Image copyrightAPImage caption Ndege ya kivita Marekani
Jeshi la Marekani limesema kuwa limetekeleza shambulizi kwa kutumia ndege isiokuwa na rubani nchini Somalia, ikilenga gari moja lilokuwa limewabeba wanachama watatu wa kundi la kigaidi la al-Shabab.
Kulingana na msemaji wa pentagon, aliyelengwa hasa ni Hassan Ali Dhoore ambaye anatuhumiwa kuandaa mashambulizi ya hivi karibuni ya mabomu katika uwanja wa ndege wa Mogadishu na katika hoteli moja ambapo raia wa Marekani waliuwawa.
Shambulio hilo la majeshi ya Marekani limetekelezwa katika eneo la kaskazini mwa mji wa Jilib, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia, huku Marekani ikisema ingali inatathmini matokeo ya shambulio hilo.
Image copyrightAFPImage caption Wapiganaji wa al-Shabab Shambulizi hilo la hivi karibuni la Marekani linajiri wiki chache baada ya shambulizi jingine katika kambi ya mazoezi ya al-Shabab kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani na nyingine iliokuwa na rubani.
Image caption Mechi kati ya Collingwood na Richmond
Shirikisho la soka nchini Australia limeshtumu mashabiki walioweka kitambara chenye maandishi dhidi ya msikiti katika mechi moja huko mjini Melbourne siku ya Ijumaa.
Maandishi hayo yalioonekana katika mechi kati ya Collingwood na Richmond pia yalishirikisha nembo ya kundi la mrengo wa kulia la United Patritic Front.
Hatahivyo kitambara hicho chenye maandishi kiliondolewa na mashabiki waliokiweka pia wakaondolewa uwanjani.
Shirikisho la soka nchini humo mara kwa mara limekabiliwa na maswala ya ubaguzi kufuatia kuzomwa kwa mchezaji mmoja wa Aborigine.
Mkuu wa shirikisho hilo Gillon McLachlan amesema kuwa maandishi hayo yalikuwa na ubaguzi,yaliwapuuza wengine na kuwakosea heshima.
Idadi ya waislamu nchini Australia ni asilimia 2.
Mnamo mwezi Novemba ,utafiti ulionyesha kwamba waislamu wa Australia wanakabiliwa mara tatu na ubaguzi unaokabili makabila mengine.
Image copyrightAPImage caption Salah Abdeslam akikamatwa na maafisa wa polisi wa Ubelgiji
Mshukiwa wa shambulio la Paris aliyenusurika Salah Abdeslam alikataa kujilipua ili kuokoa maisha ,nduguye amesema.
Mohammed Abdeslam alikuwa akizungumza na runinga ya BFMTV nchini Ufaransa baada ya kukutana na Salah katika seli yake ya Ubelgiji ambapo anangojea kusafirishwa hadi Ufaransa.
Kungekuwa na waathiriwa zaidi iwapo ningefanya hivyo,Salah alimwambia nduguye.
Shambulio la ufyatuaji risasi pamoja na lile la bomu katika ukumbi mmoja wa tamasha,uwanjani,mgahawani na baa moja mnamo tarehe 13 mwezi Novemba liliwauwa watu 130 mnamo mwaka 2015.
Abdeslam mwenye umri wa miaka 26 alikamatwa mwezi uliopita mjini Brussels siku nne kabla ya shambulio la bomu mjini Brussels lililowaua watu 32. Image copyrightBelgianFrench police Image caption Abdeslam Maafisa wa polisi wanaamini kwamba mtandao huohuo wa wanamgambo ndio uliohusika na mashambulio hayo ya miji hiyo miwili.
Raia huyo wa Ufaransa aliyezaliwa mjini Ubelgiji alikuwa mafichoni katika mji huo mkuu wa Ubelgiji kwa zaidi ya miezi minne.
Baada ya kukamatwa Abdeslam alihojiwa kuhusu jukumu lake katika mashambulio hayo ya Paris.
Mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump, hana ufahamu wowote wa sera za kigeni wala maswala ya ulimwengu!
Haya ni kulingana na rais wa Marekani Barrack Obama.
Obama ameyasema haya kufuatia matamshi ya Donald Trump kuwa wanajeshi wa Marekani wanafaa kuondoka Japan na Korea Kusini, na mataifa hayo yanafaa kutengeneza zana zao za kinyuklia.
Image caption Trump Mataifa hayo mawili pia hayakufurahishwa na matamshi ya bwana Trump
Image copyrightImage caption(kulia) Kiongozi wa chama cha EFF Julius Malema.
Kiongozi wa mrengo wa kushoto nchini Afrika Kusini Julius Malema ameonya kuwa chama chake kitamzuia Rais Jacob Zuma kuhutubia bunge kufuatia uamuzi ulitolewa na mahakama ya juu zaidi nchini humo kuwa alikiuka katiba kwa kukataa kuilipa serikali pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafsi.
Amesema kuwa chama chake cha Economic Freedom Fighters kitashinikiza kuondolewa kwa Rais Zuma na kuvunjwa kwa bunge ili kufanyika uchaguzi wa mapema.
Image copyrightGettyImage captionMakao ya Zuma yaliyofanyiwa ukarabati.
"Kati ya sasa na wakati wa kumuondoa madarakani, Rais hatuzungumza bungeni. Tutamzuia.Tutamsukuma." Malema alismema.
Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.
Mahakama ilisema kwa wizara ya fedha itatambua ni kiasi gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma atalipa yenye mwenyewe.
Image copyrightStatehouse TanzaniaImage captionMshtakiwa alikuwa kwenye baa ya Soweto eneo la Makumbusho
Kondakta wa daladala amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli.
Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji, alidaiwa kutenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto, maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Wakili wa serikali Keneth Sekwao aliambia mahakama Alhamisi kuwa mshtakiwa, akiwa katika baa hiyo, alitishia kumuua Dkt Magufuli kwa maneno kwa njia ya kujitoa mhanga.
“Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli, mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alinukuliwa na Wakili Sekwao.
Mshtakiwa alikana shtaka hilo.
Hakimu Mkazi, Hellen Liwa aliweka wazi dhamana ya mshtakiwa huyo na kumtaka kutafuta wadhamini wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.
Alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na akawekwa rumande hadi 14 Aprili kesi ikatapotajwa tena.
Image copyrightGettyImage captionMkutano wa dunia kuhusu Nuklia
Korea kaskazini imekuwa gumzo wakati wa mkutano wa dunia juu ya usalama wa nyuklia unaofanyika mjini Washngton.
Baada ya kukutana na Rais Xi Jinping wa China, Rais Barack Obama amesema wote wanawajibu wa kulifanya eneo hilo la rasi ya Korea kuwa eneo huru lisilo na nyuklia na kuiweka vikwazo zaidi dhidi ya Pyongyang.
Hali ya wasiwasi imetanda juu ya jaribio la Korea kaskazini kuendelea silaha za nyuklia na majaribio yake ya teknolojia ya makombora.
Awali Rais Obama alikutana na viongozi wa Japan na Korea kusini kuweka msimamo wa pamoja juu ya suala la usalama katika rasi hiyo ya Korea.
Pamoja na kwamba nchi ya pili kwa nuklia duniani Urusi haijahudhuria mkutano huo, Rais Obama alifanya mazungumzo na Rais Xi Jinping of China ambapo amesema yeye pamoja na Rais XI wamekubaliana kuondoa nuklia katika eneo la rasi ya Korea na kutekeleza vikwazo vipya vilivyopitishwa na Umoja wa Matiafa kwa lengo la kuipa shinikizo jipya Korea Kaskazini.
Kwa upande wake Rais Xi amesema China inataka kuongeza mawasiliano na kuratibu jambo hilo ambapo nchi zote mbili zimekubaliana kukutana kila mwaka kuzungumzia masuala ya usalama wa nyuklia.
Wamesema pia watafanya kazi kwa pamoja kuzuia malighafi za kutengeneza nuklia na kuratibu juhudi za kuzuia malighafi hizo kuangukia mikononi mwa magaidi.
Hata hivyo kasoro moja katika mkutano huo ni kutokuwepo kwa Rais Vladimir Putin. Urusi na Marekani wanamiliki karibu asilimia 90 ya silaha za nyuklia hivyo Mosco kukataa kuhudhuria mkutano huo unaweza kufanya makubaliano yatakayofikia isiyatekeleze.