Habari kutoka nchini Syria zinasema kuwa, wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wanakimbia ovyo hivi sasa baada ya jeshi la Syria kukomboa mji mwingine muhimu uliokuwa umetekwa na kundi hilo katika viunga vya mkoa Homs wa katikati mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
Mji wa Qaryatain ulitekwa na genge la Daesh mwaka 2015, lakini baada ya jeshi la Syria kufanikiwa kuukomboa mji wa kihistoria wa Palmyra (Tadmor), imekuwa rahisi kwake kuukomboa mji huo mwingine muhimu kutoka mikononi mwa Daesh. Hivi sasa wataalamu wa kutegua mabomu wa Syria kwa kushirikiana na wale wa Russia wanaendelea kutegua mabomu yaliyotegwa na magaidi wa Daesh kwenye mji huo. Afisa mmoja wa jeshi la Syria amesema kuwa, magaidi wa Daesh wametega mabomu yenye uzito wa kilo 50 katika barabara kuu na njia za ndani za mji huo, kama walivyofanya katika mji wa Palmyra. Hadi hivi sasa zaidi ya mabomu 3000 yameshateguliwa katika mji wa Palmyra pekee. Huku hayo yakiripotiwa, serikali ya Syria inaendelea kufanya mazungumzo ya kusitisha mapigano na baadhi ya makundi ya waasi hasa katika mikoa wa Damascus na Dar'a. Pamoja na hayo baadhi ya makundi hayo yameendelea kuvunja makubalano hayo. Siku ya Jumamosi kuliripotiwa kesi saba za kuvunjwa makubaliano hayo na makundi ya waasi katika mikoa ya Halab, Damascus na Latakia. Makundi hayo ya waasi yameshirikiana na wanamgambo wa al Qaida kuvunja makubaliano hayo ya kusitisha vita na serikali. Kwa upande wao, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa, hatua ya serikali ya Syria ya kubadilisha mkuu wa timu yake ya mazungumzo kwa kumuweka Faisal Miqdad badala ya Bashar al Jaafari, inaonesha hamu ya serikali ya Damascus ya kutatua haraka mgogoro wa nchi hiyo kwa njia ya mazungumzo. Wachambuzi hao wanaamini kuwa Faisal Miqdad anakubalika zaidi mbele ya wapinzani na hata pande za kimataifa zinazofanya mazungumzo na serikali ya Syria. Wakati huo huo Mikhail Bognadov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa karibuni hivi atakutaka na wawakilishi wa timu ya mazungumzo ya wapinzani wa Syria. Tarehe 9 mwezi huu wa Aprili ndiyo siku iliyopangwa kufanyika duru nyingine ya mazungumzo kati ya serikali ya Syria na wapinzani. Amma katika suala la wakimbizi wa Syria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amenukuliwa akisema mjini Geneva Uswisi kuwa, hali ya wakimbizi hao ni mbaya na kwamba mgogoro huo hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi. Alisema hayo Jumamosi usiku katika mkutano wa kujadili wakimbizi wa Syria na kuongeza kuwa, jamii ya kimataifa - katika mkutano wa mwezi uliopita wa mjini London Uingereza ambao ulijadili njia za kutatua tatizo la wakimbizi wa Syria - ulichukua maamuzi muhimu kuhusu suala hilo. Vilevile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezishukuru baadhi ya nchi jirani na Syria kwa kujitolea kwa hali na mali kuwapokea wakimbizi wa Syria. Ametoa mfano akisema, nchi kama ya Lebanon ambayo ina jamii ya watu milioni karibu nne, imepokea wakimbizi zaidi ya milioni moja wa Syria. Alaakullihaal, jeshi la Syria kwa kushirikiana na waitifaki wake linazidi kupata ushindi katika medani za mapambano, na kila leo linakomboa maeneo muhimu kutoka mikononi mwa magenge ya kigaidi. Lakini kama wanavyoamini wataalamu wengi, hatimaye mgogoro wa nchi hiyo utatatuliwa tu kwa njia za kisiasa. Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, hakuna chaguo lolote la kuweza kutatua mgogoro huo isipokuwa mazungumzo ya kisiasa. Ni jambo lisilo na shaka kuwa, wananchi wenyewe wa Syria ndio wenye haki ya kujiamulia mambo yao na hakuna mtu yeyote asiye mwananchi wa Syria mwenye haki ya kuwaamulia wananchi hao nini cha kufanya.

No comments:
Post a Comment