Friday, April 15, 2016

City wapewa Real Madrid ligi ya mabingwa


PepImage copyrightReuters
Image captionPep Guardiola atakuwa meneja wa Manchester City msimu ujao
Klabu ya Manchester City ya Uingereza imeepuka kukutana na meneja wake wa msimu ujao Pep Guardiola kwenye nusufainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Miamba hao wa Uingereza wamepwa Real Madrid ya Uhispania.
Bayern Munich wa Ujerumani, ambao kwa sasa wamo chini ya Pep Guardiola watakutana na Atlético Madrid ya Uhispania.

Safari ya kuelekea Milan

Droo ya nusufainali Ligi ya Mabingwa Uefa 2016

Manchester City (Uingereza) v Real Madrid (Uhispania)
Atletico Madrid (Uhispania) v Bayern Munich (Ujerumani)
Allsports
Mpangilio huo natoa nafasi ya kuwepo debi ya Madrid fainali iwapo Atletico na Real zitafika fainali au hata kukutanisha Pep Guardiola na klabu yake ya msimu ujao fainali iwapo City na Bayern watafuzu.
Man City watakuwa nyumbani dhidi ya Real Madrid Jumanne 26 Aprili, na ugenini Bernabeu Jumatano 4 Mei.
Atletico Madrid watakutana na Bayern Munich nyumbani Jumatano 27 Aprili na mechi ya marudiano iwe Ujerumani Jumanne tarehe 3 Mei.
Katika Europa League, klabu ya Liverpool ya Uingereza imekabidhiwa Villarreal ya Uhispania katika hatua ya nusu fainali.
Shakhtar Donetsk kutoka Ukraine nao watakutana na mabingwa watetezi Sevilla.
Liverpool walifika nusufainali kwa kulaza Borussia Dortmund Alhamisi kwenye mechi ya kusisimua wakitoka nyuma 2-0 wakati wa mapumziko na kushinda 4-3 uwanjani Anfield.
LiverpoolImage copyrightAP
Image captionMeneja wa Liverpool Jurgen Klopp alikuwa mkufunzi wa Borussia Dortmund
Walifanikisha ushindi wa jumla wa 5-4.
Sevilla, ambao wanapigania kushinda kikombe kwa mara ya tatu mtawalia, walitinga nusufainali kwa kuwashinda Athletic Bilbao kupitia mikwaju ya penalti.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment