Sunday, June 26, 2016

SIMBA YAJIBU MAPIGO YA YANGA



Haji Manara-Afisa habari Simba SC
Haji Manara-Afisa habari Simba SC
Awali ya yote klabu inaendelea kutoa pongezi kwa ndugu zetu Waislaam wanaoendelea kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani tunaamini Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kwa ibada hiyo muhimu.
Ndugu wanahabari katika siku za karibuni hususan kuelekea mchezo wa Yanga na klabu kutoka Congo DRC  TP Mazembe Englebert kumekuwa na maneno mengi kutoka klabu ya Yanga yakiishutumu klabu yetu kuhusiana na kutokutoa ruhusa kwa mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ na pia kuhusiana na namna mashabiki watakavyokaa majukwaani siku ya mchezo huo Jumanne ya wiki hii.
Klabu ya Simba kwa maksudi kabisa inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na mambo hayo mawili yanayoleta sintofahamu miongoni mwa wadau wa mchezo huu murua wa kandanda.
Hakuna barua yoyote ambayo klabu ya Yanga imetuandikia kuhusiana na suala la mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ pia hakuna hata mazungumzo yaliyofanyika baina ya viongozi wa vilabu hivi ili kutuomba walau kwa mdomo kama taratibu zinavyotaka.
Ikumbukwe Simba huwa haina tatizo kuruhusu matakwa binafsi ya mchezaji na nyote mnajua utamaduni huo wa klabu yetu.
Kwa wasiofahamu mwaka 1998 klabu ya Simba iliwaazima wachezaji watatu Yanga ili wacheze hatua ya makundi kama hii ya klabu bingwa Afrika wachezaji hao ni Shaban Ramadhani Monja Liseki na Alphonse Modest sasa jiulize kama tuliweza kuwaazima wachezaji vipi tushindwe kumruhusu mchezaji waliyemsaini? Pamoja na maneno yao ya kuudhi Simba ni waungwana wa kutosha na wao wasitumie ukimya wetu kuwapotosha wanachama na washabiki wao eti tumewakatalia kuwajibu barua ya Hassan Ramadhani ‘Kessy’
Msimamo wetu kuhusiana na jambo hili inategemea uungwana wao tu.
Pia Yanga kupitia msemaji wao wamenukuliwa kuwa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe watakaa kwenye majukwaa yote hata yale ambayo kwa utamaduni wa uwanja wa taifa hukaliwa na mashabiki wa klabu yetu.
Tunafahamu kuwa kauli hii ina nia ya kuchochea vurugu kubwa kwenye mchezo huo na sote tunajua athari ya vurugu michezoni tunawashauri Yanga wasijaribu kuleta mashabiki wao kwenye majukwaa wanayokaa washabiki wa Simba ili kuleta amani siku hyo ya mchezo.matarajio yetu vyombo vinavyohusika vitasimamia kwa ukaribu jambo hilo.
Mwisho ingawa si kwa umuhimu klabu haimzuii yoyote kushangilia timu yoyote siku ya mchezo huo kama zilivyo desturi ya wao Yanga kushangilia klabu yoyote inayocheza na Simba hususan wageni toka nje.kama ilivyokuwa miaka michache nyuma ambapo walishangilia na kuvaa jezi za TP Mazembe.
Waarabu wana msemo wao maarufu “KAMA TUDINI TUDANI” kama ulivyofanya na wewe utafanyiwa hivyohivyo.

Waethiopia 19 wapoteza maisha ndani ya lori la wasafirishaji haramu wa watu:IOM

Wakimbizi wa kutoka Ethiopia na Eritrea amabo wanaokolewa na wafanya kazi wa IOM.(Picha:© IOM 2015)
Takribani Waethiopia 19 wamekutwa wamekufa ndani ya lori nchini Zambia baada ya kukosa hewa . Lori hilo linasadikiwa kuwa ni la mtandao wa usafirishaji haramu wa binadamu na lilikuwa likielekea Afrika ya Kusini.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM , wahanga hao walikutwa baada ya manusura kugongagonga kontena walimokuwa wakihitaji msaada. Msemaji wa IOM Joel Millman amesema tukio hilo ni baya sana kulishuhudia.
(SAUTI YA JOEL MILLMAN)
"Hili ni kubwakabisa tunalolifahamu, lakini kumekuwa na visa vingine vya kutisha kwatika safari hizo siku za nyuma.Nadhani ilikuwa mwaka jana au miwili iliyopita kulikuwa na tukio la wahamiaji kuzama, ambao walishuhudiwa wakiliwa na mamba, lakini hatujawahi kuona vifo vya kukosa hewa kwenye kontena kama hivi"
Kwa mujibu wa IOM manusura 76 waliojumuisha watoto, wamepelekwa kwenye makazi ya dharura.

Ban ahuzunishwa na mapigano Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Sudan SPLA na vikundi vyenye silaha mjini Wau,  na maeneo jirani  nchini Sudan Kusini.
Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu akisema kuwa amesikitishwa na taarifa za vifo kufuatia machafuko hayo.
Amevitaka vikosi kinzani kusitisha uhasama hima, kuruhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kufika katika maeneo hayo na kushirikiana na wadau wa misaada ya kibinadamu ili kuwezesha ufikishwaji wa misaada.
Ban amezitaka pande hizo kukubali majadiliano ili kutatua mizozo yao ya kisiasa huku pia akipongeza UNMISS na timu ya misaada ya kibinadamu nchini humo kwa hatua za kulinda raia wanoakimbia mjini Wau.
UNMISS iko katika mchakato wa kutuma vikosi zaidi ili kukabiliana na dharura

Umuhimu wa mabaharia utambuliwe : IOM

Baharini kwa wote ni kauli mbiu inayotumika kwa ajili ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya mabaharia leo Juni 25, 2016.
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, linaadhimisha siku hii kwa mara ya sita kwa kuangazia umuhimu wa mabaharia katika bahari duniani ambapo Katibu Mkuu wa IOM Kitack Lim amekaririwa akisema mabaharia hawatambuliwi huku wakitimiza jukumu muhimu la kuisongesha dunia.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wa kuadhimisha siku hii amesema mabaharia wanalisha dunia, huvalisha na kuihifadhi.

Ban amesema wana umuhimu katika kukuza uchumi jumuishi na aunaojali mazingira.
Sherehe za siku ya mabaharia zitafanyika rasmi Septemba 29 ambayo ni siku ya kimataifa ya masuala ya bahari,ambapo umuhimu wa dhana hiyo utamulikwa.

Habari za wiki Hapa na pale Vipindi Taarifa maalumu Kuhusu Idhaa Hati ya mtumiaji 25/06/2016 Jumuiya ya Ulaya chondechonde wathaminini wakimbizi,wahamiaji: Ban

Ban Ki-moon akiwatia moyo wakimbizi nchini Ugiriki. Picha na Rick Bajornas wa UMAkiwa ziarani nchini Ufaransa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisisitiza kuwa uamuzi wa Uingereza kujitoa katika jumuiya ya Ulaya EU, haupasiwi kuwa mzigo kwa wakimbizi, wahamiaji na wasaka hifadhi barani humo.
Akizungumza na vyombo vya habari akiwa ameambatana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande, Ban amesema anatarajia nchi za Ulaya zitaheshimu sheria za  kimataifa na kuonyesha ubinadamu kwa makundi hayo yasiyo na hatia.
Akitolea mfano Katibu Mkuu amesema juma lililopita alitembelea kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki ambapo alikutana na kushuhudia madhila ya wakimbizi kutoka Syria, na Iraq.
Amesema wakimbizi hao ambao waliosafiri safari zisizo salama za muda mrefu ni wachovu na wanachotaka ni uslama na watoto wao, elimu na ajira ili waweze kushiriki katika maendeleo

Mke wa Rais Obama ziarani barani Afrika

 media
Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi barani Afrika, Jumapili hii, akiambatana na watoto wake, Sasha na Malia, ziara ambayo ni sehemu ya juhudi zake za kuhamasisha elimu kwa mtoto wa kike.
Ziara hii ya siku sita barani Afrika, itashuhudia mke wa rais Obama, akisafiri kwenye nchi za Morocco na Liberia, ambapo pia atasafiri hadi Hispania.
Ziara ya Michelle Obama imebeba ujumbe wa "Waache wasichana wasome", ilizinduliwa na Serikali ya Marekani kupitia rais Barack Obama na mkewe mwenyewe mwaka 2015.
Mradi huu ni sehemu ya Serikali ya Marekani katika juhudi zake za kueneza elimu na kuondoa vikwazo ambavyo vinawazuia zaidi ya wasichana milioni 62 duniani kutokwenda shule.
Kwenye ziara hiyo, Michelle atasindikizwa na muigizaji, Meryl Streep na Freida Pinto nchini Morocco, ambako watazungumza na wasichana wadogo kuhusu changamoto zinazowakabili kupata elimu, ilisema taarifa ya ofisi ya mke wa rais.
Akiwa nchini Liberia, atatembelea kituo cha Marekani cha wafanyakazi wa Marekani wanaojitolea, pamoja na shule moja ya wasichana akiambatana na rais wa Liberia, Ellen Johansson Sirleaf, mwanamke wa kwanza Rais aliyechaguliwa kidemokrasia na mshindi wa tuzo la Nobel.
Nia ya Michelle Obama kuwasaidia wasichana kupata elimu, ilizidi baadaya tukio la kutekwa nyara kwa wasichana zaidi ya 200 wa Chibok kaskazini mwa Nigeria, mwezi Aprili mwaka 2014, ambapo aliandika kwenye mtandao wake #BringBackOurGirls.

Watu 11 wauawa katika shambulizi la Al Shabab mjini Mogadishu


media Shambulizi katika Hoteli ya Naasa Hablood mjini Mogadishu Somalia 25 06 2016 REUTERS/Feisal Omar
Takriban watu 11 wameuawa jana Jumamosi katika shambulizi kwenye hoteli ya mjini Mogadishu nchini Somalia ambalo linadaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab.
Shambulizi hilo ambalo ni la karibuni katika mfululizo wa mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la Al Shabab kulenga hoteli na migahawa, lilianza wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alipolipua bomu lililokuwa limetegwa garini nje ya jengo la hoteli.
Watu wenye silaha walivamia hoteli iitwayo Naasa Hablood na milio ya risasi ilisikika kwa saa kadhaa, mashahidi wamesema, kabla ya mamlaka kutangaza mashambulizi kumalizika.
Vikosi maalum vya usalama vimekomesha shambulizi hilo baada ya kuwaua washambuliaji watatu ndani ya hoteli.
Msemaji wa wizara ya usalama Abdi Kamil Shukri, amewaambia waandishi wa habari kuwa raia kumi na mmoja, wawili kati yao madaktari, wameuawa katika shambulio hilo.