Saturday, April 30, 2016

MKURUGENZI WA IDARA YA MAAFA NCHINI ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA MAFURIKO


Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge wa viti Maalum (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akimweleza jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila (wa tatu kutoka kushoto) wengine ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia,Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava .
Baadhi ya wananchi katika kjiji cha Mandaka mnono ambao mashamba yao yameathirika kwa mafuriko.
Sehemu ya barabara inayounganisha vijiji vya Miwaleni na Mandaka Mnono ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko.
Usafiri wa pikipiki pekee ndio unatumika kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.(P.T)
Hivi ndivyo hali inavyoonekana.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,Mbazi Msuya akizungumza na wananchi katika eneo hilo lililoharibika vibaya.
Madereva wa bodaboda wakijaribu kupita katika eneo hilo kwa umakini mkubwa.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

Tuma Maoni

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Vibali vya kukamatwa dhidi ya Compaoré na Guillaume Soro vyafutwa



Wakazi wa Ouagadougou wakiweka vizuizi katika mitaa ya mji mkuu baada ya kutangazwa kwa mapinduzi ya serikali, Septemba 17, 2015.
Wakazi wa Ouagadougou wakiweka vizuizi katika mitaa ya mji mkuu baada ya kutangazwa kwa mapinduzi ya serikali, Septemba 17, 2015.
© AFP PHOTO / AHMED OUOB

Mahakama Kuu ya Ouagadougou imefuta kibali cha kimaiafa cha kukamatwa kiliyotolewa na vyombo vya sheria vya kijeshi dhidi ya aliyekuwa Rais wa Burkina Faso Blaise Compaoré na Spika wa Bunge la Cote d'Ivoire Guillaume Soro, Mwanasheria Mkuu wa Mahakama hiyo amesema.

"Vibali vyote vya kimataifa vimefutwa leo na Mahakama Kuu kutokana na kasoro za utaratibu. Uamuzi huo unahusu vibali vyote vilivyokua vinalenga kumkamata Blaise Compaoré, Guillaume Soro na wengine," Mwanasheria Mkuu wa Mahakama, Armand Ouedraogo, ameliambia shirika la habari la AFP.
"Uamuzi huo wa kufuta vibali hivyo umechukuliwa kutokana na kasoro za utaratibu kwa sababu ilikua inabidi kuomba maoni ya Kamishna wa serikali (Mwendesha mashtaka), maoni ya Mahakama ya kijeshi kabla ya kutoa vibali hivyo. Utaratibu huu haukutekelezwa, Mahakama imeamua kufuta vibali vyote vya kimataifa," Ouedraogo amesema.
Kamishina wa serikali amekiomba Baraza la udhibiti kisha Mahakama Kuu kwa kuweza kufuta vibali hivi, chanzo cha karibu na faili hii kimebaini.
"Ibara ya 130 ya Kanuni ya Jinai inamuagiza jaji maoni ya Mwendesha mashtaka kabla ya kutoa kibali chochote cha kimataifa cha kukamatwa," chanzo hicho kimesema.
Tarehe 4 Disemb 2015 vyombo vya sheria vya kijeshi nchini Burkina Faso vilitoa kibali cha kimataifa cha kukamtwa dhidi ya Blaise Compaoré, aliyekimbilia Cote d'Ivoire tangu utawala wake ulipoangushwa Oktoba 31, 2014.
Compaoré ameshitakiwa kwa kuhusika kwake katika mauaji ya Rais Thomas Sankara aliyeuawa Oktoba 15, 1987 wakati wa mapinduzi yaliyomueka madarakani.
Pia ameshitakiwa kwa "mauaji", ya raia wa Burkina Faso kama sehemu ya uchunguzi ulioanzishwa mwezi Machi 2015 na utawala wa mpito wa Burkina Faso.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Watu 13 wakisiwa kupoteza maisha katika ajali ya helikopta



Maafisa wa Idara za huduma za dharura wakiendelea na shughuli ya uokoaji katika eneo la ajali karibu na Bergen, Norway.
Maafisa wa Idara za huduma za dharura wakiendelea na shughuli ya uokoaji katika eneo la ajali karibu na Bergen, Norway.
REUTERS/Scanpix/Marit Hommedal

Watu 13 waliokua katika helikopta iliyoanguka katika pwani ya magharibi mwa Norway Ijumaa hii wanasadikiwa kuwa wamepoteza maisha, polisi ya nchi hiyo imetangaza katika magazeti mawili ya kila siku ya AFTENPOSTEN na VG.

Mamlaka ya safari za ndege nchini Norway, imechukua hatua za tahadhari ya kawaida, kupiga marufuku safari za helikopta aiana ya H225 Super Puma, muundo wa helikopta iliyofanya ajali.
“Watu wote waliokua ndani ya helikopta wanakisiwa kuwa wamefariki” amesema mratibu wa operesheni za polisi akinukuliwa na magazeti hayo mawili.
Mashahidi wanasema wameona kifaa cha injini ya helikopta kikidondoka kabla ya ajali hiyo, kwa mujibu wa vyombo vy habari vya Norway.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Zuma atakiwa kujibu mashtaka


Mahakama , Afrika Kusini imeamua Rais Zuma atapaswa kujibu mashtaka yaliyotupiliwa mbali mnamo mwaka wa 2009. Hata hivyo chama chake cha ANC kimesema uamuzi huo hauna maana kuwa Zuma ana makosa.
Mashtaka juu ya kashfa iliyohusu mkataba wa silaha wa mabilioni ya fedha yalifutiliwa mbali na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali, hatua iliyomfungulia njia bwana Zuma ya kuchaguliwa kuwa Rais, wiki chache tu baadae.
Akitoa hukumu, Hakimu wa Mahakama Kuu Aubrey Ledwaba alisema uamuzi wa kusimamisha kesi dhidi ya Zuma ulikuwa kinyume cha mantiki. Hakimu huyo amesema Rais Zuma lazima afikishwe mahakamani kujibu mashtaka.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Democratic Alliance, Mmusi Maimane amesema lazima Zuma afikiswhe mahakamani. Maimane ameeleza kuwa mtu yeyote, au Rais yeyote hapaswi kuwa juu ya sheria. Amesema wanachi wote wanapaswa kuwa sawa mbele ya sheria na kwa hivyo uamuzi wa kusimamisha kesi dhidi ya Zuma ulienda kinyume na mantiki.
Uamuzi uliotangazwa na Hakimu Aubrey Ledwaba unawaruhusu waendesha mashtaka kuanzisha tena kesi ya ufisadi dhidi ya Rais Jacob Zuma. Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani na chama cha upinzani cha Democratic Alliance,DA.
Zuma azidi kuzama katika dimbwi la matata.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance Mmusi Maimane
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance Mmusi Maimane
Rais Zuma tayari amebanwa kutokana na uamuzi wa Mahakama ya katiba kwamba Rais huyo alikiuka katiba, kwa sababu ya kushindwa kulipa fedha za umma alizotumia kwa ajili ya kukikarabati kijiji chake binafsi katika jimbo la lake za uzawa la Kwa -Zulu.
Mwendesha mashtaka aliuhalalisha uamuzi wa kuisimamisha kesi iliyokuwa inamkabili Zuma kwa sababu simu zilizodakizwa kati ya maafisa waandamizi wa utawala wa Rais Thabo Mbeki, zilionyesha ujiingizaji wa kisiasa katika kesi hiyo.
Nakala za simu hizo zilizoitwa "kanda za ujasusi",zilifichwa,lakini hatimaye zilitolewa hadharani mnamo mwaka wa 2014 na kukabidhiwa kwa chama kikuu cha upinzani, DA baada ya miaka mitano ya mapambano ya kisheria.
Kiongozi wa chama hicho Maimane amesema uamuzi uliotolewa na mahakama ni pigo kubwa kwa Rais Zuma.
Shinikizo la kumtaka Rais Zuma ajiuzulu linazidi kuongezeka na mashujaa kadhaa wa chama kilichomwezesha Madiba kuingia madarakani mnamo mwaka 1994 wanaunga mkono. Zuma anaepaswa kuimaliza mihula yake miwili mnamo mwaka wa 2019, hataweza kugombea tena urais.
Hata hivyo chama chake cha ANC kilichojaa makada wanaomtii, kinaweza kumwondoa madarakani kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu. Chama hicho kimesema baada ya kutangazwa hukumu dhidi ya Zuma kuwa haitaathiri nafasi yake katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Syria kusitisha mapigano baadhi ya maeneo


Syria imetangaza usitishaji wa mapigano wa muda mfupi karibu na Damascus na katika jimbo moja lakini haikutaja juu ya mapigano katika medani kuu ya mapambano katika mji wa Aleppo kufuatia kuibuka upya kwa mapambano.
Taarifa ya jeshi la Syria imesema utaratibu mpya wa utulivu kuanzia saa saba za usiku Jumamosi utadumu kwa siku moja tu katika kitongoji cha mjii mkuu cha Ghouta na siku tatu katika viunga vya kaskazini vya jimbo la mwambao la Latakia.
Vitongoji vyote viwili vimekuwa vikishuhudia kupamba moto kwa mapambano katika siku za hivi karibuni.Hata hivyo taarifa hiyo haikuutaja mji wa Aleppo wenye mapigano makali ambao umegawika kati ya maeneo yanayoshikiliwa na serikali na yale yalioko chini ya mikono ya waasi.
Mashirika ya habari ya Urusi yamemnukuu kiongozi mmoja wa upinzani akisema kwamba suluhu hiyo mpya pia itatumika Aleppo lakini hakuna uthibitisho tafauti kuhusu hilo.
Hatua za kijeshi na matumizi ya silaha ni marufuku
Wanajeshi wa Syria.
Wanajeshi wa Syria.
Taarifa ya kijeshi ya Syria haikutowa ufafanuzi juu ya maana ya neno la "utaratibu wa utulivu " lakini shirika la habari la Interfax nchini Urusi limemkariri afisa wa kituo cha kusimamia usitishwaji mapigano cha Urusi akisema inamaanisha hatua zote za kijeshi zitasitishwa na kupigwa marufuku kwa matumizi ya silaha za aina yoyote ile.
Generali Sergei Kuralenko mwenye kusimamia kituo hicho nchini Syria pia amesema kwamba haoni hatari ya hali hiyo kugeuka kuwa mzozo kamili wa kijeshi.Shambulio la anga kwenye hospitali ilioko katika mji wa Allepo limeuwa takriban watio 30 wakiwemo watoto watatu hapo jana.
Akizungumza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien Naibu Katibu Mkuu katika masuala ya Kibinaadamu na Mratibu wa Msada wa Dharura amesema kuna ishara nzuri sana za matumaini kwa mchakato wa kisiasa.
O'Brien) amesema "Tatizo ni kwamba watu hawawezi kuzungumza iwapo wanashambuliwa kwa mabomu, kwa bunduki za rashasha na kufa njaa.Kwa hiyo kuna haja ya kuwaelewesha watu kwamba usitishwaji wa mpigano lazima ufanye kazi vnginevyo inauyumbisha kabisa mzozo huo wa kisiasa."
Ujerumani yaonya
Msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Seibert.
Msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Seibert.
Serikali ya Ujerumani imesema Ijumaa shambulio katika hospitali ya Aleppo lilliouwa watu kadhaa yumkini ilikawa ni kazi ya vikosi vya serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Berlin Steffen Seibert amesema ni ukiukaji wa wazi wa sheria ya ubinaadamu.
Serikali ya Ujerumani imeonya kwamba kupamba moto kwa mapigano huko Aleppo kunatishia kudhoofisha mazungumzo ya amani ya Geneva na kuwa hilo halina budi kuepukwa na kwamba Urusi ina wajibu wa kuzuwiya kusambaratika kwa usitishwaji wa mapigano na mchakato wa kisiasa.
Mkuu wa masuala ya haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein naye ameyashutumu mataifa makubwa yenye kuunga mkono pande zinazohasimiana nchini Syria kwa kuwa washiriki katika umwagaji damu nchini Syria pamoja na kukiita kitendo cha kushindwa kupigania haki za wahanga wa vita hivyo kuwa cha aibu.
Kauli yake inaonekana kuikusudia Marekani yenye kuwaunga mkono makundi fulani ya waasi na Urusi mmungaji mkono mkuu wa Rais Bashar al- Assad.Serikali ya Syria inaelezea suluhu waliyoitangaza katika baadhi ya maeneo ni juhudi za kuyaokowa makubaliano ya kukomesha uhasama.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Kenya kuchoma moto tani za pembe za ndovu na faru


Kenya inajitayarisha kuchoma moto tani 105 za pembe za ndovu na faru leo Jumamosi (30.04.2016), ambapo Leonardo DiCaprio na Elton John watakuwa miongoni mwa watu watakaohudhuria tukio hilo.
Elfenbeinverbrennung in Kenia
Kiasi cha tani 105 za pembe za ndovu zitakazochomwa moto nchini Kenya
Kenya itachoma tani 105 za pembe za ndovu na zaidi ya tani moja ya pembe za faru leo Jumamosi (30.04.2016) ikiwa sehemu ya kupambana na majangili.
Leonardo DiCaprio na Elton John ni miongoni mwa watu mashuhuri watakaoshuhudia lundo la pembe za ndovu likichomwa moto wakati wa tukio hilo la kwanza la aina yake tangu mwaka 1989.
Elfenbeinverbrennung in Kenia
Mmoja kati ya walinzi wa wanyama pori nchini Kenya akipanga pembe hizo
Kwa mujibu wa wakfu wa wanyama pori barani Afrika AWF, kiasi cha pembe za ndovu 35,000 wameuwawa katika bara la Afrika mwaka jana, kutoka jumla ya tembo 500,000.
Hali ni mbaya zaidi kwa faru. Tangu mwaka 1960, karibu asilimia 98 ya faru weusi wa Afrika, wameuwawa.
Biashara haramu
Kilo moja ya pembe ya ndovu inaripotiwa na shirika linalopigania ulinzi wa wanyamapori kuwa ina thamani ya dola 1,100 katika soko la chini kwa chini, wakati pembe ya faru inakwenda mara 50 zaidi ya kiasi hicho, na China ikiwa ndio soko kuu.
Thailand Zoll beschlagnahmt 3 Tonnen Elefantenstoßzähne
Pembe za ndovu zikipangwa
Mashirika ya ulinzi wa mazingira yameeleza kuunga kwao mkono kuharibiwa kwa shehena hiyo. "Kuhifadhi pembe hizo zilizokamatwa ni kazi kubwa na yenye gharama kubwa," amesema Daniela Freyer kutoka shirika la Pro Wildlife.
Pia kuna hatari, wakati mataifa masikini yanaweza kupata fedha nyingi kwa kujiingiza katika biashara haramu ya pembe za ndovu.
Serikali ya Kenya kwa muda mrefu ilikuwa inataka kupigwa marufuku biashara hiyo duniani, wazo litakalojadiliwa tena katika mkutano wa shirika la CITES ambao unaanza mjini Johannesburg mwishoni mwa mwezi Septemba.
Deutschland Uhuru Kenyatta in Berlin
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Nchi nyingi zimepiga marufuku biashara ya pembe za ndovu katika miaka ya 1980, lakini kuna tofauti, wakati China na Japan zinaruhusu kununua pembe hizo kutokana na kulegezwa kwa vizuwizi, Freyer amesema.
Wanastahili maisha zaidi
Mamlaka ya hifadhi ya mali asili nchini Kenya imelitangaza tukio la leo Jumamosi katika ukurasa wa Twitter chini ya hashtag: "worthmorealive" wanastahili maisha zaidi.
Dai hilo hakika ni la kweli kwa ajili ya nchi hiyo ya Afrika mashariki ambayo ni maarufu kwa utalii, ambayo imejipatia kiasi ya dola bilioni 2.2 ama kiasi ya asilimia 4 ya pato jumla la taifa kutokana na utalii mwaka jana, kwa mujibu wa shirika la utalii la dunia.
Großbritanien BAFTA 2016 Leonardo DiCaprio
Mcheza sinema Leonardo DiCaprio atakuwapo katika tukio hilo nchini Kenya.
Zaidi ya asilimia 9 ya wakaazi milioni 46 nchini Kenya wanafanyakazi katika sekta hiyo, wakati idadi inaongezeka kila mwaka. Watalii wanavitiwa nchini humo na maili kadhaa za fukwe nzuri katika bahari ya Hindi na mbuga za wanyama ndani ya nchi hiyo.
Gavin Shire kutoka kitengo cha samaki na wanyamapori nchini Marekani FWS amesema kwamba maafisa wa Kenya wanahitajika kuhakikisha kwamba pembe hizo zinaharibiwa katika njia ambayo inafanya soko haramu la pembe hizo linakuwa halifai.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Hii Video mpya ya Lil Durk ‘Mud’ Enjoy


Lil Durk gets down and dirty. After delivering that “Good Good” and “Trap House,” the Chicago spitter unleashes the music video for “Mud,” a single off his 300 Days, 300 Nights mixtape.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Puff Daddy atangaza kustaafu muziki na hii ndio kazi nyingine atakayofanya.


Rapa,Producer, mwigizaji na mfanya biashara maarufu Puff Daddy ametangaza rasmi kuwa album ya No Way Out 2 na kwamba baada ya hapa atastaafu muziki.
Pdd ni CEO wa Bad Boys Entertainment na ameweka wazi kuwa baada ya kustaafu muziki kazi yake kubwa itakuwa kuigiza na kutayarisha filamu tu.
Puff Daddy aliyetumikia muziki kwa miaka 20 amesema pia baada ya kuachana na muziki atatumia muda wake mwingi na watoto wake sita.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Hii video mpya ya Young Thug ‘Texas Love’ Enjoy


Young Thug amedondosha video mpya ya wimbo wake wa “Texas Love.” na kwenye wimbo huu anaimba “If Texas love was a drug…” huku akikata coabo kwa kuimba “No features, I don’t do features / I don’t like leeches.” Wimbo upo kwenye mixtape yake ya ‘I Came From Nothing 4’.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Drake asema Kanye West ni role model wake,kuna kazi kubwa wanafanya pamoja.


Wamiliki wa lebel kubwa za OVO na G.O.O.D. Music Drake na Kanye wanaelekea kufanya colabo au mixtape kubwa hivi karibuni.
Kwenye interview na Zane Lowe Drake amesema alimwangalia Kanye West kama role model wake toka akiwa msanii mchanga na Kanye West anamchango kubwa sana kwa yeye kuwa hapa leo.
Drake amesema wawili hawa walikuwa na mpango wa kutoa mixtape ila ratiba zilingiliana na sasa wana mpango wa kufanya kazi nyingine kubwa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Hii video mpya ya Flo Rida Ft Jason Derulo ‘Hello Friday’ Enjoy.


Hii video mpya ya bata refu sana kutoka kwa Flo Rida na Jason Derulo “Hello Friday.” Wimbo wa Flo Rida wa mwisho “My House,”ulishika namba 4 kwenye Billboard Hot 100.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Hii video ya chizi matatoo Machine Gun Kelly ‘All Night Long’ Enjoy


MGK aka Machine Gun Kelly amerudi kwenye kiki kubwa na video yake mpya ya “All Night Long” kutoka kwenye cd yake ya mwaka jana ya General Admission.
Bonyeza Play Kuitazama
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Wenger: Benki zilitaka nisalie kocha wa Arsenal


Image copyrightEPA
Image captionArsene Wenger
Mkufunzi wa timu ya Arsenal Arsene Wenger sasa anasema kuwa uwepo wake katika kilabu hiyo uliisaidia kilabu hiyo kupata mkopo wa ujenzi wa uwanja wa Emirates.
Mashabiki wanatarajiwa kufanya maandamano wiki hii baada ya kukasirishwa na matokeo ya kilabu hiyo msimu huu ambayo yamesababisha timu hiyo kushindwa kushinda taji la ligi.
''Wakati tulipojenga uwanja wa Emirates, benki zilitaka niweke sahihi ya mktaba wa miaka mitano'',alisema Wenger mwenye umri wa miaka 66.
''Wataka kujua ni kilabu ngapi nilikataa wito wao wakati huo''?
Ujenzi wa uwanja wa Emirates uliogharimu pauni milioni 390 ulianza mwaka 2004,mwaka ambapo Wenger alishinda taji lake la mwisho la ligi na kilabu hiyo.
''Benki zilitaka niendelee kuhudumu ili wawe na hakika ya kulipwa fedha zao'',aliongezea Wenger ambaye amekuwa akiisimamia kilabu hiyo tangu mwaka 1996.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Barcelona: Tunakabiliwa na upinzani mkali


Image copyrightAFP
Image captionLuis Enrique na Lionel Messi
Klabu ya Barcelona italazimika kushinda mechi zake zote za mwisho ili kushinda taji la ligi ya La Liga kwa kuwa huenda wapinzani wao wasipoteze hata pointi moja kulingana na kocha Kuis Enrique.
Viongozi Barcelona walioanza mwezi wa April wakiwa na pointi nane kileleni mwa ligi hiyo,wako sawa kwa pointi na Atletico Madrid huku Real Madrid ilio nafasi ya tatu wakiwa nyuma kwa pointi moja.
''Haiwezekani kwamba timu zilizo nyuma yetu zitapoteza pointi'',alisema Enrique siku ya Ijumaa.
Image copyrightGetty
Image captionReal Madrid na Atletico Madrid
''Mchezo wetu ni mzuri katika kipindi hiki cha mwisho''.
Barcelona iko mbele ya Atletico kutokana na tofauti ya mabao.
Barca,Atletico na Real Madrid zote zinacheza Jumamosi katika muda tofauti.
Image copyrightGetty
Image captionReal Madrid dhidi ya Barcelona
KIabu ya Zinedine Zidane inaweza kwa masaa machache kupanda katika kilele cha ligi iwapo itashinda dhidi ya Real Sociedad katika mechi ya mapema.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mtoto wa miaka 2 amuua mamake Marekani


PriceImage copyrightAP
Image captionPrice alipigwa risasi na mwanawe akiendesha gari
Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa katika mji wa Milwaukee, Marekani.
Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari.
Mwanamke huyo, Patrice Price, 26, alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye ni mlinzi na ambaye alikuwa ameacha bunduki yake kwenye gari, babake Andre Price amesema.
Polisi wa Milwaukee wanasema mwanamke huyo alipigwa risasi moja kutoka nyuma akiendesha gari mapema Jumanne asubuhi.
Mamake Price na mwanawe mwingine wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja walikuwa kwenye gari hilo wakati wa kutokea kwa kisa hicho.
Bw Price alisema ana binti mwingine mkubwa, lakini akasema Patrice alikuwa na bidii sana.
“Sasa hayupo nasi tena. Inaniuma sana,” Bw Price aliambia kituo cha habari cha WISN, Milwaukee.
Mwezi uliopita, mvulana wa umri wa miaka minne alimpiga risasi mamake Jamie Gilt katika jimbo la Florida katika hali sawa.
Bi Gilt alinusurika na majeraha.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Jumba lililoporomoka lawaua watu 7 Nairobi


Image captionJumba lililoporoka Nairobi
Polisi katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wanasema kuwa takriban watu saba waliuawa wakati nyumba moja ilipoanguka katika mtaa mmoja mjini humo.
Waokoaji wanaendelea kutafuta watu wanaohofiwa kukwama ndani ya vifusi vya jengo hilo la ghorofa sita kufuatia mvua kali inayoendelea kunyesha ambayo imesababisha mafuriko.
Takriban watu 120 wameokolewa kufikia sasa katika mtaa huo wa Huruma.
Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa takriban familia 150 ziliathiriwa na mkasa wa jumba hilo lililojengwa miaka miwili iliopita
Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya Mama Lucy iliopo mjini humo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Forbes wametaja vijana 30 wa Afrika wanaotarajiwa kuwa wafanyabiashara wakubwa, Mtanzania akiwemo


Forbes wametaja list ya vijana 30 wajasiriamali kutoka nchi tofauti tofauti za Afrika, vijana ambao wanatazamiwa kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa kwa siku za usoni, list ya vijana hao 30 wanaotajwa kutoka sehemu mbalimbali Afrika wametajwa na kuelezewa historia zao za miradi yao midogo waliyoanza nayo.
Katika list ya vijana 30 wanaotajwa na Forbes na wanatarajiwa kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa kuna jina la mtanzania pekee ambaye Tanzania inapaswa kujivunia. Jina la Nadeem Juma ndio jina la mtanzania pekee lililotajwa kuwa katika list ya vijana hao 30.
Cover01
Nadeem Juma
Kama humfahamu Nadeem Juma ni mwenyekiti wa kampuni ya  AIM Group. Nadeemni kijana wa Tanzania aliyeanza kufanyabiashara akiwa na umri wa miaka 19 kwa kuanzisha shule ya kimataifa ya Dar es Salaam International Academy (DIA).
Nadeem aliamua kuanzisha shule hiyo ya kimataifa baada ya kuona kuna ulazima waTanzania kuwa na shule itakayotoa elimu ya viwango vya kimataifa, kwani kwa kipindi hicho Tanzania kulikuwa hakuna shule za viwngo na asilimia kubwa wazazi wengi walikuwa wanalazimika kupeleka watoto wao KenyaSouth Africa na Swaziland.
Haya ndio majina ya vijana wengine wa Afrika waliotajwa na Forbes katika list ya wajasiriamali 30
  • Simbarashe Mhuriro, Zimbabwe
  • Ntombenhle Khathwane, Swazi
  • Olatorera Oniru, Nigerian
  • Bonobo Ramokhele, South Africa
  • Thato Kgatlhanye & Rea Ngwane, South Africa
  • Lee Grant, South Africa
  • Samuel Malinga, Uganda
  • Vanessa Zommi, Cameroon
  • Neo Ramaphakela, South Africa
  • Mutoba Ngoma, Zambia
  • Hilda Moraa, Kenya
  • Eugene Mbugua, Kenya
  • Jamie Pujara, Kenya
  • Tyrone Moodley, South Africa
  • Rachel Sibande, Malawi
  • Mike Chilewe Jr, Malawi
  • Kelvin Name, Rashad Seini na Kofi Amuasi, Ghana
  • Ogunlana Olumide Chukwuwezam Obanor, Nigeria
  • Kasope Ladipo-Ajai, Nigeria
  • Yasmine El Baggari, Morocco
  • Aisha Ayensu, Ghana
  • Anda Maqanda, South Africa
  • Trushar Khetia, Kenya
  • Abiola Olaniran, Nigeria
  • Clarisse Iribagize, Rwanda
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mengine yalioandikwa kuhusu Jose Mourinho na Man United


Bado headlines za kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal kutimuliwa na ndani ya Man United na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho zinazidi kuchukua headlines, huu ni mtihani ambao majibu yake yatajulikana mwisho wa msimu baada ya Ligi Kumalizika.
Hadi sasa habari za Jose Mourinho kujiunga na Man United hazina uhakika wala dalili kama kweli atajiunga na Man United au la, kwani leo Sky Sports wameripoti kuwa Jose Mourinho hana makubaliano yoyote na Man United, licha ya kuwa amekuwa akiripotiwa kutaka kujiunga na Man United.
Hayo yameripotiwa na Sky Sports lakini The Sun imeandika kuwa klabu ya Man Unitedimemuhakikishia Jose Mourinho kuichukua nafasi ya Louis van Gaal mwisho wa msimu, licha ya kuwa mwenyekiti wa Man United Ed Woodward anaripotiwa bado anafikiria juu ya maamuzi hayo ambayo yamekuwa topic kubwa katika mitandao.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Jipya kuhusu kifo cha Pamba Wemba, tazama huyu jamaa kwenye video


Taarifa  ambazo zinazidi kuenea kwenye vyombo vya habari Congo na mitandao ya kijamii hata hapa Tanzania ni msiba wa Papa Wemba lakini sasa mjadala umehamia kwenye namna kifo chake kilivyotokea
Kipande cha video kinachomuonesha jamaa akichukua mic halafu akairudisha kwenye stage na baada ya Pamba Wemba Kuanguka inadaiwa jamaa yuleyule badala ya kumsaidia alikimbilia mic ili isijulikane. Taarifa zinazoenea ni kwamba mic ile ilikuwa imewekewa sumu.
Hapa Mwanamuziki wa Congo anayeishi Tanzania, Papii Catalogue ameitafsiri video hiyo kwa lugha ya kiswahili, unaweza kuitazama……
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.