Monday, April 4, 2016

Senegal kupokea wafungwa wa Guantanamo



Image copyrightGetty
Image captionSenegal kuwapokea wafungwa wa Guantanamo
Senegal imekubali kuwapokea wafungwa wawili wa Guantanamo Bay kwa misingi ya kibinadamu .
Serikali ya taifa hilo la Magharibi mwa Afrika inasema kuwa kutokana na mafunzo ya dini ya kiislamu wamekubalika kuwapokea walibya hao 2 kwa mujibu wa waziri wa maswala ya kigeni wa nchi hiyo.
Wafungwa hao 2 walikuwa wanatumikia kifungo cha miaka 14 jela bila kufunguliwa mashtaka yeyote.
Kauli hiyo inafuatia uamuzi wa serikali ya rais Barack Obama ya kufunga jela hiyo ya kisiwa cha Guantanamo Bay.
Image copyrightAFP
Image captionWafungwa hao 2 walikuwa wanatumikia kifungo cha miaka 14 jela bila kufunguliwa mashtaka yeyote.
Rais huyo wa Marekani aliahidi kufunga kituo hicho miaka 7 iliyopita.
Mataifa machache yamekubali kuwapokea wafungwa wa Guantanamo Bay yakiwemo baadhi ya mataifa ya kiafrika kama Uganda, Ghana na Cape Verde.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment