Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa limewaua wanachama 16 wa kundi la Boko Haram katika mapigano yaliyodumu saa kadhaa.
Msemaji
wa jeshi alisema kuwa mapigano hayo yalianza wakati washambuliaji wa
kujitolea mhanga waliokuwa wakitumia pikipiki walijaribu kuingia katika
kambi ya jeshi eneo la Rann karibu na mpaka na Cameroon.Wanajeshi wawili waliuawa huku wenyeji wakisema kuwa raia 7 nao walipoteza maisha yao.
Harakati za Boko Haram ambazo zimedumu kipindi cha miaka 7 zimesababisha vifo vya takriban watu 20,000 kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuwalazimu karibu watu milioni 2 kuhama makwao.
No comments:
Post a Comment