Monday, April 4, 2016

Kenya kupatiwa msaada wa Euro milioni 250 kwa ajili ya kuboresha miundombinu



Kenya kupatiwa msaada wa Euro milioni 250 kwa ajili ya kuboresha miundombinu
Kenya na Ufaransa zimetiliana saini hati saba ya maelewano ambapo kupitia mikataba hiyo, Kenya itapatiwa msaada wa Euro milioni 250 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 28.8 za Kenya.
Makubaliano hayo yametiwa saini baada ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kukutana na mwenyeji wake, Rais Francois Hollande.
Hii ni mara ya kwanza kwa Marais wa Ufaransa na Kenya kukutana katika kipindi cha miaka 14 iliyopita. Imeelezwa kuwa, fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuboresha miradi mbalimbali na miundombinu nchini Kenya.
Katika safari yake hiyo huko Ufaransa, Rais Uhuru Kenyatta ameafuatana na Mawaziri Amina Mohamed, Henry Rotich, Najib Balala na Eugene Wamalwa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment