Saturday, April 30, 2016

Dubai kwenye mpango mpya utakaovunja rekodi ya dunia

Dubai ni mji ambao kwa sasa watanzania wengi wanaenda kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali, Dubai  umekua kwa haraka zaidi kutokana na kuweka vizuri njia za ukusanyaji wa mapato na ni mfano ya mji ambao Uongozi wake unafanya kazi kwa kuwa baada ya miaka 25 macho ya Dunia nzima yamehamia Dubai.
Dubai wameelezea mipango yao zaidi kwenye mji huo ambapo maeneo ya makazi mapya, Dubai Creek Harbour yatauzunguka mjengo mrefu ambao bado haujapatiwa jina lakini nickname yake ni ‘the needle‘. Mjengo huo utakuwa mrefu kuzidi uliopo wa Burj Khalifa  wenye 2,717 ft na umepangwa kujengwa 2020.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

KUMBE RAY KIGOSI KAMUIGA MESSI KUNYWA MAJI?

lionel-messi-museum

Kwa hili la Messi huenda Ray Kigosi ameiga,kila mmoja huwa anapenda kula vyakula haswa kwa sisi wa hali ya chini mara nyingi hupendelea kula ugali kwa nchi za Afrika tatizo pesa sio kwamba hatupendi kula vitamu na vizuri lakini kuna watu wanapenda kula baga wengine wali lakini kwa Mwanasoka bora wa Dunia mara tano Lionel Messi anapenda kula na hivi vifuatavyo .

ANAPENDA KULA NINI?

Licha ya vyakula vingine, lakini Lionel Messi anapendelea sana kula nyama nyekundu, mtandao wa Mail Online na Mundo Deportivo imeripoti kuwa Messi anakula kiasi kikubwa cha nyamamessi

1.Anakunywa maji mengi

2.Matunda na mboga za majani kwa wingi

3.Anatumia mafuta yajulikanayo kama OLIVE

4.Hapendi vyakula vilivyopuliziwa madawa

5.Hapendi vyakula vyenye sukari nyingi

6.Anakula kwa wingi nyama nyekundu

Kwa wenye kumbukumbu sahihi, Mrisho Ngasa alishindwa kula kuku mzima pale London alipokwenda kujaribu bahati yake Westham United akaja Didier Dogba amekula kuku wawili pale Serena wakawa wanamshangaa tusubiri Farid Mussa nae kapata timu daraja la pili huko  Hispania.

TOTO VS YANGA,PLUIJM ANADI USHINDI

KOCHA wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, Hans Pluijm ametamba timu yake leo kuibuka na ushindi dhidi ya Toto Africans ili kuzidi kukaribia kutetea taji hilo.

Akizungumza  wakati wa mazoezi ya timu hiyo jijini hapa, Pluijm alisema kuwa licha ya uzuri wa Toto Africans, lakini wataibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo CCM Kirumba.

“Jambo muhimu kwetu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi ili tuweze kubaki kileleni mwa Ligi Kuu na kutwaa taji.” alisema Pluijm.

“Golikipa wetu Barthez na Godfrey Mwashiuya ni majeruhi ila nina imani mapengo yao yatazibwa na wachezaji waliopo,” alisema Pluijm.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Toto Africans, Dominik Glawogger alisema anategemea vijana wake watacheza vyema na kuweza kuifunga Yanga.

ARSENAL WAMTAKA DIEGO SIMEONE BADALA YA WENGER

Mashabiki wa Arsenal wamemshambilia meneja wa timu hiyo Arsene Weger katika mtandao wa twitter na kumtaka aondoke na nafasi yake ichukuliwa na raia wa Argentina, Diego Simeone.Diego Simeone (Atletico Madrid)Wamesisitiza kuwa timu ya Arsenal chini ya Wenger haijatwaa ubingwa wa Ulaya tangu mwaka 2004 na wala haijashinda UEFA Champions League hata mara moja.

Aidha mashabiki hao walimkubali zaidi Diego Simeone baada ya kuiongoza vyema klabu yake ya Hispania Atletico Madrid na kufanikiwa kuwafunga vigogo wa Ujerumani Bayern Munich 1-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya UEFA.

Kambi ya Wenger msimu huu imetikisika kwa kias kikubwa kutokana na shinikizo kutoka kwa wadau wa klabu hiyo na kusababisha kuharibika kwa mbio zao za ubingwa walizoanza vyema.

DAR YAJITENGA NA UMILIKI WA UDA

UMILIKI wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa Jiji la Dar es Salaam, umekoma rasmi baada ya Kampuni ya Simon Group kukamilisha malipo ya ununuzi wa hisa za jiji hilo katika shirika hilo ambazo ni asilimia 51.UDA

Kutokana na kukamilika kwa malipo hayo, sasa Uda inamilikiwa Kampuni ya Simon Group yenye asilimia 51 ya hisa ambazo ndizo zilizokuwa hisa za Jiji na Serikali yenye asilimia 49.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru alisema mpaka katikati ya Aprili, mwaka huu, Kampuni ya Simon Group ilikuwa imemaliza kulipia malipo ya hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na Jiji.

Kwa mujibu wa Mafuru, sasa Serikali inapaswa kuitambua Kampuni ya Simon Group kuwa mwenye hisa katika shirika hilo, kwa kuwa kampuni hiyo imewasilisha nyaraka za ununuzi wa hisa hizo na Jiji limethibitisha kupokea fedha zao na kukubali kwamba muamala huo wa malipo ni halali.

Akifafanua namna ununuzi huo ulivyo halali, Mafuru alisema Jiji walifungua kesi kuomba mahakama iagize Kampuni ya Simon Group ilipe fedha za hisa za Jiji kufikia Aprili 30 mwaka huu, kinyume cha hapo hisa hizo zirudishwe kwa Jiji la Dar es Salaam.

MJADALA JUU YA MAFUTA YA UGANDA WAANZA

Waziri wa Nishati wa Uganda Bi. Irene Muloni pamoja na timu ya wataalamu wa wizara yake wapo nchini kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka nchini humo hadi jijini Tanga.

Bomba hilo litakalojengwa kwa ushirikiano baina ya serikali za Uganda na Tanzania, awali lilikuwa lipitie nchini Kenya na litakuwa likisafirisha mafuta ghafi kutoka eneo la magharibi mwa Uganda mahali ambako imegundulika hazina kubwa ya nishati ya mafuta.

Mwenyeji wake, Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospeter Muhongo amewaambia waandishi wa habari  kuwa mbali ya bomba la mafuta, mkutano huo unaohusisha wataalamu kutoka nchi zote mbili, utajadili pia ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Tanzania kwenda nchini Uganda.muhongoKwa mujibu wa Profesa Muhongo, bomba la gesi litatumika pia kupeleka nishati hiyo katika mikoa ya kanda ya ziwa, kwa kutumia michoro na miundombinu itakayopita kwenye eneo lile lile ambako bomba la mafuta litajengwa.

ZITTO:TAKUKURU PELEKENI MAHAKAMANI WAHUSIKA WA ESCROW

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo) ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuwafikisha mahakamani wahusika wa sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow ili sheria ichukue mkondo wake.

Zitto aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akichangia kwenye hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, iliyowasilishwa na Waziri Angela Kairuki pamoja na ile ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), iliyowasilishwa na Waziri wake, George Simbachawene.zitto-kabwe-facebook-front

Alisema mwaka 2014, Takukuru waliijulisha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwamba ilikuwa inachunguza na kumaliza uchunguzi kuhusu miamala ya kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenda Benki ya Stanbic Tanzania.

Alisema katika taarifa zote ambazo Takukuru inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna mahali inapozungumzia maendeleo ya suala hilo. “Hata siku moja hakuna mahala Takukuru wanasema kuhusu uchunguzi huu na lini wahusika waliochota fedha za umma watafikishwa mahakamani.

Naomba tupate kauli ya serikali kuhusu jambo hili kwani ni moja ya jipu,” alisema Zitto ambaye aligusia suala la ukiukwaji wa Sheria ya Bajeti. Alisema kuna ukiukwaji kadhaa wa sheria ya bajeti kama vile sheria namba 11 ya mwaka 2015, ambapo kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinaeleza namna ambavyo mfumo wa Bajeti ya Serikali unapaswa kuwa.