Saturday, April 2, 2016

Jeshi la Yemen lakomboa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Taiz



Jeshi la Yemen lakomboa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Taiz
Jeshi la Yemen kwa kushirikiana na vikosi vya wananchi limefanikiwa kukomboa wilaya ya al Wazi'iya ya mkoani Taiz kusini mwa nchi hiyo, kutoka kwa mamluki wa Saudi Arabia.
Televisheni ya al Alam imeripoti leo kuwa, makumi ya mamluki vamizi wa Saudia wameuawa kwenye operesheni hiyo. Jeshi la Yemen limefanya mashambulizi pia katika maeneo ya mamluki hao wa Aal Saud katika eneo la Jabal Kahbub. Huku hayo yakiripotiwa, ndege za kivita za Saudia zimefanya mashambulio katika uwanja wa ndege wa mji wa al Hudaida, magharibi mwa Yemen.
Televisheni ya al Manar ya nchini Lebanon imeripoti kuwa, zaidi ya hospitali 500 zimeharibiwa na zaidi ya madaktari na wauguzi 300 wa Yemen wameshauawa tangu Saudi Arabia ilipoivamia nchi hiyo ya Kiislamu na Kiarabu na kufanya mashambulizi ya kikatili kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Nao Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umeripoti kuwa, zaidi ya watoto elfu kumi wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi ya kuambukiza na kukosekana madawa katika kipindi cha mwaka mmoja wa uvamizi wa Saudi Arabia nchini Yemen. UNICEF imeongeza kuwa, hivi sasa watoto wa Yemen wanateseka kwa kukosa chanjo na madawa na wanahitajia msaada wa haraka wa madaktari kutokana na kuongezeka sana maradhi ya kuambukiza.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment