Ama kwa hakika usemi wa “mfupa uliomshinda fisi, Mbwa hauwezi”, Kocha wa zamani wa Dar es salaam Young Africans ambae alikuja kwa mbwembwe nyingi mwisho akashindwa kuendana na kasi ya timu hiyo ametupiwa virago na Timu ya Taifa ya Togo.
Thom Santfiet aliwahi kuifundisha Yanga kabla kutimuliwa na baadae kupata kibarua nchini Togo kukinoa kikosi hicho, nako pia ametimuliwa kwa kile kilichodaiwa kuwa mwenendo wa timu hiyo kutoridhisha hasa katika kuelekea Afcon ambapo kwasasa Togo inashika nafasi ya Tatu katika kundi lake.

No comments:
Post a Comment