Saturday, April 2, 2016

Maandishi dhidi ya msikiti yawekwa uwanjani Australia



Image caption Mechi kati ya Collingwood na Richmond
Shirikisho la soka nchini Australia limeshtumu mashabiki walioweka kitambara chenye maandishi dhidi ya msikiti katika mechi moja huko mjini Melbourne siku ya Ijumaa.
Maandishi hayo yalioonekana katika mechi kati ya Collingwood na Richmond pia yalishirikisha nembo ya kundi la mrengo wa kulia la United Patritic Front.
Hatahivyo kitambara hicho chenye maandishi kiliondolewa na mashabiki waliokiweka pia wakaondolewa uwanjani.
Shirikisho la soka nchini humo mara kwa mara limekabiliwa na maswala ya ubaguzi kufuatia kuzomwa kwa mchezaji mmoja wa Aborigine.
Mkuu wa shirikisho hilo Gillon McLachlan amesema kuwa maandishi hayo yalikuwa na ubaguzi,yaliwapuuza wengine na kuwakosea heshima.
Idadi ya waislamu nchini Australia ni asilimia 2.
Mnamo mwezi Novemba ,utafiti ulionyesha kwamba waislamu wa Australia wanakabiliwa mara tatu na ubaguzi unaokabili makabila mengine.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment