Sunday, July 10, 2016

Obama kurejea nyumbani mapema; mauaji yaitikisa Marekani



Rais Obama atafupisha ziara yake katika mataifa ya kigeni na kwenda Dallas wiki ijayo wakati mashambulizi ya risasi yaliyofanywa na kijana mweusi ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliyetia nia ya kuwauwa polisi wazungu.
NATO Gipfel in Warschau Obama PK zu Dallas Rais Barack Obama wa Marekani
Mauaji hayo yamesababisha miito ya haraka kuleta hali ya kuvumiliana nchini humo kutokana na matatizo ya kibaguzi.
Polisi waligundua vifaa vya kutengenezea mabomu na silaha katika nyumba ya kijana huyo Micah Johnson mwenye umri wa miaka 25, mkaazi wa eneo la Dallas ambaye aliwapiga risasi polisi watano kabla ya kufariki katika mapambano ya silaha na polisi.
USA Ermordung von Polizisten in Dallas Täter Micah Xavier Johnson Micah Xavier Johnson aliyewauwa polisi watano mjini Dallas
Ikulu ya Marekani ya White House imeondoa uwezekano wa mahusiano kati ya mshambuliaji huyo mwenye silaha na makundi yanayotambulika ya kigaidi, mahusiano katika ukurasa wake wa Facebook yanaelekeza katika makundi ya wanaharakati wenye msimamo mkali ya Wamarekani weusi ambayo yameorodheshwa kuwa ni makundi ya chuki nchini Marekani.
Akielezewa na polisi kuwa ni mshambuliaji aliyeamua kutenda kitendo hicho peke yake na hakuwa na rekodi ya uhalifu hapo nyuma , Johnson aliwaambia watu waliokuwa wanafanya nae majadiliano kabla ya kufariki kwamba alitaka kuwauwa polisi wazungu kwa kulipiza kisasi kutokana na kuuwawa kinyama hivi karibuni kwa watu wawili weusi.
USA Trauer nach Ermordung von Polizisten in Dallas maua yakiwekwa katika eneo polisi walipouwawa mjini Dallas
Maandamano ya amani
Mashambulizi hayo jimboni Texas, ambayo yalizuka siku ya Alhamis usiku wakati wa maandamano ya amani dhidi ya ukatili wa polisi, yanakuja katika wakati wa hali ya kutafakari kuhusiana na matumizi ya silaha kwa ulinzi wa amani kuelekea Wamarekani weusi.
Viongozi wa harakati za Maisha ya Weusi ni muhimu wameshutumu mauaji hayo mjini Dallas, huku wakiapa kuendelea na maandamano yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa juma, huku makundi makubwa ya watu wakijikusanya usiku wa Ijumaa mjini Atlanta Georgia na wengine wengi wakiwa nje ya Ikulu ya Marekani White House.
Akihutubia maelfu ya watu katika sala iliyofanyika kwa heshima ya maafisa wa polisi waliouwawa, meya wa Dallas Mike Raswlings amewataka Wamarekani , kuimarisha hatua , kuponesha vidonda vya ubaguzi nchini humo.
USA Ermittlung nach Ermordung von Polizisten in Dallas Magari ya polisi yakizuwia barabara kulinda usalama mjini Dallas
Maandamano yataendelea
"Hatutajitenga na ukweli uliopo kwamba sisi kama wakaazi wa mji, wa jimbo, na kama taifa tunapambana na masuala ya kibaguzi," ameliambia kundi la watu waliokusanyika.
Rawlings amerudia ujumbe uliotolewa na rais Obama wakati taifa hilo linahangaika kutokana na ghasia hizo za hivi karibuni: Kwamba maisha ya weusi ni muhimu , na kama ilivyo kwa maisha ya wazungu, wale maafisa wa polisi.
USA Trauer nach Ermordung von Polizisten in Dallas Waombolezaji wakiweka maua katika eneo la mauaji
"Tunapaswa kuongeza nguvu na kuyakabili masuala tata kwa njia nyingine," amesema Rawlings. "Na masuala ya kibaguzi yanautata."
Obama , ambaye ameamuru bendera zote zipepee nusu mlingoti katika majengo ya serikali kwa muda wa siku tano, aliweka wazi kwamba ghasia dhidi ya polisi, haziwezi kuhalalishwa kabisa."
Rais alizungumzia mashambulizi hayo akiwa katika mji mkuu wa Poland, Warsaw , ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa kilele wa NATO, na kuiita hali hiyo , "inayojirudia na ya kukera."
USA Dallas Schießerei bei Demonstrationen gegen Polizeigewalt Polisi wakimtafuta muuaji

Takriban 150 wauwawa katika mapigano Sudan Kusini


Takriban wanajeshi 150 kutoka makundi yanayohasimiana nchini Sudan Kusini wameuwawa katika mapigano katika mji mkuu wa Juba na kuzusha wasi wasi wa kuheshimiwa kwa mchakato dhaifu wa amani.
Milio ya risasi,maguruneti na mizinga ilisikika hapo Ijumaa jioni karibu na Ikulu ambapo Rais Salva Kiiri alikuwa akikutana kwa mazungumzo na makamo wake wa rais Riek Machar. Viongozi hao wote wawili ambao huo nyuma walikuwa mahasimu wamesema hawajuwi kile kilichochea mapigano hayo kati ya makundi yao na wametowa wito wa kuwepo utulivu.
Chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mafunzo mjini Juba ambayo ni hospitali kuu ya serikali imepokea zaidi ya maiti tisini za askari na raia ambapo kwa mujibu wa daktari mmoja katika hospitali hiyo ambaye amekataa kutajwa jina lake amesema nyingi ya maiti zilikuwa za wanaume.
Jeremiah Young mfanyakazi wa misaada wa shirika la hisani la World Vision aliyeko Juba amesema "kuna watu wanaotembea mitaani lakini wana wasi wasi mkubwa na kwamba kuna uwezekano wa hali kuzidi kuwa mbaya."
Hali ni shwari Juba
Riek Machar (kushoto)baada ya kula kiapo cha kuwa makamo wa rais kufuatia kurudi kwake Juba hapo mwezi wa Aprili (kulia) ni Rais Salva Kiir. Riek Machar (kushoto)baada ya kula kiapo cha kuwa makamo wa rais kufuatia kurudi kwake Juba hapo mwezi wa Aprili (kulia) ni Rais Salva Kiir.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Lul Ruai Koang amesema hali katika mji mkuu huo inarudi kuwa ya kawaida.Wakati James Gatdet msemaji wa Machar amevilaumu vikosi vya usalama vya Kiir kwa kuzuka kwa mapigamo hayo ambapo amesema viliwashambulia walinzi wa Machar.
Kwa upande wake Gatijach Deng msemaji wa kitengo cha kijeshi katika kundi la Machar amesema mapigano hayo yalitokea karibu na Ikulu na katika kambi za kijeshi.Deng amesema hapo asubuhi walikusanya maiti 35 kutoka upande wa kundi la (SPL-IO) la Machar na themanini kutoka vikosi vya serikali.Amesema yumkini idadi ya vifo ikaöngezeka kwa upande wa kundi la Machar kutokana na kwamba majeruhi wengi wako mahtuti.
Takriban wanajeshi watano waliuwawa hapo Alhamisi katika mapambano kama hayo kati ya pande hizo mbili.
Taifa hilo changa kabisa barani Afrika linaibuka kutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe vilioanza hapo mwezi wa Disemba mwaka 2013 baada ya Kiir kumtimuwa Machar katika wadhifa wa makamo rais.
Vita hivyo vilipiganwa kwa kiasi kikubwa chini ya misingi ya kikabila ambapo Kiir alikuwa akiungwa mkono na kabila lake na Dinka na Machar akiungwa mkono na kabila lake la Nuer.
Makubaliano ya amani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Rais Salva Kiir mjini Juba. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Rais Salva Kiir mjini Juba.
Makubaliano ya amani yaliofikiwa mwezi wa Augusti yalikomesha vita hivyo lakini Kiir na Machar bado hakuviunganisha vikosi vyao kipengele muhimu katika makubaliano hayo.
Mapigano hayo ya Alhamisi na Ijumaa ni kuibuka kwa matumizi makubwa ya nguvu kuwahi kushuhudiwa mjini Juba tokea Machar arudi katika mji mkuu huo hapo mwezi wa Aprili baada ya kumchaguwa tena kama makamo wa rais wake.
Shuhuda wa shirika la habari la Uingereza amesema hapo Jumamosi kwamba Juba iko shwari lakini kuna wasi wasi mkubwa ambapo katika baadhi ya barabara kumewekwa vizuizi vya barabara. Magari makubwa ya kijeshi yameonekana yakipiga doria na takriban shughuli zote za kibiashara zimefungwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewahimiza viongozi wa nchi hiyo kutekeleza makubaliano hayo ya amani na kwamba kinachojidhihirisha hakuna kujitolea kwa dhati katika makubaliano hayo.
Sudan Kusini ambapo vita vyake vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisa kushuka kwa uzalishaji wake wa mafuta vimefuta sherehe za kuadhimisha siku ya uhuru wa nchi hiyo kutokana na ukosefu wa fedha.

Syria yarefusha muda wa kusitisha mapigano

Jeshi la Syria limesema Jumamosi(09.07.2016) limerefusha usitishaji mapigano nchi nzima licha ya kutokea mapambano makali kuwania kudhibiti barabara pekee kuingialia maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa Aleppo
Syrien Krieg - Blick auf Aleppo Mji wa Aleppo unaokabiliwa na mashambulizi ya waasi na serikali
Mashambulizi hayo ya makombora yamewauwa zaidi ya raia 50 katika mji huo wa kaskazini.
Shirika la habari la Syria SANA limesema uongozi wa jeshi umerefusha , "muda wa siku tatu wa utulivu" ambao ulimalizika usiku wa manane siku ya Ijumaa. Usitishaji huo sasa utaendelea kwa masaa mengine 72 hadi usiku wa manane siku ya Jumanne.
Syrien Luftangriff auf Rebellengebiet von Aleppo Mji wa Aleppo ukiwa magofu baada ya mashambulizi
Tamko la kusitisha mapigano lililotangazwa siku ya Jumatano limeingiliana na kuanza kwa sikukuu ya Idd ul-Fitr, ambayo inaadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kiasi ya raia 155, ikiwa ni pamoja na watoto 48, waliuwawa katika mapigano yaliyotokea katika sehemu mbali mbali za Syria wakati wa sikukuu hiyo iliyodumu kwa siku tatu, limeripoti shirika la linaloangalia haki za binadamu nchini Syria.
Tangazo la kurefusha usitishaji mapigano
Kurefushwa kwa usitishaji mapigano kulitangazwa wakati majeshi ya serikali na waasi yakiendelea kupigana kuwania udhibiti wa njia pekee kuingia katika eneo la mashariki ya mji wa Aleppo linalodhibitiwa na waasi, huku kukiwa na mashambulizi ya makombora kutoka kila upande katika sekta zote za mji huo uliogawika.
Syrische Armee Soldaten Aleppo Wanajeshi wa serikali wakifanya doria
Shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria limeripoti mashambulizi mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga katika magari yaliyofanywa na tawi la al-Qaeda , la al-Nusra Front, katika jaribio la kuyarejesha nyuma majeshi ya serikali ambayo siku ya Alhamis yamedhibiti na kuzuwia barabara muhimu ya Castello, njia pekee ya kujipatia mahitaji kwa eneo linaloshambuliwa sana la mashariki.
Shirika la habari la Syria SANA, likinukuu duru za kijeshi ambazo hazikutajwa , limesema kwa majeshi ya serikali siku ya Jumamosi yalipanua udhibiti wao kuzunguka barabara muhimu ya Castillo.
Hasara kubwa kwa waasi
Hatua hiyo inayodaiwa ya kusongambele imekuja baada ya majeshi ya serikali kutoa kipigo kikali na kusababisha "hasara kubwa" katika kile shirika hilo ilichosema kuwa ni "magaidi" likimaanisha waasi wanaopigana kuuondoa utawala wa rais Bashar al-Assad.
Syrien Aleppo Zerstörung nach Luftangriff Mashambulizi ya anga yameharibu sehemu kubwa ya mji wa Aleppo
Kiasi ya raia 38 waliuwawa usiku wa Ijumaa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na waasi katika eneo la Aleppo magharibi linalodhibitiwa na serikali, kwa mujibu wa shirika hilo linaloangalia haki za binadamu, ambalo linakusanya ripoti zake kutokana na mtandao wake wa wanaharakati ndani ya Syria.
Wakati huo huo , kiasi ya raia 17 wameuwawa , ikiwa ni pamoja na watoto sita , waliouwawa katika mashambulizi ya makombora na ya anga yaliyofanywa na jeshi la serikali katika sekta ya mashariki ya mji wa Aleppo.
Syrien - Russische Soldaten unterstützen Assad Marubani wawili wa Urusi waliuwawa na wapiganaji wa Dola la Kiislamu baada ya kuidungua helikopta yao
Na marubani wawili raia wa Urusi wamefariki karibu na mji wa Syria wa Palmyra wakati helikopta yao ilipodunguliwa na wapiganaji wa Dola la Kiislamu, na kufikisha idadi ya wanajeshi wa Urusi waliouwawa nchini Syria kufikia 12, imesema serikali ya Urusi.
Wizara ya ulinzi imesema helikopta ya Syria ikirushwa na marubani Riafagat Khabibulin na Yevgeni Dolgin " ilishambuliwa " na wapiganaji wa IS jana Jumamosi na kuanguka na kuwauwa marubani wote wawili.

Msichana mweusi kuwa Iron Man


 Image caption Msichana mweusi kuwa Iron Man
Kampuni ya vitabu vya vibonzo vya ucheshi ya Marvel imefichua kwamba msichana mweusi wa umri wa miaka 15 ndiye atakayeigiza Iron Man katika filamu ijayo ya mfululizo wa filamu hizo.
Katika filamu hiyo itakayoitwa Civil War II, mavazi ya Iron Man yatavaliwa na mhusika atakayeitwa Riri Williams.
Atachukua majukumu hayo kutoka kwa Tony Stark.
Mhusika Riri Williams ni mzaliwa wa Chicago ambaye ni gwiji wa sayansi na anasomea chuo cha MIT.
Image caption Atachukua majukumu hayo kutoka kwa Tony Stark.
Mtunzi wa hadithi za Iron Man Brian Michael Bendis ameambia gazeti la Time kwamba alibuni mhusika Williams baada ya kuguswa na “visa vya ghasia, fujo na ukatili” ambavyo vilikuwa vinatokea Chicago alipokuwa anafanya kazi huko.
“Na simulizi hii ya mwanamke kijana, mwerevu ambaye maisha yake yamekumbwa na mikasa na hatari ambayo ingeangamiza maisha yake, ghasia mitaani, na alifanikiwa kwenda chuo ilinigusa sana,” amesema.
Image caption Mhusika wa Iron Man alianza kutumiwa mara ya kwanza 1963.
"Nilifikiri hiyo ni aina ya kisasa zaidi ya hadithi ya shujaa ambayo nimewahi kuisikia.”
Mhusika wa Iron Man alianza kutumiwa mara ya kwanza 1963.
Habari kwamba mhusika wa sasa atakuwa mwanamke na mweusi imesifiwa na wengi wanaoitazama kama hatua ya kukumbatia jinsia na watu wa asili mbalimbali.

Simu milioni 10 za Android zaathiriwa na kirusi


Kirusi kinachoathiri simu za Android
Hadi simu milioni 10 aina ya Android zimeambukizwa virusi vinavyotoa Clicks bandia kwa ajili ya matangazo kulingana na watafiti.
Programu hiyo pia inaweka apps na kumchunguza mwenye akaunti.
Kirusi hicho kinawapatia takriban dola 300,000 kila mwezi waliokianzisha.
Simu nyingi ambazo zimeathiriwa na kirusi hicho zipo nchini China
Ongezeko la simu zilizoathiriwa na kirusi hicho lilibainika na kampuni ya usalama wa mitandao Checkpoint na Lookout.
Kirusi hicho kinatoka familia ya Shedun by Lookout but Hummingbad by Checkpoint.
Image caption Smartphone
Katika blogu,Checkpoint imesema kuwa imefanikiwa kubaini kithibiti cha simu zilizoathiriwa ambacho kinaonyesha kuwa Hummingbad imeathiri simu milioni 10.
China ,India,Ufilipino na Indonesia zinaongoza katika mataifa yenye simu zilizoathirika.

Boko Haram yashambulia kambi ya jeshi Nigeria


 
Image caption Jaribio la Boko Haram kushambulia kambi ya kijeshi Nigeria lilitibuka 16 kati yao waliuawa
Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa limewaua wanachama 16 wa kundi la Boko Haram katika mapigano yaliyodumu saa kadhaa.
Msemaji wa jeshi alisema kuwa mapigano hayo yalianza wakati washambuliaji wa kujitolea mhanga waliokuwa wakitumia pikipiki walijaribu kuingia katika kambi ya jeshi eneo la Rann karibu na mpaka na Cameroon.
Image copyright BOKO HARAM VIDEO
Image caption Wapiganaji wa Boko haram walishambulia kambi ya kijeshi wakiwa na pikipiki na mabomu
Wanajeshi wawili waliuawa huku wenyeji wakisema kuwa raia 7 nao walipoteza maisha yao.
Harakati za Boko Haram ambazo zimedumu kipindi cha miaka 7 zimesababisha vifo vya takriban watu 20,000 kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuwalazimu karibu watu milioni 2 kuhama makwao.

Mapigano yazuka upya Sudan Kusini


 
Image caption Hali bado ni tete Sudan Kusini
Msemaji wa jeshi tiifu kwa makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar ameiambia BBC kuwa majeshi yao yanakabiliana na jeshi la serikali tiifu kwa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.
Kanali William Gatjiath amesema kuwa wanajeshi watiifu kwa bw Machar wamevamia mji mkuu wa Juba kutoka pande zote .
Kanali Gatjiath anasema wanajeshi hao wanalipiza kisasi kufuatia mashambulizi makali kutoka kwa jeshi la rais Kiir.
Serikali haijasema lolote tangu machafuko hayo yaanze muda mchache uliopita.
Awali Wanajeshi wanamuunga mkono makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar walisema kuwa kambi yao ilishambuliwa usiku wa kuamkia leo kwa risasi na bunduki nzito nzito.
Image copyright Reuters
Image caption Rais Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar wamewasihi wafuasi wao kulinda amani
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini unasema kuwa kulitokea ufyatulianaji wa risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba..
Maeneo yanayodhaniwa kuathirika sana ni yale ya Jebal.
Ujumbe huo unasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa rasasi ulishuhudiwa karibu na kambi ya umoja wa mataifa
Siku za hivi majuzi ziaidi ya watu 100 wanaripotiwa kuuawa mjini Juba wakati wa mapigano kati ya wafuasi wa rais Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar
Wawili hao walikubaliana kumaliza vita vya wenywe kwa wenyewe na wametoa wito wa kuwepo utulivu.
Ripoti za awali kutoka nchini Sudan Kusini zilisema kuwa takriban watu 100 waliuawa wakati wa mapigano kati ya wanajeshi hasimu katika mji mkuu Juba.
Hata hivyo idadi kamili bado haijulikani lakini wengi wa wale waliouawa wanaripotiwa kuwa wanajeshi.
Mapigano hayo yaliyoanza siku ya Alhamisi yaliendelea hadi mapema Jumamosi.
Mwandishi wa habari mjini Juba anasema kuwa wanajeshi wameweka vizuizi vya barabarani mjini humo.
Anasema kuwa masoko yamefunguliwa lakini watu wengi wamebaki nyumbani.
Sudan Kusini inaadhimisha miaka mitano ya uhuru wake.