Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesisitiza juu ya udharura wa kuimarishwa uwezo wa makombora wa taifa hili.
Ayatullah Sadiq Amoli Larijani amesema hayo leo katika kikao chake na maafisa wa vyombo vya mahakama ambapo mbali na kusisitiza udharura wa kuimarishwa uwezo wa kimakombora wa Iran amebainisha kwamba, kudhoofisha, kuharibu na kuzitilia alama ya swali juhudi, mafanikio ya kijeshi, kiusalama na kimakombora ya Iran kwa kizingizio cha uhuru wa kutoa maoni ni hiyana na usaliti kwa malengo matukufu ya Jamhuri ya Kiislamu.
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran ameongeza kuwa, hatua ya Iran ya kuwa mfano na kiigizo kwa nchi za Kiislamu ni hatari kubwa kwa madola ya kibeberu ya Magharibi na sasa madola hayo yamekuwa yakifanya njama na kutumia kila wenzo kudhoofisha, kuharibu na kutilia alama ya swali mfumo huu.
Ayatullah Larijani ameashiria njama za Marekani dhidi ya Iran na kusema kuwa, Washington imekuwa ikikwamisha mambo kwa kuyashinikiza mashirika ambayo yana hamu ya kushirikiana na Iran.
Amesema, Marekani inapaswa kutambua kwamba, Iran haiko tayari kulegeza kamba kuhusiana na maslahi yake na taifa hilo halitaruhusu mashirika ya kigeni kufanya uwekezaji hapa hapa nchini kwa thamani yoyote ile.
No comments:
Post a Comment