Mamia ya wanafunzi na wakazi wa mji wa Garissa nchini Kenya, wamefanya maandamano ya kulaani hujuma ya kundi la kigaidi la ash-Shabab katika chuo kikuu cha mji huo mwaka mmoja uliopita.
Washiriki wa maandamano hayo yaliyowashirikisha shakhsia mbalimbali wakiwamo viongozi wa serikali, wametoa mwito wa umoja kwa raia wa nchi hiyo Waislamu na Wakristo kuungana katika kukabiliana na kundi la kigaidi la ash-Shabab.
Aidha waandamanaji wamewasha mishumaa kama alama ya kuwakumbuka ndugu na jamaa zao waliopoteza maisha katika hujuma hiyo ya kigaidi ya mwezi Machi mwaka jana.
Shambulio la kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa, ni shambulio kubwa zaidi kuwahi kufanywa nchini Kenya tangu mwaka 1998. Watu 148 waliuwa wengi wao wakiwa wanafunzi wa chuo hicho katika shambulio hilo la kivamizi la ash Shabab.
Ni vyema kuashiria kuwa, kundi la kitakfiri la ash-Shabab ni tawi la mtandao wa kigaidi al-Qaidah nchini Somalia na limefanya mashambulizi kdhaa ya kigaidi nchini Kenya likilenga idara za serikali, askari, magari ya abiria na mahoteli pamoja na shule na vyuo.
No comments:
Post a Comment