Jeshi la Syria limeendelea kusonga mbele na kuyatia hasara kubwa makundi ya kigaidi nchini humo.
Jeshi la Syria Jumatano ya jana liliendelea kusonga mbele katika maeneo tofauti ya nchi hiyo na kusambaratisha ngome za kundi la kitakfiri lenye mafungamano na Israel la Daesh katika viunga vya miji ya Homs magharibi na Deir ez-Zor, mashariki mwa Syria. Aidha katika operesheni hizo, makumi ya magaidi waliangamizwa na wengine kutiwa mbaroni. jeshi la Syria limeteketeza magari 20 ya kundi hilo la Daesh kaskazini mashariki mwa mji wa Palmyra. Kadhalika jeshi limeshambulia mjumuiko wa wanachama wa Daesh katika kijiji cha 'al-Marbaiyyah' katika viunga vya mashariki mwa mji wa Deir ez-Zor, ambapo katika shambulio hilo makumi ya magaidi wa genge hilo wameuawa. Mbali na hayo jeshi la Syria limeilenga ngome ya magaidi wa Daesh katika vijiji vya Abu Hubailat na eneo la Wadi al-Uzaib katika viunga vya mashariki mwa mji wa Hama. Katika upande mwingine wataalamu wa Russia wametegua mabomu 120 yaliyokuwa yametegwa na magaidi wa Daesh baada ya kufurushwa kutoka mji wa Palmyra. Baada ya jeshi la Syria kupata mafanikio makubwa nchini humo, magaidi wengi wa Daesh na Jab'hatu Nusra na wengine wamelazimika kukimbilia nchini Libya kwa ajili ya kuokoa maisha yao.
No comments:
Post a Comment