Friday, April 28, 2017

Rais Magufuli kupokea taarifa vyeti feki LEO


RAIS John Magufuli leo anatarajiwa kupokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika Ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais katika Ikulu Ndogo ya Chamwino Dodoma, Jaffar Haniu ilisema taarifa hiyo itawasilishwa kwa Rais Magufuli na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki.

Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma liliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba, 2016. 
Hivi karibuni wakati akifungua rasmi nyumba mpya za makazi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Rais Magufuli alisema anasubiri ripoti kuhusu watumishi wa umma wenye vyeti feki wapatao 9000.

“…Kwa hiyo mnaweza mkaona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa ni zaidi ya 56,000, kila mahali unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima niyatatue matatizo kwa sababu mlinichagua kwa ajili hiyo,” alisisitiza Rais katika hotuba yake hiyo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Sunday, April 9, 2017

Uganda yamshikilia mwanaharakati kwa kumkosoa mke wa raisi Museven


media


Janet Museven Waziri wa Elimu wa Uganda na mke wa raisi Yoweri Museven
Uganda inamshikilia mwanaharakati na muhadhiri wa chuo kikuu cha Makerere kwa kumkosoa mke wa raisi wa Uganda kupitia mtandao wa kijamii.
Stella Nyanzi alimkosoa Bi Janet Museveni, ambaye ni waziri wa elimu kupitia ukurasa wake wa face book baada ya serikali kusema inaandaa mpango wa kugawa taulo za kike kwa wasichana wanafunzi ambao wapo katika mazingira magumu ya kupata vifaa hivyo.
Msemaji wa polisi Emilian Kayima amethibitisha kukamatwa kwa Stela Nyanzi ambaye atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu jijini kampala kwa matumizi mabaya ya mtandao na kuvunja sheria ya mawasiliano ya mwaka 2011.
Kwa mujibu wa Kayima Bi Stella Nyanzi amekuwa akichapisha masuala yanayotazamwa kama vita kupitia mtandao wa kijamii ambayo hayana maslahi kwa taifa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Miripuko ya mabomu yauwa zaidi ya watu 30 nchini Misri


Mabomu yameripuka katika makanisa mawili kwenye miji tafauti nchini Misri na kuuwa takriban watu 38 na kujeruhi wengine takriban 100 katika mashambulio yanayodaiwa kufanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu.
Mabomu yameripuka katika makanisa mawili kwenye miji tafauti wakati waumini wakiadhimisha Jumapili ya Mnazi nchini Misri na kuuwa takriban watu 38 na kujeruhi wengine takriban 100 katika mashambulio yanayodaiwa kufanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu.
Katika shambulio la kwanza Jumapili (09.04.2017) bomu liliripuka katika mji wa mwambao wa Alexadria ambao ni makao ya kihistoria ya Wakristo nchini Misri na kuuwa watu 11 na kujeruhi wengine 35 muda mfupi tu baada ya Papa Tawadros wa Pili kumaliza misa.Wasaidizi wake baadae wamekiambia chombo cha habari cha eneo hilo kwamba kiongozi huyo wa kidini amenusurika bila ya kujeruhiwa.
Kundi la Dola la Kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo kupitia shirika lake la habari la Aamaq baada ya kuonya hivi karibuni kwamba itazidisha mashambulizi yake dhidi ya Wakristo wa Misri.
Miripuko hiyo inakuja mwanzoni mwa Wiki Takatifu kuelekea Pasaka na ikiwa ni wiki chache tu kabla ya Papa Francis kuanza ziara yake katika nchi hiyo yenye idadi kubwa kabisa ya watu katika ulimwengu wa nchi za Kiarabu.
Kituo cha televisheni cha CBC kimeonyesha mkanda kutoka ndani ya kanisa huko Tanta ambapo idadi kubwa ya watu walikuwa wamezunguka kile kinachoonekana kuwa ni miili ya watu waliokufa ikiwa imefunikwa makaratasi.Naibu waziri wa afya wa mkoa Mohammed Sharshar amethibitisha maafa hayo.
Papa Francis alaani mshambulizi
Papa Francis amelaani mashambulio hayo ya mabomu na kutuma rambi rambi nzito kwa nduguye Papa Tawardos wa Pili, Kanisa la Koptik na watu wote katika taifa hilo la Misri.Habari za mshambulizi hayo zimekuja wakati Papa Francis mwenyewe alipokuwa akiadhimisha Jumapili hiyo ya Mnazi katika uwanja wa kanisa la Peter huko Vatikani.
Sheikh Mkuu Ahmed el Tayeb ambaye ni mkuu wa Al-Azhar kituo kikuu cha elimu kwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni pia amelani mashambulio hayo kwa kuyaita kuwa "miripuko ya kigaidi ambayo imewalenga wau wasiokuwa na hatia."Israel na kundi la Hamas linalotawala Gaza pia wamelani mashambulio hayo.
Mashambulizi hayo yameongeza hofu kwamba Waislamu wa itikadi kali ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana na vikosi vya usalama katika rasi ya Sinai sasa wanaelekeza mashambulizi yao kwa raia.
Kundi la Dola Kiislamu laonya
Kundi lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu limedai kuhusika na shambulio la kujitowa muhanga katika kanisa la Cairo hapo mwezi wa Disemba ambalo limeuwa watu 30 wengi wao wakiwa ni wanawake pamoja na kufanya mfululizo wa mauaji katika eneo tete la Sinai na kusababisha mamia ya Wakristo kukimbilia maeneo yalio na usalama zaidi nchini humo.
Hivi karibuni kundi hilo limetowa mkanda wa video likiapa kuzidisha mashambulizi dhidi ya Wakristo ambao imewaita "makafiri" wenye kuyawezesha mataifa ya magharibi dhidi ya Waislamu.
Wakristo wa Kikoptik kwa kiasi kikubwa wameunga mkono kupinduliwa na jeshi kwa Rais Mohammed Mursi Muislamu wa itikadi kali na wameshukiwa na ghadhabu za Waislamu wengi wa itikadi kali ambao wameshambulia makanisa na taasisi nyengine za Wakristo baada ya kupinduliwa kwake.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Muzbekistan mtuhumiwa mkuu wa shambulio liliouwa wanne Sweden.


Mwanaume wa miaka 39 raia wa Uzbekistan mbaroni kwa tuhuma za kuiteka nyara lori na kulibamiza kwa umati mkubwa wa watu Stockholm na kuuwa watu wanne kujeruhi wengine 15 katika shambulio la kigaidi.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 39 raia wa Uzbekistan alioko kizuizini ni dereva anayetuhumiwa kuliteka nyara la kusambaza bia ambalo liliuvamia umati mkubwa wa watu katikati ya mji mkuu wa Stockholm na kuuwa watu wanne na kujeruhi wengine 15 katika kile kinachoonekana dhahir kuwa ni shambulio la kigaidi.
Mwanaume huyo ambaye alikuwa akijulikana kabla na mashirika ya ujasusi ya Sweden ambaye ni mtu aliyejitenga asiekuwa na uhusiano unaofahamika na makundi ya Kislamu ya itikadi kali anatuhumiwa kuwaponda wapita njia katika mtaa wenye harakati kubwa za manunuzi na kulibamiza gari hilo hadi ndani ya duka moja hapo Ijumaa (07.04.2017).
Dan Elliason mkuu wa jeshi la polisi nchini Sweden ameuambia mkutano wa wandishi wa habari hapo Jummamosi kwamba hakuna kinachoashiria kwamba mtu huyo waliemkamata sie aliehusika na shambulio hilo na kwamba kinyume chake tuhuma zimezidi kuimarika wakati uchunguzi ukiendelea.
Mtu huyo aliekamatwa Ijumaa usiku kwa madai ya kuhusika na ugaidi baada ya kutokea shambulio katikati ya mji mkuu wa Stockhlom inaonekana alichukuwa hatua hiyo peke yake lakini mkuu huyo wa polisi amesema "bado hawafuti uwezekano watu wengine zaidi wakawa wanahusika."
Hakuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi
Schweden - Stockholm nach dem Anschlag - Prinzessin Victoria (picture alliance/Lehtikuva/dpa/A. Aimo-Koivisto) Mwana mrithi wa ufalme Victoria nchini Sweden akiwasili na mwana mfalme Daniel katika eneo la maombolezo karibu na shambulio lilipotokea
Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa TT mtuhumiwa huyo kutoka Jamhuri ya Uzbekistan ilioko Asia ya kati atawakilishwa na wakili atakayeteuliwa na mahakama Johan Eriksson.Polisi hauikutaja jina la mtuhumiwa huyo na kwamba inaonekansa alikuwa pembezoni mwa repoti za ujasusi.Mkuu wa polisi wa usalama wa Sapo Anders Thornberg amesema wamepokea taarifa za ujasusi mwaka jana lakini hawakuona uhusiano wowote na makundi ya itikadi kali.
Mkuu wa jeshi la polisi Eliasson amesema shambulio hilo linafanana kabisa na lile lililokea London mwezi uliopita ambapo kwayo watu sita wameuwawa akiwemo mshambuliaji mwenyewe ambaye aliendesha gari lililokuwa limekodiwa na kuwagonga wapita njia waliokuwepo katika daraja nje ya bunge la Uingereza.
Magari pia yametumiwa kama silaha katika mji wa Nice nchini Ufaransa na Berlin nchini Ujerumani mwaka uliopita katika mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na kundi linalojiita kundi la Dola la Kiislamu.
Hakukuwa na taarifa iliyotolewa mara moja kudai kuhusika na shambulio hilo nchini Sweden ambayo hadi hisi sasa ilikuwa hauikuguswa na mashambulio makubwa ya kigaidi na ambapo wengi walikuwa wakijivunia kuwa ni taifa la kidemokrasia lililo na uwazi.
Kifaa chafanana na bomu la kienyeji
Schweden - Stockholm nach dem Anschlag - Dan Eliasson (Getty Images/AFP/TT/A. Wiklund) Mkuu wa jeshi la polisi Sweden Dan Eliasson -akizungumza na waandishi wa habari.
Polisi imesema imegunduwa kifaa chenye kutia shaka ndani ya gari hilo ambalo liliishia kujibamiza katika duka la Ahlens lakini imesema hawajui iwapo kifaa hicho lilikuwa bomu la kienyeji kama ilivyoripotiwa na kituo cha matangazo cha SVT.
Maafisa wa serikali za mitaa katika mji wa Stockholm ambapo bendera zimekuwa zikipepea nusu mlingoti kwenye majengo ikiwa ni pamoja na bunge na kasri la kifalme wamesema watu 10 akiwemo mtoto mmoja bado wanaendelea kupatiwa matibabu hospitali huku watu wazima wawili wakiwa kituo cha wagonjwa mahtuti.
Sweden hapo Jumatatu mchana itabaki kimya kwa dakika moja kuomboleza wale waliopoteza maisha yao.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Wimbo Wamponza Diamond......Gwajima Aahidi Kupambana Nae


Mwanamuziki Diamond Platnumz amemuomba msamaha Askofu Gwajima kufuatia kile kilichodaiwa na askofu huyo kuwa ameimbwa kwenye wimbo wa mtu anayepotosha haki ili kutetea vyeti feki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema leo mchana  Askofu Gwajima aliandika, “Aliyeniweka kwenye wimbo wa lengo la kupotosha haki ili kusapoti vyeti feki, jiandae, Almasi itageuka maji kesho!”
Kauli hii ya Askofu Gwajima imekuja ikiwa ni saa chache tu tangu mwanamuziki Diamond Platnumz alipotoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Acha Nikae Kimya ambapo ndani ya waliotajwa ni pamoja na Askofu Gwajima. Katika wimbo huo, Diamond alisema kuwa, ugomvi kati ya Makonda na Gwajima unachcochewa na dada mmoja kwenye mitandao.

Baada ya Gwajima kutoka maneno hayo, Diamond amejitokeza na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akifafanua kile alichokiimba kuhusu Gwajima kuwa hakina lengo baya, huku akimtaka Askofu Gwajima kutomgeuza maji kesho kanisani kwake, kwani yeye akimpania mtu huwa hatoki

“Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…” aliandika Diamond na kuongeza;

“Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭 Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁"
 
Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟..... lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa... Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: "mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea....ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea..." Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza...nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana...ikapelekea hadi kufikia hapa...asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭 Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua mzee wa single touch ukimuamulia mtu....... naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁😆😅
 
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Nape Atema Cheche Kwa Wapiga Kura Wake


Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Mtwara kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye amtaka Rais Magufuli aunde tume huru ambayo itaweza kuchunguza matukio ya uhalifu ya uvamizi wa studio unaoendelea nchini.

Hatua hiyo inatokana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea Tanzania na kuacha maswali mengi vichwani mwa wananchi kushindwa kufahamu kuwa watu hao na vikundi hivyo vya kihuni vinavyofanya vitendo hivyo vinapata wapi mamlaka hayo kuwa na nguvu kushinda Dola.

“Ombi langu kwa Rais namuomba aunde tume huru ichunguze matendo haya yasijirudie tena kwa sababu yasipochukuliwa hatua yataharibu sura ya Tanzania pia yataweza kuibuka makundi ya wahuni kuanza kuteka watu nao kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa. Tumsaidie Rais Magufuli kwa kumwambia ukweli naimani atasikia na atafanyia kazi kwa kuwa Rais wetu anapenda kusikiliza watu”. Alisema Nape

Aidha Mbunge huyo amesema watu wanaofanya mambo hayo wanalengo la kuwagombanisha wananchi na Rais wao jambo ambalo sio zuri kwa taifa.

 "Juzi amepotea msanii Roma Mkatoliki na wengine lakini mpaka sasa haifahamiki wapo wapi, yaani kama vile amepotea Nzi, tulisikia kijana mmoja wa CHADEMA anaitwa Ben Sanane amepotea saizi miezi mitano imepita, matendo haya ya kina Ben Sanane, Roma Mkatoliki, na wengine yanajenga chuki ya wananchi kwa Rais, lakini pia yanajenga chuki kwa wananchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ". Alisema Nape Nnauye

Vile vile Nape amesema yeye mpaka sasa haamini yule mtu aliyemtolea silaha siku ya mkutano wake na wanahabari kama alitumwa ila shida aliyokuwa nayo ni kutaka kujua vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya nini mpaka matukio yote yanatokea.

==>Haya ni Maneno ya Nape
1.usema kuwa nilifanyakazi kubwa CCM haimaanishi kuwa wengine hawakufanya. Wote tunajua tulivyokipigania chama

2..Nilipopewa Uwaziri kwa miezi 15, sina mashaka, nilifanya kazi kwa umakini mkubwa kwa kutumia uwezo wangu wote

3.Kama ambavyo siku ya kuteuliwa hatukujadiliana, miezi 15 ilipopita aliyeniteua aliamua kufanya mabadiliko ya baraza.

4.Kama ikibainika kuwa alivamia kituo cha Clouds, alafu nisipochukua hatua, sitakuwa na sababu ya kuendelea kuwa waziri.

5.Nilipogundua ni kweli alivamia Clouds, niliamua kuchukua hatua na kusimamia maneno yangu nisionekane mpumbavu ni mimi.

6.potishiwa kwa bastola, nilimwambia yule mtu taratibu, unaharibu sababu tukio lile lilikuwa likirushwa mubashara.

7. yule aliyenitisha walisema si Polisi, mara hajulikani.Lakini mtu mwingine akinyanyua bastola hapa, Polisi hawatakuacha.

8..RPC alikuwa pale, kama hakuwa Polisi kwanini wasimkamate? Na mtu yule si kweli kwamba hajulikani, anajulikana.

9. Mazingira ya kupotea kwa Ben Saanane yanautata mkubwa sana. Watu wengi sana wanatishiwa sasa. Juzi studio wametekwa wanne.

10.Matukio yanayoendelea sasa nchini yanawafanya watu kuwa na hofu. Hawaamini kama wakitoka watarudi majumbani mwao salama.

11. Namuomba Rais wangu aunde tume huru ya kuchunguza matendo haya ili impelekee taarifa kamili aweze kuchukua hatua.

12.Tusipochukua hatua, yatajitokeza makundi ya wahuni nao watapitia mlango huo huo kwa sababu hakuna hatua zinazochukuliwa.

13.Matendo haya yasipokomeshwa haraka, CCM tutapata tabu sana kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Breaking News: Msani Roma Mkatoliki na wenzake waliotekwa wapatikana Wakiwa Salama


Muda mfupi  baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kuwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kusema ni lini mwanamuziki  Roma na wenzake watapatikana, taarifa kutoka kwa mmiliki wa studio walipokamatiwa, amethibitisha kuwa wamepatikana.

J Murder ambaye ndiye mmiliki wa Tongwe Records walipokuwa Roma na wenzake kabla ya kukamatwa na watu wasiojulikana, amesema kuwa wasanii hao wamepatikana na wapo katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aidha,Mkuu wa polisi (OCD) wilaya ya Kinondoni, Abubakar Kunga amethibitisha kupatikana kwa wasanii hao, lakini kwa sasa amesema wanafanya nao mahojiano ya kipolisi katika kituo cha Oysterbay.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.
“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye.

“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu."
Alisema kamanda Sirro mapema Asubuhi wakati akiongea na waandishi wa habari
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Monday, April 3, 2017

Maoni: Siyo mwisho wa enzi kwa Merkel


Matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Mecklenburg-Vorpommern yalikuwa pigo la kufedhehesha, lakini kwa uhakika siyo mwisho wa ukansela wa Angela Merkel, au mwanzo wa kubadili mwelekeo wa kisiasa, anasema Charlotte Potts.
Mwisho wa Ukansela," Ni makofi mangapi amebakiza Merkel," "Pigo kwa Merekl," hivyo ndivyo baadhi ya vichwa vya habari vilivyopamba magazeti ya leo nchini Ujerumani. Kwa miezi kadhaa kuwekuwepo na matukio kama hayo ambayo yameeashiria kuhitimisha ukansela wa Merkel: baada ya kauli yake iliyozuwa utata ya Tunamudu mwaka mmoja uliyopita na kuchomwa kwa makaazi ya wakimbizi, baada ya matukio ya kesha wa mwaka mpya mjini Cologne, ambamo wakimbizi walidaiwa kuwashambulia wanawake kingono, baada ya mashambulizi ya kigaidi katika miji ya Würzburg na Ansbach, ambayo yalifanywa na waomba hifadhi. Na licha ya hayo yote Merkel ameendelea kuwa Kansela. Na bado anaendelea kushikilia msimamo wake kuhusu wakimbizi.
Uchaguzi wa jimbo usitiwe chumvi
Bila shaka matokeo ya uchaguzi jimboni Mecklenburg-Vorpommern ni pigo la fedheha kwa chama cha CDU. Na bila shaka mafanikio ya chama cha AfD ambacho kwa sasa kinawakilishwa katika majimbo tisa kati ya 16 ya Ujerumani, uvipe changamoto vyama vikuu vya siasa vya Ujerumani. Hakukuwa na chama cha kidemokrasia cha upinzani kwa mrengo wa kulia - lakini kuibuka kwa AfD kumewka chama cha namna hiyo. Na bila shaka sera ya Merkel kuhusu wakimbizi ndiyo ya kulaumiwa - Merkel alifanya uamuzi kuhusu sera hiyo mwishoni mwa majira y akiangazi mwaka 2015.
Alikataa kuwafungia milango wakimbizi waliokuwa wamekwama nchini Hungary, na kwa njia hiyo kukitwika mzingo chama chake. Ukweli kwamba uamuzi mzito kama huo unaambatana na matatizo makubwa ni jambo linalijieleza lenyewe. Lakini pia ukweli kwmaba siyo kila mmoja ndani ya CDU ameshawishika haishangazi. Lakini siyo jambo jipya kwamba wanasiasa watafuta umaarufu wanajribu kuziba ombwe la kisiasa linalosababishwa na vyama vya siasa za mrengo wa kulia wa wastani.
Potts Charlotte Kommentarbild App Mwandishi wa DW Charlotte Potts.
Historia inaonyesha ni jimbo lisilotabirika
Lakini matokeo ya uchagui huu wa jimbo hayapaswi kutiliwa chumvu. Tunazungumzia uchaguzi wa kieneo katika jimbo ambalo mara kadhaa limekuwa likipiga kura za upinzani. Tangu mwaka 2006 chama cha itikadi kali za mrengo wa kulia cha NPD kimekuwa na uwakilishi katika bunge la jimbo hilo. Ni jimbo ambalo kwa kwa miaka kadhaa limekuwa nyumbani kwa siasa kali, ambako siasa kali za mrego wa kulia kama zilivyo za kusohoto, zimekuwa imara. Na ambamo chama cha CDU hata katika uchaguzi wa mwisho miaka mitano iliyopita - muda mrefu kabla ya mgogoro wa wakimbizi, kililishinda zaidi asilimia 20 tu.
Ingekuwa busara zaidi kuhiji na kusema kwamba chama cha CDU kimepoteza tu asilimia nne ya kura katika kipindi9 cha miaka mitano, kipindi ambacmo mambo mengi yamebadilika jimboni humo. Mecklenburg-Vorpommern ni jimbo ambalo halitoi mchango wowote kiuchumi kwa taifa. Likiwa na wapigakura milioni 1.3 ambao ni chini ya asilimia 60 yake ndiyo walishirki uchaguzi huo. Na matokeo ya uchaguzi huo yameamua kuubakiza muungano mkuu. Watu 800,000 tu hawamui hatma ya ukansela.
Tatizo si Merkel
Tatizo halisi la CDU jimboni Mecklenburg-Vorpommern haliko kwa Merkel, bali kwa mgombea wa CDU asie na umaarufu Lorenz Caffier. Kampeini ilionyesha kuwa hakuwa na jipya alilokuja nalo tofauti na AfD. Caffier alijitanabahisha kama mgombea wa usimamizi wa sheria, akitetea upigaji marufuku wa vazi la Burqa. Ni jambo linalotia wasiwasi iwapo kweli wakaazi wa Mecklenburg wanalo tatizo na vazi hilo lilalofunika mwili mzima. Ni wakimbizi 200,000 tu waliopelekewa jimboni humo wakati wa mgawanyo wa wakimbizi katika majimbo na mapaka wakimbizi wengi wamekwisha ondoka huko, hivyo msimamo wa Caffier haukuwa na msaada wowote.
Licha ya hayo CDU na Kansela Merkel wanapaswa kuangalia uchaguzi huo kama wito: siyo kwa ajili ya kubadili meuelekeo wa sera yake bali kuweka ukweli bayana: kwamba katika mwaka wa 2016 wakimbizi wachache sana wameingia Ujerumani, na kwamba wakimbizi wote walioingia awali wamesajaliwa na kupatiwa makazi. Na kwamba wanawasiana vizuri kuhakikisha matatizo yaliokuwepo yanashughulikiwa, kuikamilisha makubaliano na uturuki, kwa sababu ukweli hauko wazi kama AfD inavyojaribu kuuonyesha. Wapugakura wangependa utafutaji kidogo wa umaruf na ukweli zaidi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Upinzani DRC waitisha mgomo wa kitaifa


Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anatazamiwa kukutana na ujumbe wa upinzani kusaka njia za kuukwamua mkwamo wa kisiasa unaotishia kuyavunja makubaliano ya Disemba 31.
Hata hivyo, hakuna uhakika endapo upinzani utashiriki kwenye mazungumzo hayo yaliyoitishwa wakati upinzani nao ukipanga mgomo wa nchi nzima kumshinikiza Kabila kutekeleza kwa vitendo makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Kanisa Katoliki nchini Kongo.
Wakati huo huo, mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ametoa wito wa kupatikana kwa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akitaka umwagaji damu ukomeshwe mkoani Kasai.
"Taarifa za mapigano zinaendelea kuwasili kutoka Kasai, ambayo yanapelekea wahanga wengi zaidi na kuwakosesha watu makaazi yao," mkuu huyo wa Kanisa aliwaambia waumini wapatao 2,000 katika mji wa Carpi ulio kaskazini mwa Italia, ambao wenyewe ulikumbwa na matetemeko mawili makubwa ya ardhi mwaka 2012.
"Kila mmoja aombe ipatikane amani na kwamba nyoyo za wanaohusika na uhalifu huu zisibakie watumwa wa chuki na ghasia," alisema.
Watu wapatao 400 wamekufa ndani ya kipindi cha miezi sita ya machafuko ambayo yamesambaa kwenze majimbo ya Kasai-Central, Kasai, Kasai-West na Lomami.
Vatikanstadt - Papst Franziskus empfängt EU Vertreter (Reuters/Pool/A. Medichini) Papa Francis ataka kusitishwa kwa mauaji ya Kasanga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mkoa huu unakabiliwa na mapigano tangu vikosi vya serikali kumuuwa kiongozi wa kimila na mkuu wa kundi moja la wanamgambo, Kamwina Nsapu, katikati ya mwezi Agosti 2016. Nsapu anaripotiwa kuanzisha uasi dhidi ya serikali kuu ya Rais Joseph Kabila mjini Kinshasa.
Siku ya Alhamis (30 Machi), viongozi wa kanisa na mwakilishi wa Papa Francis nchini Kongo walivitaka vyombo vya usalama, ambavyo vinatuhumiwa kwa kuwatesa wapinzani, kujizuia kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa operesheni zao.
Mwezi uliopita, polisi iliwatuhumu waasi kwa kuwauwa maafisa 39 jimboni Kasai, na wiki iliyopita miilki ya wahandisi wawili wa Umoja wa Mataifa ilipatikana baada ya kutekwa nyara huko Kasai-Central.
Raia wawili wa kigeni walitekwa na watu wasiojuilikana tarehe 12 Machi sambamba na raia wengine wanne wa Kikongo waliokuwa wanawasindikiza.
Bensouda asema uhalifu wa kivita umetendeka DRC
Fatou Bensouda Pressekonferenz (picture-alliance/dpa) Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, anaamini kuna uhalifu dhidi ya ubinaadamu unatendeka nchini DRC.
Katika hatua nyengine, mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Fatou Bensouda, amesema kuuawa kinyama kwa timu ya wataalamu ya Umoja wa Mataifa na ghasia nyengine nchini Kongo kunaweza kuwa sawa na uhalifu unaoweza kushitakiwa na mahakama yake.
Katika taarifa yake ya Ijumaa, Bensouda alisema amesikitishwa sana ghasia kwenye jimbo la Kasai. Miili ya raia wa Marekani, Michael Sharp, Msweden Zaida Catalan, na mkalimani raia wa Kongo, Betu Tshintela, ilipatikana mapema wiki hii.
Wataalamu hao walikuwa wakichunguza tuhuma za uvunjaji wa haki za binaadamu uliofanywa na jeshi la Kongo na makundi ya wanamgambo kwenye eneo hilo.
Watu wengine watatu kwenye timu yao, bado hawajuilikani walipo, lakini Bensouda ameitaka serikali ya Kinshasa kufanya uchunguzi wa kina na "wa hakika".
Kawaida, ICC inaweza kutoa waraka wa kukamatwa kwa washukiwa, lakini ni juu ya taifa mwanachama kuwakamata na kuwafikisha mahakamani kujibu mashitaka.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Wamachinga wapoteza mitaji kufuatia bomoabomoa machinga complex


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli
Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga jijini Dar es salaam, Tanzania wamekumbwa na taharuki baada ya kufika katika eneo lao la biashara nje ya jengo la machinga complex na kukuta vibanda vyao vimebomolewa.
Zoezi hilo limefanyika usiku wa kuamkia Jumatatu na kwa hasira wafanyabiashara hao wakachoma moto barabara kwa kutumia matairi na takataka nyingine.
Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa wafanyabiashara hao wamedai kuwa walipewa siku tatu kuhakikisha wanaondoa bidhaa zao.
Hata hivyo wamedai kuwa waliandika barua ya kuomba kusitishwa kwa zoezi hilo ili wapatiwe vizimba lakini cha kushangaza ni kwamba wamevunjiwa hata bila kupata majibu ya baraua yao.
Pia wamelalamika kupotea kwa bidhaa zao ambazo baadhi yake zimeibiwa na nyingine hawajui zimepelekwa wapi.

Mfanyabiashara wa machinga Complex Yohana William amelalamika kuwa mtaji wake wote umepotea kwani alikuwa ameaminiwa na mali za watu kufanya biashara lakini vunjavunja hii imemharibia biashara yake, na amepoteza kila kitu.
“Vibanda vyetu vimebomolewa, nimebakia hivihivi kama nilivyo unavyoona nina mkopo wa watu, walikuwa wananiamini kwenye kizimba tuko kikundi pamoja sasa tunashangaa…,” mfanyabiashara huyo amesema kwa masikitiko makubwa.
“Sasa tunashangaa rais ameruhusu wafanyabiashara kama sisi wako barabarani, lakini sisi wafanyabiashara wadogo tuliovumilia miaka yote, miaka sita tuko hapa, hili jengo linaitwa machinga complex sasa tumekuja wamachinga wenyewe tunatolewa. Na pale ambapo wananambia niende sijaelekezwa,” amesema William.
Wakinamama wajasiriamali katika soko hilo walilaumu zoezi hilo la kubomoa vibanda vyao vya biashara ambavyo ndio vilikuwa vinawapatia riziki zao.
Mmoja wa wafanyabiashara hao Mariam Hassan amewauliza viongozi waliobomoa vibanda vyao wanataka wawe mahakaba na majambazi?
Mwandishi wetu ameripoti kuwa vibada vyao vinadaiwa kubomolewa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri wa nchi ofisi ya rais (TAMISEMI), George Simbachawene la kuwataka waingie ndani ya jengo badala ya kuweka vibanda nje ya jengo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

UZINDUZI WA BARABARA YA MGAGADU-KIWANI PEMBA


SA
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDIZI DK ALI MOHAMED SHEIN AKIKATA UTEPE KUZINDUA BARABARA YA MGAGADU-KIWANI MKOA WA KUSINI PEMBA ,(PICHA NA IKULU)
SA 1
Rails DK.SHEIN AKIPATA MAELEZO ALIPOTEMBELEA UJENZI WA BARABARA HIYO.
SA 2
WANANCHI WA KIWANI WAKIMSIKILIZA RAIS WAKATI ALIPOZUNGUMZA NAO BAADA YA UZINDUZI WA BARABARA YAO
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

BAJETI YAPITISHWA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI


ZA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akisoma taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara katika mwaka wa fedha 2016/17 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi, Maliasili na Utalii – Dodoma.
ZA 1
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii; Mhe. Atashasta Ndetiye akiongoza majadiliano wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilioshirikisha Kamati yake na watendaji wakuu wa Wizara na taasisi zake – Dodoma.
ZA 2
Mbunge wa Korogwe mjini, Mhe. Mary Chatanda akishiriki mjadala wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilioshirikisha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na watendaji wakuu wa Wizara na taasisi zake – Dodoma.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Haina haja ya kupeleka mechi Mwanza, maandalizi ndio kila kitu’ – Niyonzima


Kiungo wa Yanga raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo amesema, katika soka la kisasa maandalizi ndio kilakitu katika kuhakikisha timu inapata matokeo na sio kubadili uwanja.
Hivi karibuni Yanga iliwasilisha maombi shirikisho la soka Afrika CAF ili mechi yao ya nyumbani ya mchujo kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya kombe ka shirikisho barani Afrika ichezwe kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza badala ya uwanja wa taifa. Maombi hayo hayakufanikiwa baada ya uwanja wa CCM Kirumba kutokidhi viwango vya CAF na kutakiwa kufanyiwa marekebisho ambayo hayawezi kukamilika ndani ya muda kabla ya mechi hiyo.
“Ukijiandaa vizuri haijalishi uwanja, Mwanza sio mbali mashabiki wanasafiri hadi nje ya nchi sasa Mwanza watashindwaje kwenda kwa hiyo presha ambayo tunaipata hapa haitakuwa tofauti sana na ya Mwanza kwa sababu ni Tanzania ileile.”
“Kwa upande wangu haina haja kubadili uwanja kwa sababu mpira unaweza kuchezeka sehemu yoyote. Sidhani hata kama walimu walipendekeza hivyo, itakuwa ni wadau lakini mpira wa kisasa hauko hivyo, sehemu yoyote unacheza mpira inategemea na wewe ulivyojiandaa.”
Kwa maana hiyo, Yanga itacheza mechi yake dhidi ya MC Algers kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam na si vinginevyo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Coyo - Ziwafikie (Official Video) | Download Mp4














Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Anachoamini Mkude baada ya Simba kufungwa 2-1 na Kagera Sugar


Baada ya Simba kupoteza mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar kwa kuchapwa 2-1, nahodha wa Simba Jonas Mkude amesema bado wanaendelea kufukuzia ubingwa hadi mwisho kwa sababu bado ipo nafasi ya kushinda taji hilo ikiwa watafanya vizuri kwenye mechi zao zilizosalia kwenye ratiba ya ligi.
“Ndiyo matokeo ya mchezo, tumepoteza mechi lakini bado hatukati tama, tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunashinda ubingwa wa ligi,” alisema Mkude mara baada ya mchezo wakati akizungumza na Azam TV.
“Nafasi bado ipo, sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu mbili zilizobaki huku Kanda ya Ziwa. Mashabiki waendelee kutuunga mkono wasife moyo bado tupo kwenye nafasi nzuri.”
Simba ina mechi mbili dhidi ya timu za mkoa wa mwanza (Toto Afrikans na Mabao FC)ambazo zote zinapambana kukwepa mkasi wa kushuka daraja hivyo Wekundu wa Msimbazi watakutana na upinzani mkali kutoka kwa timu hizo huku Toto Africans ikiwa na historia nzuri kuifunga Simba kwenye mechi za ligi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Download Audio: Coyo – Ziwafikie









http://yingamedia.com/wp-content/uploads/2017/03/download-w-2.png










Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

‘Najituma kwenye soka nipate pesa za kumtunza mdogo wangu’ – Kabunda


Na Zainabu Rajabu
MOJA ya sababu inayomfanya kiungo wa Mwadui FC ya Shinyanga Hassan Kabunda kucheza soka kwa kujituma ni kutafuta pesa kwa ajili ya kumsaidia mdogo wake kike ambaye ni mlemavu na anamtegemea kwa sasa.
Tangu Kabunda asajiliwe na Mwadui FC ya Shinyanga akitokea timu ya Asanti United ya ligi daraja la kwanza, amekuwa na msimu mzuri katika ligi kuu na kufanikiwa kutikisa nyavu mara 6.
Shaffihdauda.co.tz. ilimtembelea Hassan Kabunda nyumbani kwao na kupiga nae stori kadhaa kuhusiana na maisha yake ya soka ambapo alisema: “Nimekuwa najituma na kupambana katika maisha yangu ili niweze kumpa maisha mazuri dada yangu kipenzi Noun Kabunda ambaye amekuwa ndiyo furaha yangu pale ninapo muona akitabasamu.”
“Ninapo muangalia dada yangu katika hali aliyonayo naumia sana lakini huwezi kumkufuru Mwenyenzi Mungua kwa livyomuumba, napambana ili niweze kumtimiza mahitaji yake nikiwa kama kaka mkubwa.”
Kinda huyo amesema, amekuwa akivutiwa na uchezaji wa Farid Mussa anaekipiga katika timu ya Tenerife ya nchini Hispania, huku akisema ni mchezaji ambaye anaweza kujilinganisha nae kutokana na kwamba wote wanacheza katika nafasi inayofana.
Mdogo wake Kabunda ana ulemavu wa viungo ambao alizaliwa nao na kaka yake (Hassan Kabunda) anapambana kwenye soka ili kupata pesa za kuweza kumtunza na kumpatia mahitaji muhimu.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Zitto Kabwe Agonga Mwamba Ubunge ELA....... Spika Ndugai Agomea Maombi Yake


Mbunge  wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo),  amegonga mwamba baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge kutoa msimamo wake kuhusu uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Hatua hiyo inatokana na Zitto kuwasilisha barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Machi 28, mwaka huu akitaka kamati hiyo kutoa ufafanuzi wa mgombe wa kundi C ili kila chama kiweze kushiriki uchaguzi, badala ya kupewa kwa vyama vilivyokuwa na idadi kubwa ya wabunge.

Kutokana na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti yake, Zitto, alisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na si uchaguzi.

Alisema pia mwongozo huo, mbali na kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotaka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo, lakini pia inavinyima vyama vingine vyenye uwakilishi bungeni haki ya kuchaguliwa.

Chanzo cha kuaminika kimeema  kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Kanuni, kilichokutana juzi mjini Dodoma chini ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, huku Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akihudhuria.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe pamoja na wajumbe kadhaa, ambapo baada ya kufunguliwa kwa kikao hicho kilichomalizika usiku wa juzi, Spika Ndugai, alihoji uhalali wa Zitto kuandika barua ya kuhoji mgawanyo huo wa wabunge wa EALA.

“Kifupi ni kwamba Zitto amekwama na hana tena namna maana Spika alimsema sana kutokana na mgawanyo lakini kabla ya kuendelea zaidi kwamba alimuuliza Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Kabudi kama kuna tatizo naye akasema hakuna na Spika hajakosea.

“… ila ni kikao ambacho Spika kwa kweli amesimamia sheria na ni kiongozi asiyeyumba katika kusimamia sheria, sasa tunakwenda kwenye uchaguzi huku ukweli ukiwa umeshajulikana, CCM watakuwa na viti sita, Chadema viwili na CUF kimoja,” alisema mtoa habari huyo

Baaada ya majadiliano ya kina na ufafanuzi wa kisheria kuhusu mgawanyo huo wajumbe wa Kamati ya Kanuni walikubaliana na Spika Ndugai kwa kauli moja, huku hoja ya Zitto ikitupwa na uchaguzi huo wa EALA  utafanyika kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya wabunge wa vyama vyenye uwakilishi bungeni.

Hata hivyo kanuni ya 5(5) ya nyongeza ya tatu ya kanuni za Bunge inaeleza “Chama  chochote cha siasa chenye haki ya kusimamisha mgombea wa EALA kinaweza kuweka wagombea watatu katika  ya wagombea ubunge”.

Kutokana na hilo msingi huo wa kikanuni inaonesha kuwa vyama vingine tofauti na Chadema , CUF na CCM, haviwezi kusimamisha wagombea kwa sababu havikidhi kigezo cha kanuni ya 12 za Kudumu za Bunge.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Aliyetumbuliwa na Rais Magufuli Dk Mwele Malecela Ateuliwa Kuwa Mkurugenzi Shirika la Afya Duniani (WHO)


Salamu za pongezi zimeendelea kumiminika kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Dk Mwele Malecela baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika vya Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.

Pia, Dk Mwele  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mpango wa Maalumu wa WHO wa kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele (Espen) na sasa atahamia kituo chake cha kazi Congo-Brazaville. 

Mradi wa Espen ulianza kutekelezwa mwaka 2016 hadi 2020, una lengo la kumaliza magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwa kutoa vifaa tiba, elimu na dawa. 

Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni pamoja na matende, mabusha, kichocho, minyoo ya tumbo na usubi. 

Miongoni mwa waliomtumia pongezi ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Sikika, Irenei Kiria ambaye aliandika katika ukurasa wake wa Twitter: “Hongera Mwele kwa kupata nafasi hiyo ina maana ulipangwa kulisaidia Taifa letu ukiwa nje.”

 Mwingine ni Mhadhiri wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kitila Mkumbo aliyeandika katika ukurasa wake wa twitter akisema: “Nina furaha kwa uteuzi wa Dk Mwele kuwa Mkurugenzi wa WHO.Nahisi kusamehewa kwa kuikosoa Serikali baada ya kumuondoa Nimr.” 

Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile yeye aliandika katika ukurasa wake akimpongeza Dk Mwele na kusema, “Nimezidiwa na furaha baada ya kupata taarifa kuwa umepata kazi kubwa katika ogani ya kimataifa. Mlango mmoja ukifungwa mwingine hufunguliwa. Katumikie vyema.” 

Dk Mwele aliondolewa kuwa Mkurugenzi wa Nimr na Rais John Magufuli Desemba 17 mwaka jana. 
Kuondolewa kwake katika nafasi hiyo kulifanyika siku moja baada ya kutoa ripoti ya utafiti wa magonjwa, ndani yake ikiwamo taarifa ya virusi vya ugonjwa wa Zika katika maeneo ya Morogoro, Geita na Magharibi mwa Tanzania. 

Taarifa ya Dk Mwele, ilieleza kuwa kati ya watu 533 waliopimwa, asilimia 15.6 walibainika kuwa na virusi hivyo. 

Siku moja baada ya kutoa takwimu hizo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa na Dk Mwele aliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo kwamba ugonjwa huo bado haujaingia nchini.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika mikoa yote 31 kwa siku 195


Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 zimezinduliwa rasmi jana katika uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi na unatarajiwa kuzunguka katika mikoa yote 31, ukipita kwenye halmashauri 195 kwa muda wa siku 195.

Katika sherehe hizo za uzinduzi, kiongozi wa mbio hizo kwa mwaka huu pia ametangazwa rasmi, ambapo atakuwa ni Amour Amad Amour kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar.

Kiongozi huyo atasaidiana na wenzake watano katika kukimbiza mwenge huo ambao ni pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi Fatima Yunus Hassan (Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia Mwakitalima (Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi).

Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU'

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kwa niaba ya Rais wa serikali hiyo Dkt. Ali Mohamed Shein, ambapo katika ujumbe wake amesisitiza umuhimu wa watanzania wote kuweka nguvu zao katika kujenga taifa la viwanda

Alisema hadi sasa tangu serikali yake iingie madarakani kwa muhula wa pili tayari viwanda vitatu vya watu binafsi vimekwishajengwa visiwani Zanzibar

Balozi Seif alisema mbali na kaulimbiu ya mwaka huu kusisitiza umuhimu wa viwanda, pia mbio hizo zitakuwa zikieneza ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya Malira, UKIMWI, Dawa za Kulevya pamoja na rushwa.

Mbio hizo zimeanzia katika wilaya ya Mpanda, na kilele chake kitakuwa ni Oktoba 14 katika mkoa wa Mjini Magharibi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya lEo Jumatatu ya April 3


Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.