Saturday, April 2, 2016

Hamas: Tunawashikilia wanajeshi wanne wa Israel



Hamas: Tunawashikilia wanajeshi wanne wa Israel
Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimesema kuwa, hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kuhusiana na kuachiliwa huru wanajeshi wanne wa Israel kutoka mikononi mwa wanamapambano wa Palestina.
Kituo cha Upashaji Habari cha Palestina leo Jumamosi kimeripoti matamshi ya Abu Ubaidah, msemaji rasmi wa Brigedi za Izzuddin Qassam akisema kuwa, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu amewadanganya Waisraeli na familia za wanajeshi wanne Wazayuni wanaoshikiliwa mateka katika Ukanda wa Ghaza.
Abu Ubaidah amesisitiza kuwa, Brigedi za Izzuddin Qassam haijawahi hata mara moja kuipa Israel maelezo yoyote kuhusiana na wanajeshi hao wanne walioko mikononi mwao. Wanajeshi hao wa Israel walitekwa nyara na wanamapambano wa Palestina wakati utawala wa Kizayuni ulipovamia na kufanya mashambulizi ya siku 50 katika ukanda huo mwaka 2014.
Akitoa taarifa rasmi jana Ijumaa, msemaji huyo wa Izzuddin Qassam amesema kuwa, Hamas haijawasiliana kwa namna yoyote ile na Israel kuhusu wanajeshi hao. Hivi karibuni, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel alidai kuwa kumepigwa hatua nzuri katika juhudi za kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa utawala huo waliotekwa nyara katika Ukanda wa Ghaza. Hadi hivi sasa utawala wa Kizayuni umeshindwa kusema chochote kuhusiana na matamshi hayo ya HAMAS.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment