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment