Monday, August 8, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
tukutane pamoja

Alitaja masharti ambayo jeshi hilo liliwapa kuwa ni pamoja na kutokuwapo kwa maandamano ya bodaboda, ya miguu au magari, kutokukashifu chama au utawala wa kiongozi yeyote na kuzingatia muda wa kuanza na kumaliza mkutano. Alisema kuwa cha kushangaza jana baada ya kukamilisha maandalizi yote ikiwamo kufanya matangazo na kufunga vyombo vya muziki, baadhi ya viongozi waliitwa kwenye Ofisi ya Polisi Wilaya ya Chalinze na kuambiwa wasifanye mkutano huo. Alisema walielezwa kuwa ujumbe ambao unaenea kwenye mtandao unasema mkutano huo utaleta watu wengi sana, hivyo usalama utakuwa mdogo. Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Boniventura Mushongi alisema lengo la Polisi si kuwakataza kufanya mkutano, lakini kilichoonekana ni kuwa walikiuka maelekezo kwani awali walipaswa kufanya mkutano wa ndani na si wa nje. “Sisi hatuwakatazi kufanya mikutano yao, lakini ni vema wafuate makubaliano, maana sisi Jeshi la Polisi tuliwaruhusu wafanye mkutano wa ndani lakini tulishangazwa kuona wanaanza kufanya nje huku wakipiga muziki,” alisema. Mushongi alisema pia polisi inazuia mikutano yote ambayo haina madiwani wala wabunge katika eneo husika, jambo ambalo halikuwa kwenye maelekezo ya OCD. “Chadema katika eneo la Chalinze hawana diwani wala mbunge, hivyo wamekosa sifa za kufanya mkutano huu. Kama ni kikao cha ndani hatuna tatizo wafanye hata wakialika watu 200,” alisema Mushongi. Hata hivyo, Mushongi alisema Chadema Pwani walipopeleka barua ya maombi mkutano huo walipewa masharti hayo. Mbowe: Tuko tayari kwa lolote Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema yeye na makamanda wake wako tayari kwa lolote kwa ajili ya kutetea misingi thabiti ya utawala bora unaoheshimu utawala wa sheria. Akizungumza jana, Mbowe alisema hakuna mtu wa kuwafundisha makamanda wa Chadema, hivyo mikutano ya Ukuta itafanyika nchi nzima kuanzia Septemba Mosi. “Ambao hawako tayari warudi nyuma, hakuna aliyelazimishwa, watuache sisi tutangulie wa kufa wafe na wa kupona wapone. Haiwezekani mtu apuuze sheria, avunje katiba halafu taifa linyamaze,” alisema. “Sisi tumeamua kuchukua mzigo huo kwa niaba ya wananchi wote. Kama ataua wacha aue tu, kama atatufunga wacha atufunge tu lakini tutakuwa tumeacha legacy (kumbukumbu) duniani,”alisisitiza. Mbowe alisema sifa ya kiongozi bora anayeheshimu misingi ya kidemokrasia ni kuheshimu utawala bora unaoheshimu utawala wa sheria. Kwa mujibu wa Mbowe, Rais anakiuka Katiba na sheria za nchi zinazoruhusu vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara na hakuna mtu ndani ya CCM anayezungumzia hilo. Mbowe alisema Rais amejisahau kuwa yeye (Mbowe) ni mwenyekiti wa taifa kama alivyo Rais, hivyo anastahili kuzunguka nchi nzima kujenga uhai wa chama. “Rais anazunguka kwenye mikoa anavisema vyama vya upinzani na kutoa amri mbalimbali lakini sisi (upinzani) hatuna jukwaa la kujibu au kutoa ufafanuzi. Anasema tusubiri hadi 2020,” alilalamika Mbowe. “Rais anatoa amri, wakuu wake wa mikoa wanatoa amri, wakuu wa wilaya wanatoa amri, watu wanafukuzwa kazi ovyo. Nchi haiwezi kwenda kwa staili hii,” alisema. “Wewe unanyanyuka tu na kusema watu wahamie Dodoma kivipi? Issue ya kuhamia Dodoma ni suala la kitaifa siyo mamlaka ya mtu mmoja tu kwa kuwa ni Rais.”Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Created By Designscrazed
No comments:
Post a Comment