Monday, August 8, 2016

HUU NI UJUMBE WA HAJI MANARA, SIMBA IKIADHIMISHA MIAKA 80


Haji Manara
Happy birthday my lovely club..80 yrs anniversary
Na Haji S Manara
Watanzania wenzangu hususan wana Simba, tarehe kama ya leo 8-8-1936, wazee wetu ambao wengi wao tayari wapo mbele ya haki walianzisha klabu yetu hii ambayo leo tunaishangilia na kuipenda sana.
Klabu hii ndiyo klabu bora ya karne kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa na rekodi isiyoguswa kwa kutwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa wa vilabu kwa kanda yetu hii, sambamba na kuwa klabu yenye rekodi bora zaidi kwa vilabu vya Tanzania, nje ya mipaka ya nchi yetu.
Wanasimba mnajua wengine watajisikia vibaya kwa mimi kuwakumbusha huo ukweli, ila hiyo ni ‘fact’ isiyohitaji shule kubwa kuijuan kwa vigezo vyovyote vile vinavyokubalika na FIFA na CAF Simba ndio timu bora ya muda wote kwenye zone yetu hii.
Tujivunie ukweli huu na tutembee kifua mbele.
Wanaotupinga hujadili miaka minne ya nyuma ambayo sote tunajua hatujafanya vizuri, lakini niwaambie wanakosea mno, katika miaka minne iliyopita ukuaji wa uchumi kwa taifa la Marekani huwezi kulinganisha na China.
Sasa kiakili utalinganisha Marekani na China kwa ukubwa wa taifa? Lipi taifa kubwa kati ya USA na China kwa vigezo vya taifa imara kiuchumi, kiulinzi, kisiasa na kiutamaduni?
Sisi ni mfano wa Marekani na wao ni mfano wa China, mbingu na ardhi na ndio maana jina letu maarufu ni Simba TAIFA KUBWA.
Najua miaka hii themanini tumepitia changamoto nyingi sana ambazo nyingine si nzuri hata kidogo, lakini siijui klabu yenye umri kama wetu duniani isiyopitia maswahibu kama yetu.
Moja ya changamoto kubwa tuliyonayo ni kutojitegemea kama klabu na kutokuwa na uwanja wake wa mazoezi wenye hadhi ya TAIFA KUBWA.
Kwa sasa hili la uwanja uongozi wenu unaongozwa na Rais Evans Aveva umeamua kulivalia njuga, hivi ninavyoandika ujumbe huu, mkandarasi yupo SITE tayari ujenzi wa uwanja wa mazoezi unajengwa na ndani ya majuma machache yajayo jiwe rasmi la msingi litawekwa na ndani ya msimu huu tutaanza kuutumia.
Uwanja huu utakuwa ni wa nyasi bandia na pia utakuwa na hosteli ya kuishi wachezaji wetu wanapokuwa kambini na huduma muhimu zinazopaswa kuwepo kwenye kambi ya klabu yenye hadhi kama ya Simba.
Ieleweke kwa sasa kipaumbele ni kuanza na sehemu ya kuchezea, ambayo inatutafuna mamilioni ya shilingi kwa kukodisha viwanja vya kufanyia mazoezi.
Kuhusu kutokujitegemea kwa klabu, huu ndio mzigo mzito tulio nao kwa miaka yote, Simba inaendeshwa kwa kutegemea wafadhili na kwa miaka ya karibuni wadhamini, huku mapato ya mlangoni yakiwa ndio chanzo kikuu cha mapato kinachoendesha klabu, sambamba na sehemu tulizopangisha kwenye majengo yetu yaliyopo mtaa Msimbazi jijini Dar es salaam. Huku pia tukipata ‘kiduchu’ sana toka kwa wanachama wetu kama ada ambao baadhi yao nao hutegemea ufadhili wa kulipiwa ada hasa inapofika wakati wa uchaguzi mkuu wa klabu.
Kwa mapato na vyanzo hivyo ni wazi sasa laizma tutoke hapo, ni lazma tubadilishe fikra zetu kwa Simba mpya, hatuwezi kuwa na muundo huu tena baada ya kuishi nao kwa miaka themanini.
Rai yangu kwa wanachama na wapenzi wa Simba, kwa kuwa uongozi wetu nao unaafiki mabadiliko ya kimuundo mpya, sote tushirikiane kuleta Simba mpya.
Haitapendeza katika kipindi hiki kulumbana mitandaoni au kwenye vyombo vya habari kwa kisingizio cha mabadiliko, mabadiko yaje huku tukiwa wamoja, yaje huku tukiwa na mawazo huru, yaje huku tukiwa tunajua sisi sote tutakuja kuandikwa kwenye historia ya klabu yetu kuwa kizazi flani kilileta mabadiliko ya kimuundo lakini kubwa yaje huku tukirejeshe heshma ya klabu ambayo imeyumba katika miaka minne ya nyuma.
Simba mwaka huu licha ya kutaka mabadiliko, kipaumbele chake kikuu ni vikombe, na ndio raha na furaha ya mwanasimba, uongozi, wanachama, wachezaji na benchi lao la ufundi na mashabiki wote.
Lazima tuwe wamoja, tuondoe chochote kile kitakachotugawa, sisi ni wamoja kiasili na ndio maana kaulimbiu yetu inasema hivyo umoja wetu hauthaminishwi na chochote kile. Wenzetu kwa bahati mbaya unaunganishwa na kitu, sisi umoja wetu ni wa damu na unaandikwa kikatiba, tusifarakane hata kidogo kwenye kipindi hiki, tuwe na subira na hayo mabadiko na uongozi naamini kwa uharaka utatekeleza maamuzi ya mkutano mkuu wa 31-7-2016.
Niwaombe sana wanasimba wenzangu ujaji wa badiliko lolote kubwa lazma liende sawia na fikra pevu zitakozoelewa nini tunataka kwa Simba ijayo, tusikurupuke kwa jazba au mihemko na tukifanya hivyo tutakuja ‘kuazimwa’ kama dera la kwendea harusini. Tujiongeze hasa nini tunataka, huku tukipokea elimu pana ya mifumo ya uendeshaji wa vilabu vilivyofanikkiwa zaidi Afrika na duniani kwa ujumla nasisitiza muundo wowote tutakaochagua, uwe wa hisa au mwingineo, lazima tuujue vizuri faida na hasara zake na hapa uongozi hatuna budi kuandaa utaratibu wa kuelimisha watu wetu kuepukwa na sisi  ‘kuazimwa.’
Mwisho niwaombe sana mliopo jijini na mikoa ya jirani tuje uwanja wa taifa mchana huu kuadhimisha miaka themanini ya klabu yetu, pia leo ni kilele cha wiki yetu inayotuingiza kwenye msimu mpya.
Jioni ya leo tutajua sura ya timu yetu msimu ujao wa ligi, njooni mumshangilie mnyama, njoon tuujaze uwanja, njooni tuoneshe tofauti yao na sisi…
Mungu ibariki Simba
Mungu ibariki Tanzania
Imeandikwa na
Haji S Manara
Happy birthday Simba SC.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment