Monday, April 4, 2016

HARUNA MOSHI BOBAN KAJIPOTEZA MWENYEWE?



BOBANI

Tanzania ina mafundi wengi wa mpira wa miguu , zamani walikosa nafasi ya kucheza mbele (Ulaya) kutokana na ugumu wa wakati huo lakini walikuwa na vipaji vya hali ya juu sana,leo tuna muangazia  mtukutu wa soka la bongo na penda kumuita Baloteli wa bongo si mwingine ni Haruna Moshi Shabani.

Haruna ni miongoni mwa wachezaji walio na vipaji vya hali ya juu sana hapa Tanzania na miongoni mwa familia za soka kuwahi kutokeaTanzania zipo nyingi mfano familia ya Kihwelo, hivi una mkumbuka Iddi Moshi huyu alicheza Yanga kwa mafanikio makubwa japo hakuwa mtata kama mdogo wake Haruna Moshi.. ufundi wa Haruna Moshi umempatia jina la mchezaji nyota na kiungo wa Zamani wa Ac Milan Zvonimir Boban haswa kwa mipira yake ya pasi za uhakika na akili nyingi pasipo kutumia nguvu ambayo ina fanana na Haruna Moshi Shabani.

Haruna ni hodari sana wa pasi za mwisho na fundi wa pasi za mbali pamoja na yote Haruna Moshi yupo mbeya City mfuatilie kwanza uone anacho kifanya anacheza vizuri na moja ya hazina ambayo endapo ingetulia angeanza kutoka yeye kimataifa kabla ya Mbwana Samata. kumbuka kuwa aliwahi kupata dili huko Denimark kucheza soka la kulipwa kabla ya kuchemka kwa mapungufu yake binafsi.

NANI KAMPOTEZA HARUNA MOSHI “BOBAN”?

Ni swali inabidi tujiulize wapenzi wa mpira ninani aliye mpoteza Haruna, nadhani majibu yake kila mtu anayo na anajibu anavyo jua, Boban“AMEJIPOTEZA MWENYEWE” mpira unahitaji nidhamu kujituma na hekima nahuo ni utaratibu wa maisha popote hata hapa Mtembezi.sports kama nitakuwa sina heshima na kufuata utaratibu wa kazi hata ikiwa nina andika makala nzuri au story nzuri siwezi kuendelea kutokana na utaratibu, Boban ana kipaji cha hali ya juu alikosa utulivu na heshima ndani ya Simba, angekuwa na Subra naamini kwa sasa tungekuwa na watu wawili kimataifa au wa tatu kuiwakilisha nchi.

KIPI KILIMSHINDA DENIMARK

Vitu viwili vili mponza Boban kucheza nje wakati umri ukiwa mdogo na alipopata dili kucheza nje,

1. Inaarifiwa kuwa kule alikosa mambo yetu yale ya kupuliza moshi kama lilivyo jina lake unajua kule wenzetu wanafanya check up kila juma hii imeshinda kwa kuwa huku tumezoea hata madaktari tunaweza kuwapa pesa wakatoa majibu ya uongo. na alianza kumlaumu wakala kuwa hajamlipa baadae eti matatizo ya kifamilia daah niliumia haswa kuona kipaji cha Haruna kinapotea.

2.Subira alikosa uvumilivu kama angekuwa na uvumilivu angepata nafasi nzuri sana ya kucheza haswa ana kiwango kizuri na nafasi yake ndio soko kubwa ulaya kiungo hadi washambuliaji huwa wana pata soko kubwa..

Haruna Moshi sasa yupo Mbeya City lakini kabla ya hapo aliwahi kuchezea Coast Union akiwa na swahiba wake Juma Nyoso kabla ya kuhama nae Mbeya city, na Timu iliyo mfanikisha na kumpa jina kubwa Tanzania ni Mnyama SIMBA . umemkumbuka Nyosso? hahaha! kaa tayari na Mtembezi itakupa mengi ya kimichezo kitaifa na kimataifa.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment