Garissa: Wakenya waadhimisha kumbukumbu za shambulio
Image captionMnara wa kumbukumbu za shambulio la Garissa
Maelfu ya Wakenya kutoka maeneo tofauti nchini siku ya Jumamosi walikongamana katika chuo kikuu cha Garissa ili kuadhimisha mwaka mmoja tangu shambulio baya la kigaidi lililowauawa watu 148 wengi wao wakiwa wanafunzi.
Usalama uliimarishwa ndani na hata nje ya chuo hicho huku wale waliokuwa wakiingia wakifanyiwa ukaguzi mkali na maafisa wa polisi.
Image captionMbio za marathon zilizoandaliwa mjini Garissa kwa lengo la kuleta uwiano
Vilevile mamia ya watu walishiriki katika mbio za marathon za kumbukumbu ya shambulio hilo.
Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo pamoja na kiongozi wa walio wengi bungeni Adan Duale walishiriki katika mbio hizo za kilomita 5.
Waandalizi wanasema kuwa mbio hizo zililenga kuleta uwiano kati ya Wakenya kufuatia shambulio hilo.
Image captionMbio za marathon
Mwandishi wa BBC katika chuo hicho anasema maadhimisho hayo yatahusisha uzinduzi wa mnara wa ukumbusho.
Share Post
UnknownWeb Developer
Follow me on:
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
No comments:
Post a Comment