Saturday, January 21, 2017

Mbilia Bel aibuka na album mpya, asema ni ya mwisho

Mwanamuziki wa Congo Mbilia Bel
Mwanamuziki wa Congo Mbilia Bel
Mbali na kusheherekea kuzaliwa kwa kutimiza miaka 57, mwanamuziki huyo Mboyo Moseka, aliyevuma kwa jina la “Mbilia Bel” na kukonga nyoyo za watu wengi ameadhimisha pia miaka 40 ya kuweko kwake katika tasnia ya muziki.
Album yake mpya ya kuwaaga wapenzi wa muziki wake inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.
Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA Saleh Mwanamilongo amesema kustaafu kwake mwanamke huyu mashuhuri kutoka kwenye tasnia ya muziki, kumekuja mwezi mmoja baada ya kuzuka kwa taarifa kwamba amefariki.
Mbilia Bel
Mbilia Bel
Kwenye kanda ya video ya dakika 5 aliyorikodi, Mbilia Bel amesema kwamba ataendelea kuwa mshauri wa wasichana chipukizi wanawania kuingia katika tasnia ya muziki hivi sasa.
Mwanamuziki Mbilia Bel, alipata sifa kubwa katika miaka ya 70 na thamanini kutokana na sauti yake nyororo.
Lakini hasa baada ya kujiunga na mwanamuziki TabuLey Rochereau. Pamoja na Tabu Ley, supasta huyu alipata umaarufu baada ya kuimba nyimbo nyingi zilitotungwa na Rochereau.
Kwa mfano nyimbo yake ya “Eswi yo wapi” inayomaanisha “kwa nini umekerwa” ikiwa ni wimbo wa fumbo baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rochereau.
Wimbo mwingine maarufu sana nchini ni “yamba ngaa” unaomaanisha “nipokee mpenzi.”
Mbilia Bel na Tabu Ley walizaa mtoto wa kike, Meledoy Tabu ambaye pia ni mwana muziki hivi sasa.
Baada ya kuvunjika kwa uhusiano wake na Tabu Ley, Mbilia Belaliunda bendi yake mwenyewe na kuimba nyimbo nyingi … kama Manzili Manzili kwa lugha yao ya kinyansi, kutoka jimbo la Bandundu kusini magharibi mwa DRC.
Hivi sasa Mbilia Bel amemaliza kurikodi album mpya ambayo inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.
Album hiyo mpya anayoita “Signature” au saini ina nyimbo 21.
Katika ukanda wa Afrika mashariki Mbilia Bel ataendelea kumbukwa hasa kutokana na wimbo unaoitwa Nairobi.

Trump alenga Obamacare

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri za serikali mojawapo ikiwa ni agizo linalolenga kuifuta bima ya Afya iliyoanzishwa na mtangulizi wake Barrack Obama maarufu kama Obamacare. Agizo hilo lenye lengo la kuipunguzia serikali mzigo wa kiuchumi, linaziamuru taasisi za kiserikali kukomesha hatua zitakazoendeleza bima hiyo inayofadhiliwa na serikali. Badala yake linataka taasisi hizo kupunguza, kuchelewesha au kufutilia mbali gharama za matibabu ambazo zilishughulikiwa na bima hiyo. Hatua ambayo itaweka gharama hiyo kwa serikali za majimbo na watu binafsi. Bima hiyo huwawezesha mamilioni ya wamarekani wasiojiweza kupata huduma ya afya kwa gharama nafuu. Kuiondoa kabisa bima hiyo kutahitaji mswada kupitishwa katika bunge la Marekani

Vigogo 5 jela miaka mitano


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewakuta na hatia na kuwahukumu kifungo cha miaka 5 jela au kulipa faini ya Sh milioni 100 kila mmoja vigogo watano waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya rushwa na utakatishaji wa fedha.
Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dar es Salaam jana ilisema kesi hiyo iliyoendeshwa kwa muda mrefu na kufuatiliwa na watu wengi ilifunguliwa Julai 21, mwaka 2010.
Taarifa hiyo ya Takukuru iliyotolewa na Ofisa Uhusiano wake Mussa Misalaba iliwataja washtakiwa waliopatikana na hatia kuwa ni Justice Lumina Katiti aliyekuwa Mhasibu Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Marcus Mussa Masila aliyekuwa Mhasibu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL.
Wengine ni Kanuti Ferdinand Ndomba mfanyabiashara wa Kampuni ya UEE Tanzania Limited, Gidion Wasonga Otullo mfanyabiashara wa kampuni ya East Africa Procurement Services na Robert Phares Mbetwa mfanyabiashara kutoka kampuni ya Romos Technology Limited.
Kesi hii iliendeshwa na waendesha mashtaka kutoka ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) na TAKUKURU ambao ni Awamu Mbagwa (DPP), Shedrack Kimaro (DPP), Estazia Wilson (DPP) na Marx Ally (Takukuru).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Takukuru, hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama hiyo Januari 17 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Renatus Rutatinisibwa baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hivyo kuwatia hatiani washtakiwa kwa jumla ya makosa 51 ya rushwa na utakatishaji wa fedha haramu.
Washtakiwa walipelekwa Magereza kutumikia kifungo cha miaka 5 baada ya kushindwa kulipwa faini hiyo ya Sh milioni 100.
Ilidaiwa kuwa kati ya mwaka 2007 na 2009 watuhumiwa kwa kushirikiana walikula njama kuchepusha Sh 3,399,251,740.24 za TTCL zilizokusudiwa kulipa kodi TRA na kulipwa kinyume cha sheria kampuni ya UEE. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Masila aligushi sahihi za watia sahihi wa TTCL na kubadili fomu za TIS zilizokusudiwa kupeleka fedha TRA na kuweka jina la UEE.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa Katiti alionesha kwenye mfumo wa TRA kuwa TTCL ilikuwa imelipa kodi zote. Ilidaiwa kuwa kati ya mwaka 2008 na 2009 Katiti , Masila, Wasonga na Mbetwa walijipatia mali nyingi na kununua magari ya kifahari na nyumba kutokana na fedha hizo haramu.

Trump aanza kufanyia mabadiliko sheria za Obama


Trump na mkewe wakitembea Washington
image caption Trump na mkewe wakitembea Washington
Rais wa Marekani Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais, baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yalioafikiwa na mtangulizi wake Barak Obama.
Muda mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake, Bw Trump, alitia amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu inayofahamika kama Obamacare, ambayo Trump aliahidi kufanyia marekebisho.
Trump pia ametia saini amri ya kuwaidhinisha mawaziri wake wapya wa Ulinzi na usalama wa kitaifa ambao uteuzi wao umepitishwa na bunge la seneti.
Utawala wa Trump pia umeaanza kufanyia marekebisho mtandao wa kijamii wa Ikulu ya White House kwa kuweka masuala yatakayopatiwa kipaumbele na uongozi huo mpya.

Gumzo la Navy Kenzo kwenye picha ya pamoja na Pah One limetolewa ufafanuzi

Kundi la PAH ONE lilivunjika mwaka 2012 na ikafanya Aika na Nahreel waliokuwepo kwenye kundi hilo wakaunda kundi la NavyKenzo ambalo mpaka leo lipo.
Kilichoteka Internet ni picha aliyoipost Aika ikionyesha wakiwa pamoja na wale wa zamani waliokua wanaunda PAH ONE, Nahreel amekaa mbele ya AyoTV na kusema yafuatayo >>> ‘Tumekua tukikutana hapa na pale hata kama watu wanaona tulikua mbalimbali’

Kila mtu amekua akisema tumemiss kitu ambacho tulikua tunakiona mwanzo hata sisi wenyewe kwenye mioyo yetu tulikua tunatamani siku ije itokee tena, washkaji walituchek na kusema kwanini tusifanye kitu…….. mimi na Aika tukaaamua kukaa chini ili tufanye kitu, tuko nao kwenye mazingira ya kufanya kazi pamoja kama THE INDUSTRY’ – Nahreel
Tazama hii video hapa chini kuwaona wote wakizungumza Exclusively kwenye AyoTV Entertainment…

VIDEO: Gari lilivyochomwa moto Washington DC. na waandamanaji wanaompinga Donald Trump

Wanasema haijawahi kutokea fujo za namna hii kwenye historia ya Marais wapya Marekani, hii imetokea kwenye mji wa Washington DC. wakati huu ambao Rais Donald Trump ameapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani.
Waandamanaji wanaompinga waliandamana kwa wingi kwenye mitaa mbalimbali ya mji huo wakiwa na Mabango na wakipaza sauti kuonyesha wazi kwamba hawamtaki na wengine walivunja vioo vya Maduka, Magari na hata kuchoma moto gari moja la kifahari.
Katika kuonyesha kwamba hawaogopi, Waandamanaji hao walivunja mpaka kioo cha gari la Polisi lililopita katikati yao kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini, inasemekana hadi sasa ni zaidi ya Waandamanaji 100 wamekamatwa na Polisi.

Rais Wa Gambia Akubali Kuachia Madaraka

Yahya Jammeh ambaye amekua madarakani na kuingoza Gambia kama Rais kwa miaka 22 hatimae amekubali kuachia madaraka hayo na sasa Adama Barrow aliyetangazwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu ndio anatarajiwa kuchukua nafasi.

Kupitia Television ya taifa, Yahya ametangaza kuachia madaraka ambapo AlJAZEERA wameripoti kwamba taarifa kutoka IKULU zilisema baada ya kuachia madaraka alitarajiwa kuondoka kwenye nchi hiyo ndani ya siku 3 ila media nyingine zinasema amepewa saa tu za kuondoka.

TV ya habari Nigeria imesema ECOWAS walimpa hadi saa sita mchana kuondoka lakini mwenyewe akaomba muda huo usogezwe hadi saa kumi jioni na imeripotiwa atakwenda kuishi Guinea.

Barrow aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kusema ‘Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka na anatarajiwa kuondoka kwenye nchi ya Gambia leo’