Rais Obama atafupisha ziara yake katika mataifa ya kigeni na kwenda
Dallas wiki ijayo wakati mashambulizi ya risasi yaliyofanywa na kijana
mweusi ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliyetia nia ya kuwauwa polisi
wazungu.
Mauaji hayo yamesababisha miito ya haraka kuleta hali ya kuvumiliana nchini humo kutokana na matatizo ya kibaguzi.Polisi waligundua vifaa vya kutengenezea mabomu na silaha katika nyumba ya kijana huyo Micah Johnson mwenye umri wa miaka 25, mkaazi wa eneo la Dallas ambaye aliwapiga risasi polisi watano kabla ya kufariki katika mapambano ya silaha na polisi.
Ikulu ya Marekani ya White House imeondoa uwezekano wa mahusiano kati ya mshambuliaji huyo mwenye silaha na makundi yanayotambulika ya kigaidi, mahusiano katika ukurasa wake wa Facebook yanaelekeza katika makundi ya wanaharakati wenye msimamo mkali ya Wamarekani weusi ambayo yameorodheshwa kuwa ni makundi ya chuki nchini Marekani.
Akielezewa na polisi kuwa ni mshambuliaji aliyeamua kutenda kitendo hicho peke yake na hakuwa na rekodi ya uhalifu hapo nyuma , Johnson aliwaambia watu waliokuwa wanafanya nae majadiliano kabla ya kufariki kwamba alitaka kuwauwa polisi wazungu kwa kulipiza kisasi kutokana na kuuwawa kinyama hivi karibuni kwa watu wawili weusi.
Maandamano ya amani
Mashambulizi hayo jimboni Texas, ambayo yalizuka siku ya Alhamis usiku wakati wa maandamano ya amani dhidi ya ukatili wa polisi, yanakuja katika wakati wa hali ya kutafakari kuhusiana na matumizi ya silaha kwa ulinzi wa amani kuelekea Wamarekani weusi.
Viongozi wa harakati za Maisha ya Weusi ni muhimu wameshutumu mauaji hayo mjini Dallas, huku wakiapa kuendelea na maandamano yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa juma, huku makundi makubwa ya watu wakijikusanya usiku wa Ijumaa mjini Atlanta Georgia na wengine wengi wakiwa nje ya Ikulu ya Marekani White House.
Akihutubia maelfu ya watu katika sala iliyofanyika kwa heshima ya maafisa wa polisi waliouwawa, meya wa Dallas Mike Raswlings amewataka Wamarekani , kuimarisha hatua , kuponesha vidonda vya ubaguzi nchini humo.
Maandamano yataendelea
"Hatutajitenga na ukweli uliopo kwamba sisi kama wakaazi wa mji, wa jimbo, na kama taifa tunapambana na masuala ya kibaguzi," ameliambia kundi la watu waliokusanyika.
Rawlings amerudia ujumbe uliotolewa na rais Obama wakati taifa hilo linahangaika kutokana na ghasia hizo za hivi karibuni: Kwamba maisha ya weusi ni muhimu , na kama ilivyo kwa maisha ya wazungu, wale maafisa wa polisi.
"Tunapaswa kuongeza nguvu na kuyakabili masuala tata kwa njia nyingine," amesema Rawlings. "Na masuala ya kibaguzi yanautata."
Obama , ambaye ameamuru bendera zote zipepee nusu mlingoti katika majengo ya serikali kwa muda wa siku tano, aliweka wazi kwamba ghasia dhidi ya polisi, haziwezi kuhalalishwa kabisa."
Rais alizungumzia mashambulizi hayo akiwa katika mji mkuu wa Poland, Warsaw , ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa kilele wa NATO, na kuiita hali hiyo , "inayojirudia na ya kukera."
No comments:
Post a Comment