Friday, April 28, 2017

Rais Magufuli kupokea taarifa vyeti feki LEO

RAIS John Magufuli leo anatarajiwa kupokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais katika Ikulu Ndogo ya Chamwino Dodoma, Jaffar Haniu ilisema taarifa hiyo itawasilishwa kwa Rais Magufuli na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki.

Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma liliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba, 2016. 
Hivi karibuni wakati akifungua rasmi nyumba mpya za makazi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Rais Magufuli alisema anasubiri ripoti kuhusu watumishi wa umma wenye vyeti feki wapatao 9000.

“…Kwa hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo kwa sababu mlinichagua kwa ajili hiyo,” alisisitiza Rais katika hotuba yake hiyo.

Sunday, April 9, 2017

Uganda yamshikilia mwanaharakati kwa kumkosoa mke wa raisi Museven

media


Janet Museven Waziri wa Elimu wa Uganda na mke wa raisi Yoweri Museven
Uganda inamshikilia mwanaharakati na muhadhiri wa chuo kikuu cha Makerere kwa kumkosoa mke wa raisi wa Uganda kupitia mtandao wa kijamii.
Stella Nyanzi alimkosoa Bi Janet Museveni, ambaye ni waziri wa elimu kupitia ukurasa wake wa face book baada ya serikali kusema inaandaa mpango wa kugawa taulo za kike kwa wasichana wanafunzi ambao wapo katika mazingira magumu ya kupata vifaa hivyo.
Msemaji wa polisi Emilian Kayima amethibitisha kukamatwa kwa Stela Nyanzi ambaye atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu jijini kampala kwa matumizi mabaya ya mtandao na kuvunja sheria ya mawasiliano ya mwaka 2011.
Kwa mujibu wa Kayima Bi Stella Nyanzi amekuwa akichapisha masuala yanayotazamwa kama vita kupitia mtandao wa kijamii ambayo hayana maslahi kwa taifa.

Miripuko ya mabomu yauwa zaidi ya watu 30 nchini Misri

Mabomu yameripuka katika makanisa mawili kwenye miji tafauti nchini Misri na kuuwa takriban watu 38 na kujeruhi wengine takriban 100 katika mashambulio yanayodaiwa kufanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu.
Mabomu yameripuka katika makanisa mawili kwenye miji tafauti wakati waumini wakiadhimisha Jumapili ya Mnazi nchini Misri na kuuwa takriban watu 38 na kujeruhi wengine takriban 100 katika mashambulio yanayodaiwa kufanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu.
Katika shambulio la kwanza Jumapili (09.04.2017) bomu liliripuka katika mji wa mwambao wa Alexadria ambao ni makao ya kihistoria ya Wakristo nchini Misri na kuuwa watu 11 na kujeruhi wengine 35 muda mfupi tu baada ya Papa Tawadros wa Pili kumaliza misa.Wasaidizi wake baadae wamekiambia chombo cha habari cha eneo hilo kwamba kiongozi huyo wa kidini amenusurika bila ya kujeruhiwa.
Kundi la Dola la Kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo kupitia shirika lake la habari la Aamaq baada ya kuonya hivi karibuni kwamba itazidisha mashambulizi yake dhidi ya Wakristo wa Misri.
Miripuko hiyo inakuja mwanzoni mwa Wiki Takatifu kuelekea Pasaka na ikiwa ni wiki chache tu kabla ya Papa Francis kuanza ziara yake katika nchi hiyo yenye idadi kubwa kabisa ya watu katika ulimwengu wa nchi za Kiarabu.
Kituo cha televisheni cha CBC kimeonyesha mkanda kutoka ndani ya kanisa huko Tanta ambapo idadi kubwa ya watu walikuwa wamezunguka kile kinachoonekana kuwa ni miili ya watu waliokufa ikiwa imefunikwa makaratasi.Naibu waziri wa afya wa mkoa Mohammed Sharshar amethibitisha maafa hayo.
Papa Francis alaani mshambulizi
Papa Francis amelaani mashambulio hayo ya mabomu na kutuma rambi rambi nzito kwa nduguye Papa Tawardos wa Pili, Kanisa la Koptik na watu wote katika taifa hilo la Misri.Habari za mshambulizi hayo zimekuja wakati Papa Francis mwenyewe alipokuwa akiadhimisha Jumapili hiyo ya Mnazi katika uwanja wa kanisa la Peter huko Vatikani.
Sheikh Mkuu Ahmed el Tayeb ambaye ni mkuu wa Al-Azhar kituo kikuu cha elimu kwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni pia amelani mashambulio hayo kwa kuyaita kuwa "miripuko ya kigaidi ambayo imewalenga wau wasiokuwa na hatia."Israel na kundi la Hamas linalotawala Gaza pia wamelani mashambulio hayo.
Mashambulizi hayo yameongeza hofu kwamba Waislamu wa itikadi kali ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana na vikosi vya usalama katika rasi ya Sinai sasa wanaelekeza mashambulizi yao kwa raia.
Kundi la Dola Kiislamu laonya
Kundi lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu limedai kuhusika na shambulio la kujitowa muhanga katika kanisa la Cairo hapo mwezi wa Disemba ambalo limeuwa watu 30 wengi wao wakiwa ni wanawake pamoja na kufanya mfululizo wa mauaji katika eneo tete la Sinai na kusababisha mamia ya Wakristo kukimbilia maeneo yalio na usalama zaidi nchini humo.
Hivi karibuni kundi hilo limetowa mkanda wa video likiapa kuzidisha mashambulizi dhidi ya Wakristo ambao imewaita "makafiri" wenye kuyawezesha mataifa ya magharibi dhidi ya Waislamu.
Wakristo wa Kikoptik kwa kiasi kikubwa wameunga mkono kupinduliwa na jeshi kwa Rais Mohammed Mursi Muislamu wa itikadi kali na wameshukiwa na ghadhabu za Waislamu wengi wa itikadi kali ambao wameshambulia makanisa na taasisi nyengine za Wakristo baada ya kupinduliwa kwake.

Muzbekistan mtuhumiwa mkuu wa shambulio liliouwa wanne Sweden.

Mwanaume wa miaka 39 raia wa Uzbekistan mbaroni kwa tuhuma za kuiteka nyara lori na kulibamiza kwa umati mkubwa wa watu Stockholm na kuuwa watu wanne kujeruhi wengine 15 katika shambulio la kigaidi.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 39 raia wa Uzbekistan alioko kizuizini ni dereva anayetuhumiwa kuliteka nyara la kusambaza bia ambalo liliuvamia umati mkubwa wa watu katikati ya mji mkuu wa Stockholm na kuuwa watu wanne na kujeruhi wengine 15 katika kile kinachoonekana dhahir kuwa ni shambulio la kigaidi.
Mwanaume huyo ambaye alikuwa akijulikana kabla na mashirika ya ujasusi ya Sweden ambaye ni mtu aliyejitenga asiekuwa na uhusiano unaofahamika na makundi ya Kislamu ya itikadi kali anatuhumiwa kuwaponda wapita njia katika mtaa wenye harakati kubwa za manunuzi na kulibamiza gari hilo hadi ndani ya duka moja hapo Ijumaa (07.04.2017).
Dan Elliason mkuu wa jeshi la polisi nchini Sweden ameuambia mkutano wa wandishi wa habari hapo Jummamosi kwamba hakuna kinachoashiria kwamba mtu huyo waliemkamata sie aliehusika na shambulio hilo na kwamba kinyume chake tuhuma zimezidi kuimarika wakati uchunguzi ukiendelea.
Mtu huyo aliekamatwa Ijumaa usiku kwa madai ya kuhusika na ugaidi baada ya kutokea shambulio katikati ya mji mkuu wa Stockhlom inaonekana alichukuwa hatua hiyo peke yake lakini mkuu huyo wa polisi amesema "bado hawafuti uwezekano watu wengine zaidi wakawa wanahusika."
Hakuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi
Schweden - Stockholm nach dem Anschlag - Prinzessin Victoria (picture alliance/Lehtikuva/dpa/A. Aimo-Koivisto) Mwana mrithi wa ufalme Victoria nchini Sweden akiwasili na mwana mfalme Daniel katika eneo la maombolezo karibu na shambulio lilipotokea
Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa TT mtuhumiwa huyo kutoka Jamhuri ya Uzbekistan ilioko Asia ya kati atawakilishwa na wakili atakayeteuliwa na mahakama Johan Eriksson.Polisi hauikutaja jina la mtuhumiwa huyo na kwamba inaonekansa alikuwa pembezoni mwa repoti za ujasusi.Mkuu wa polisi wa usalama wa Sapo Anders Thornberg amesema wamepokea taarifa za ujasusi mwaka jana lakini hawakuona uhusiano wowote na makundi ya itikadi kali.
Mkuu wa jeshi la polisi Eliasson amesema shambulio hilo linafanana kabisa na lile lililokea London mwezi uliopita ambapo kwayo watu sita wameuwawa akiwemo mshambuliaji mwenyewe ambaye aliendesha gari lililokuwa limekodiwa na kuwagonga wapita njia waliokuwepo katika daraja nje ya bunge la Uingereza.
Magari pia yametumiwa kama silaha katika mji wa Nice nchini Ufaransa na Berlin nchini Ujerumani mwaka uliopita katika mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na kundi linalojiita kundi la Dola la Kiislamu.
Hakukuwa na taarifa iliyotolewa mara moja kudai kuhusika na shambulio hilo nchini Sweden ambayo hadi hisi sasa ilikuwa hauikuguswa na mashambulio makubwa ya kigaidi na ambapo wengi walikuwa wakijivunia kuwa ni taifa la kidemokrasia lililo na uwazi.
Kifaa chafanana na bomu la kienyeji
Schweden - Stockholm nach dem Anschlag - Dan Eliasson (Getty Images/AFP/TT/A. Wiklund) Mkuu wa jeshi la polisi Sweden Dan Eliasson -akizungumza na waandishi wa habari.
Polisi imesema imegunduwa kifaa chenye kutia shaka ndani ya gari hilo ambalo liliishia kujibamiza katika duka la Ahlens lakini imesema hawajui iwapo kifaa hicho lilikuwa bomu la kienyeji kama ilivyoripotiwa na kituo cha matangazo cha SVT.
Maafisa wa serikali za mitaa katika mji wa Stockholm ambapo bendera zimekuwa zikipepea nusu mlingoti kwenye majengo ikiwa ni pamoja na bunge na kasri la kifalme wamesema watu 10 akiwemo mtoto mmoja bado wanaendelea kupatiwa matibabu hospitali huku watu wazima wawili wakiwa kituo cha wagonjwa mahtuti.
Sweden hapo Jumatatu mchana itabaki kimya kwa dakika moja kuomboleza wale waliopoteza maisha yao.

Wimbo Wamponza Diamond......Gwajima Aahidi Kupambana Nae

Mwanamuziki Diamond Platnumz amemuomba msamaha Askofu Gwajima kufuatia kile kilichodaiwa na askofu huyo kuwa ameimbwa kwenye wimbo wa mtu anayepotosha haki ili kutetea vyeti feki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema leo mchana  Askofu Gwajima aliandika, “Aliyeniweka kwenye wimbo wa lengo la kupotosha haki ili kusapoti vyeti feki, jiandae, Almasi itageuka maji kesho!”
Kauli hii ya Askofu Gwajima imekuja ikiwa ni saa chache tu tangu mwanamuziki Diamond Platnumz alipotoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Acha Nikae Kimya ambapo ndani ya waliotajwa ni pamoja na Askofu Gwajima. Katika wimbo huo, Diamond alisema kuwa, ugomvi kati ya Makonda na Gwajima unachcochewa na dada mmoja kwenye mitandao.

Baada ya Gwajima kutoka maneno hayo, Diamond amejitokeza na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akifafanua kile alichokiimba kuhusu Gwajima kuwa hakina lengo baya, huku akimtaka Askofu Gwajima kutomgeuza maji kesho kanisani kwake, kwani yeye akimpania mtu huwa hatoki

“Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…” aliandika Diamond na kuongeza;

“Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭 Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁"
 
Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟..... lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa... Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: "mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea....ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea..." Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza...nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana...ikapelekea hadi kufikia hapa...asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭 Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua mzee wa single touch ukimuamulia mtu....... naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁😆😅
 

Nape Atema Cheche Kwa Wapiga Kura Wake

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Mtwara kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye amtaka Rais Magufuli aunde tume huru ambayo itaweza kuchunguza matukio ya uhalifu ya uvamizi wa studio unaoendelea nchini.

Hatua hiyo inatokana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea Tanzania na kuacha maswali mengi vichwani mwa wananchi kushindwa kufahamu kuwa watu hao na vikundi hivyo vya kihuni vinavyofanya vitendo hivyo vinapata wapi mamlaka hayo kuwa na nguvu kushinda Dola.

“Ombi langu kwa Rais namuomba aunde tume huru ichunguze matendo haya yasijirudie tena kwa sababu yasipochukuliwa hatua yataharibu sura ya Tanzania pia yataweza kuibuka makundi ya wahuni kuanza kuteka watu nao kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa. Tumsaidie Rais Magufuli kwa kumwambia ukweli naimani atasikia na atafanyia kazi kwa kuwa Rais wetu anapenda kusikiliza watu”. Alisema Nape

Aidha Mbunge huyo amesema watu wanaofanya mambo hayo wanalengo la kuwagombanisha wananchi na Rais wao jambo ambalo sio zuri kwa taifa.

 "Juzi amepotea msanii Roma Mkatoliki na wengine lakini mpaka sasa haifahamiki wapo wapi, yaani kama vile amepotea Nzi, tulisikia kijana mmoja wa CHADEMA anaitwa Ben Sanane amepotea saizi miezi mitano imepita, matendo haya ya kina Ben Sanane, Roma Mkatoliki, na wengine yanajenga chuki ya wananchi kwa Rais, lakini pia yanajenga chuki kwa wananchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ". Alisema Nape Nnauye

Vile vile Nape amesema yeye mpaka sasa haamini yule mtu aliyemtolea silaha siku ya mkutano wake na wanahabari kama alitumwa ila shida aliyokuwa nayo ni kutaka kujua vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya nini mpaka matukio yote yanatokea.

==>Haya ni Maneno ya Nape
1.usema kuwa nilifanyakazi kubwa CCM haimaanishi kuwa wengine hawakufanya. Wote tunajua tulivyokipigania chama

2..Nilipopewa Uwaziri kwa miezi 15, sina mashaka, nilifanya kazi kwa umakini mkubwa kwa kutumia uwezo wangu wote

3.Kama ambavyo siku ya kuteuliwa hatukujadiliana, miezi 15 ilipopita aliyeniteua aliamua kufanya mabadiliko ya baraza.

4.Kama ikibainika kuwa alivamia kituo cha Clouds, alafu nisipochukua hatua, sitakuwa na sababu ya kuendelea kuwa waziri.

5.Nilipogundua ni kweli alivamia Clouds, niliamua kuchukua hatua na kusimamia maneno yangu nisionekane mpumbavu ni mimi.

6.potishiwa kwa bastola, nilimwambia yule mtu taratibu, unaharibu sababu tukio lile lilikuwa likirushwa mubashara.

7. yule aliyenitisha walisema si Polisi, mara hajulikani.Lakini mtu mwingine akinyanyua bastola hapa, Polisi hawatakuacha.

8..RPC alikuwa pale, kama hakuwa Polisi kwanini wasimkamate? Na mtu yule si kweli kwamba hajulikani, anajulikana.

9. Mazingira ya kupotea kwa Ben Saanane yanautata mkubwa sana. Watu wengi sana wanatishiwa sasa. Juzi studio wametekwa wanne.

10.Matukio yanayoendelea sasa nchini yanawafanya watu kuwa na hofu. Hawaamini kama wakitoka watarudi majumbani mwao salama.

11. Namuomba Rais wangu aunde tume huru ya kuchunguza matendo haya ili impelekee taarifa kamili aweze kuchukua hatua.

12.Tusipochukua hatua, yatajitokeza makundi ya wahuni nao watapitia mlango huo huo kwa sababu hakuna hatua zinazochukuliwa.

13.Matendo haya yasipokomeshwa haraka, CCM tutapata tabu sana kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.

Breaking News: Msani Roma Mkatoliki na wenzake waliotekwa wapatikana Wakiwa Salama

Muda mfupi  baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kuwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kusema ni lini mwanamuziki  Roma na wenzake watapatikana, taarifa kutoka kwa mmiliki wa studio walipokamatiwa, amethibitisha kuwa wamepatikana.

J Murder ambaye ndiye mmiliki wa Tongwe Records walipokuwa Roma na wenzake kabla ya kukamatwa na watu wasiojulikana, amesema kuwa wasanii hao wamepatikana na wapo katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aidha,Mkuu wa polisi (OCD) wilaya ya Kinondoni, Abubakar Kunga amethibitisha kupatikana kwa wasanii hao, lakini kwa sasa amesema wanafanya nao mahojiano ya kipolisi katika kituo cha Oysterbay.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.
“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye.

“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu."
Alisema kamanda Sirro mapema Asubuhi wakati akiongea na waandishi wa habari