Sunday, July 10, 2016
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Barua pepe za Hillary Clinton kuchunguzwa upya
Kirby vile vile amekanusha shutuma kwamba wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marakeni ina utamaduni wa uzembe kuhusu masuala ya mawasiliano.
''Madai ya kwamba wizara hii kama taasisi, ina utamaduni wa uzembe, hatukubaliano nayo, na kama alivyosema mkurugenzi wa FBI, hayo siyo kweli, wala hayakuwa sehemu ya uchunguzi na mapendekezo yaliyotokana na uchunguzi huo.'' Amesema Kirby.
Clinton ayaponyoka mashitaka
Mwanzoni mwa wiki hii shirika la upelelezi la Marekani, FBI lilipendekeza Bi Clinton ambaye ananuia kugombea urais wa Marekani katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu, asifunguliwe mashitaka yoyote, kutokana na kutumia kwake anuani binafsi ya barua pepe kwa masuala nyeti ya kikazi, wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nchi za nje kati ya mwaka 2009 na 2013. Pendekezo hilo liliheshimiwa na wizara ya sheria.
Ingawa uamuzi huo ulimpa ahueni Bi Clinton, mkurugenzi wa FBI James Comey alisema bayana kwamba Clinton alifanya uzembe kupita kiasi katika mawasiliano hayo ya barua pepe.
Pendekezo la kutomfungulia mashitaka Hillary Clinton liliwachukiza warepublican, akiwemo Donald Trump ambaye anatarajiwa kuwa mpinzani wa Bi Clinton katika uchaguzi wa Novemba, wakisema kiongozi huyo amekwepa mkondo wa sheria kutokana na hadhi yake kama mwanasiasa wa ngazi ya juu.
FBI kibanoni
Jana Mkurugenzi wa FBI alilazimika kulitetea pendekezo la kutomshitaki Bi Clinton, katika kamati ya bunge inayohusua uchunguzi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje John Kirby hakutoa maelezo zaidi kuhusu uchunguzi huu mpya, mbali na kusema utakuwa na uwazi mkubwa,na utaheshimu majukumu yao kisheria.
Mkurugenzi wa FBI amesema miongoni mwa barua pepe 30,000 ambazo Hillary Clinton alizikadhi kwa shirika lake, 100 zilikuwa na taarifa nyeti. Nyingine 2000 zilipandishiwa hadhi ya unyeti, na kufanywa nyaraka za siri.
Wakati sakata hilo likiendelea kuvuma, Bi Hillary Clinton ameungana na makamu wa rais wa Marekani Joe Biden katika kampeni jimboni Pennsylvania, katika kuhamasisha umoja ndani ya chama cha Democratic, kabla ya mkutano wake mkuu utakaoanza tarehe 25 mwezi huu.
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Obama kurejea nyumbani mapema; mauaji yaitikisa Marekani
Polisi waligundua vifaa vya kutengenezea mabomu na silaha katika nyumba ya kijana huyo Micah Johnson mwenye umri wa miaka 25, mkaazi wa eneo la Dallas ambaye aliwapiga risasi polisi watano kabla ya kufariki katika mapambano ya silaha na polisi.
Ikulu ya Marekani ya White House imeondoa uwezekano wa mahusiano kati ya mshambuliaji huyo mwenye silaha na makundi yanayotambulika ya kigaidi, mahusiano katika ukurasa wake wa Facebook yanaelekeza katika makundi ya wanaharakati wenye msimamo mkali ya Wamarekani weusi ambayo yameorodheshwa kuwa ni makundi ya chuki nchini Marekani.
Akielezewa na polisi kuwa ni mshambuliaji aliyeamua kutenda kitendo hicho peke yake na hakuwa na rekodi ya uhalifu hapo nyuma , Johnson aliwaambia watu waliokuwa wanafanya nae majadiliano kabla ya kufariki kwamba alitaka kuwauwa polisi wazungu kwa kulipiza kisasi kutokana na kuuwawa kinyama hivi karibuni kwa watu wawili weusi.
Maandamano ya amani
Mashambulizi hayo jimboni Texas, ambayo yalizuka siku ya Alhamis usiku wakati wa maandamano ya amani dhidi ya ukatili wa polisi, yanakuja katika wakati wa hali ya kutafakari kuhusiana na matumizi ya silaha kwa ulinzi wa amani kuelekea Wamarekani weusi.
Viongozi wa harakati za Maisha ya Weusi ni muhimu wameshutumu mauaji hayo mjini Dallas, huku wakiapa kuendelea na maandamano yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa juma, huku makundi makubwa ya watu wakijikusanya usiku wa Ijumaa mjini Atlanta Georgia na wengine wengi wakiwa nje ya Ikulu ya Marekani White House.
Akihutubia maelfu ya watu katika sala iliyofanyika kwa heshima ya maafisa wa polisi waliouwawa, meya wa Dallas Mike Raswlings amewataka Wamarekani , kuimarisha hatua , kuponesha vidonda vya ubaguzi nchini humo.
Maandamano yataendelea
"Hatutajitenga na ukweli uliopo kwamba sisi kama wakaazi wa mji, wa jimbo, na kama taifa tunapambana na masuala ya kibaguzi," ameliambia kundi la watu waliokusanyika.
Rawlings amerudia ujumbe uliotolewa na rais Obama wakati taifa hilo linahangaika kutokana na ghasia hizo za hivi karibuni: Kwamba maisha ya weusi ni muhimu , na kama ilivyo kwa maisha ya wazungu, wale maafisa wa polisi.
"Tunapaswa kuongeza nguvu na kuyakabili masuala tata kwa njia nyingine," amesema Rawlings. "Na masuala ya kibaguzi yanautata."
Obama , ambaye ameamuru bendera zote zipepee nusu mlingoti katika majengo ya serikali kwa muda wa siku tano, aliweka wazi kwamba ghasia dhidi ya polisi, haziwezi kuhalalishwa kabisa."
Rais alizungumzia mashambulizi hayo akiwa katika mji mkuu wa Poland, Warsaw , ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa kilele wa NATO, na kuiita hali hiyo , "inayojirudia na ya kukera."
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Takriban 150 wauwawa katika mapigano Sudan Kusini
Chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mafunzo mjini Juba ambayo ni hospitali kuu ya serikali imepokea zaidi ya maiti tisini za askari na raia ambapo kwa mujibu wa daktari mmoja katika hospitali hiyo ambaye amekataa kutajwa jina lake amesema nyingi ya maiti zilikuwa za wanaume.
Jeremiah Young mfanyakazi wa misaada wa shirika la hisani la World Vision aliyeko Juba amesema "kuna watu wanaotembea mitaani lakini wana wasi wasi mkubwa na kwamba kuna uwezekano wa hali kuzidi kuwa mbaya."
Hali ni shwari Juba
Kwa upande wake Gatijach Deng msemaji wa kitengo cha kijeshi katika kundi la Machar amesema mapigano hayo yalitokea karibu na Ikulu na katika kambi za kijeshi.Deng amesema hapo asubuhi walikusanya maiti 35 kutoka upande wa kundi la (SPL-IO) la Machar na themanini kutoka vikosi vya serikali.Amesema yumkini idadi ya vifo ikaöngezeka kwa upande wa kundi la Machar kutokana na kwamba majeruhi wengi wako mahtuti.
Takriban wanajeshi watano waliuwawa hapo Alhamisi katika mapambano kama hayo kati ya pande hizo mbili.
Taifa hilo changa kabisa barani Afrika linaibuka kutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe vilioanza hapo mwezi wa Disemba mwaka 2013 baada ya Kiir kumtimuwa Machar katika wadhifa wa makamo rais.
Vita hivyo vilipiganwa kwa kiasi kikubwa chini ya misingi ya kikabila ambapo Kiir alikuwa akiungwa mkono na kabila lake na Dinka na Machar akiungwa mkono na kabila lake la Nuer.
Makubaliano ya amani
Makubaliano ya amani yaliofikiwa mwezi wa Augusti yalikomesha vita hivyo lakini Kiir na Machar bado hakuviunganisha vikosi vyao kipengele muhimu katika makubaliano hayo.
Mapigano hayo ya Alhamisi na Ijumaa ni kuibuka kwa matumizi makubwa ya nguvu kuwahi kushuhudiwa mjini Juba tokea Machar arudi katika mji mkuu huo hapo mwezi wa Aprili baada ya kumchaguwa tena kama makamo wa rais wake.
Shuhuda wa shirika la habari la Uingereza amesema hapo Jumamosi kwamba Juba iko shwari lakini kuna wasi wasi mkubwa ambapo katika baadhi ya barabara kumewekwa vizuizi vya barabara. Magari makubwa ya kijeshi yameonekana yakipiga doria na takriban shughuli zote za kibiashara zimefungwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewahimiza viongozi wa nchi hiyo kutekeleza makubaliano hayo ya amani na kwamba kinachojidhihirisha hakuna kujitolea kwa dhati katika makubaliano hayo.
Sudan Kusini ambapo vita vyake vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisa kushuka kwa uzalishaji wake wa mafuta vimefuta sherehe za kuadhimisha siku ya uhuru wa nchi hiyo kutokana na ukosefu wa fedha.
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Syria yarefusha muda wa kusitisha mapigano
Shirika la habari la Syria SANA limesema uongozi wa jeshi umerefusha , "muda wa siku tatu wa utulivu" ambao ulimalizika usiku wa manane siku ya Ijumaa. Usitishaji huo sasa utaendelea kwa masaa mengine 72 hadi usiku wa manane siku ya Jumanne.
Tamko la kusitisha mapigano lililotangazwa siku ya Jumatano limeingiliana na kuanza kwa sikukuu ya Idd ul-Fitr, ambayo inaadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kiasi ya raia 155, ikiwa ni pamoja na watoto 48, waliuwawa katika mapigano yaliyotokea katika sehemu mbali mbali za Syria wakati wa sikukuu hiyo iliyodumu kwa siku tatu, limeripoti shirika la linaloangalia haki za binadamu nchini Syria.
Tangazo la kurefusha usitishaji mapigano
Kurefushwa kwa usitishaji mapigano kulitangazwa wakati majeshi ya serikali na waasi yakiendelea kupigana kuwania udhibiti wa njia pekee kuingia katika eneo la mashariki ya mji wa Aleppo linalodhibitiwa na waasi, huku kukiwa na mashambulizi ya makombora kutoka kila upande katika sekta zote za mji huo uliogawika.
Shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria limeripoti mashambulizi mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga katika magari yaliyofanywa na tawi la al-Qaeda , la al-Nusra Front, katika jaribio la kuyarejesha nyuma majeshi ya serikali ambayo siku ya Alhamis yamedhibiti na kuzuwia barabara muhimu ya Castello, njia pekee ya kujipatia mahitaji kwa eneo linaloshambuliwa sana la mashariki.
Shirika la habari la Syria SANA, likinukuu duru za kijeshi ambazo hazikutajwa , limesema kwa majeshi ya serikali siku ya Jumamosi yalipanua udhibiti wao kuzunguka barabara muhimu ya Castillo.
Hasara kubwa kwa waasi
Hatua hiyo inayodaiwa ya kusongambele imekuja baada ya majeshi ya serikali kutoa kipigo kikali na kusababisha "hasara kubwa" katika kile shirika hilo ilichosema kuwa ni "magaidi" likimaanisha waasi wanaopigana kuuondoa utawala wa rais Bashar al-Assad.
Kiasi ya raia 38 waliuwawa usiku wa Ijumaa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na waasi katika eneo la Aleppo magharibi linalodhibitiwa na serikali, kwa mujibu wa shirika hilo linaloangalia haki za binadamu, ambalo linakusanya ripoti zake kutokana na mtandao wake wa wanaharakati ndani ya Syria.
Wakati huo huo , kiasi ya raia 17 wameuwawa , ikiwa ni pamoja na watoto sita , waliouwawa katika mashambulizi ya makombora na ya anga yaliyofanywa na jeshi la serikali katika sekta ya mashariki ya mji wa Aleppo.
Wizara ya ulinzi imesema helikopta ya Syria ikirushwa na marubani Riafagat Khabibulin na Yevgeni Dolgin " ilishambuliwa " na wapiganaji wa IS jana Jumamosi na kuanguka na kuwauwa marubani wote wawili.
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Msichana mweusi kuwa Iron Man
Atachukua majukumu hayo kutoka kwa Tony Stark.
Mhusika Riri Williams ni mzaliwa wa Chicago ambaye ni gwiji wa sayansi na anasomea chuo cha MIT.
Mtunzi wa hadithi za Iron Man Brian Michael Bendis ameambia gazeti la Time kwamba alibuni mhusika Williams baada ya kuguswa na “visa vya ghasia, fujo na ukatili” ambavyo vilikuwa vinatokea Chicago alipokuwa anafanya kazi huko.
“Na simulizi hii ya mwanamke kijana, mwerevu ambaye maisha yake yamekumbwa na mikasa na hatari ambayo ingeangamiza maisha yake, ghasia mitaani, na alifanikiwa kwenda chuo ilinigusa sana,” amesema.
"Nilifikiri hiyo ni aina ya kisasa zaidi ya hadithi ya shujaa ambayo nimewahi kuisikia.”
Mhusika wa Iron Man alianza kutumiwa mara ya kwanza 1963.
Habari kwamba mhusika wa sasa atakuwa mwanamke na mweusi imesifiwa na wengi wanaoitazama kama hatua ya kukumbatia jinsia na watu wa asili mbalimbali.
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Simu milioni 10 za Android zaathiriwa na kirusi
Kirusi hicho kinawapatia takriban dola 300,000 kila mwezi waliokianzisha.
Simu nyingi ambazo zimeathiriwa na kirusi hicho zipo nchini China
Ongezeko la simu zilizoathiriwa na kirusi hicho lilibainika na kampuni ya usalama wa mitandao Checkpoint na Lookout.
Kirusi hicho kinatoka familia ya Shedun by Lookout but Hummingbad by Checkpoint.
Katika blogu,Checkpoint imesema kuwa imefanikiwa kubaini kithibiti cha simu zilizoathiriwa ambacho kinaonyesha kuwa Hummingbad imeathiri simu milioni 10.
China ,India,Ufilipino na Indonesia zinaongoza katika mataifa yenye simu zilizoathirika.
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Boko Haram yashambulia kambi ya jeshi Nigeria
Wanajeshi wawili waliuawa huku wenyeji wakisema kuwa raia 7 nao walipoteza maisha yao.
Harakati za Boko Haram ambazo zimedumu kipindi cha miaka 7 zimesababisha vifo vya takriban watu 20,000 kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuwalazimu karibu watu milioni 2 kuhama makwao.
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Mapigano yazuka upya Sudan Kusini
Kanali Gatjiath anasema wanajeshi hao wanalipiza kisasi kufuatia mashambulizi makali kutoka kwa jeshi la rais Kiir.
Serikali haijasema lolote tangu machafuko hayo yaanze muda mchache uliopita.
Awali Wanajeshi wanamuunga mkono makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar walisema kuwa kambi yao ilishambuliwa usiku wa kuamkia leo kwa risasi na bunduki nzito nzito.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini unasema kuwa kulitokea ufyatulianaji wa risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba..
Maeneo yanayodhaniwa kuathirika sana ni yale ya Jebal.
Ujumbe huo unasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa rasasi ulishuhudiwa karibu na kambi ya umoja wa mataifa
Siku za hivi majuzi ziaidi ya watu 100 wanaripotiwa kuuawa mjini Juba wakati wa mapigano kati ya wafuasi wa rais Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar
Wawili hao walikubaliana kumaliza vita vya wenywe kwa wenyewe na wametoa wito wa kuwepo utulivu.
Ripoti za awali kutoka nchini Sudan Kusini zilisema kuwa takriban watu 100 waliuawa wakati wa mapigano kati ya wanajeshi hasimu katika mji mkuu Juba.
Hata hivyo idadi kamili bado haijulikani lakini wengi wa wale waliouawa wanaripotiwa kuwa wanajeshi.
Mapigano hayo yaliyoanza siku ya Alhamisi yaliendelea hadi mapema Jumamosi.
Mwandishi wa habari mjini Juba anasema kuwa wanajeshi wameweka vizuizi vya barabarani mjini humo.
Anasema kuwa masoko yamefunguliwa lakini watu wengi wamebaki nyumbani.
Sudan Kusini inaadhimisha miaka mitano ya uhuru wake.
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.