Tuesday, March 28, 2017

Nape Akabidhi Ofisi Kwa Mwakyembe


Aliyekuwa Waziri wa Habari Nape  Nnauye amemkabidhi ramsi ofisi Waziri mpya wa Habari, Dkt Harrison George Mwakyembe.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Malawi Yaichokonoa Tena Tanzania Kuhusu Ziwa Nyasa


Rais wa Malawi, Peter Mutharika ameanza tena chokochoko baada ya kutangaza kuwa hakuna nchi ambayo inamiliki kwa pamoja Ziwa Nyasa na kwamba haijafikia makubaliano na nchi yoyote, hivyo ameahidi kulinda umiliki na masilahi yake.

Kauli hiyo ni tofauti na mazungumzo ya Mutharika na Rais John Magufuli yaliyofanyika Januari 30 jijini Addis Ababa, Ethiopia wakati walipokuwa wakihudhuria kikao cha Umoja wa Afrika (AU).

Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Rais baada ya kikao hicho, ilisema marais wote wameridhishwa na jitihada zinazofanywa na jopo la usuluhishi lililoteuliwa na Umoja wa Maendeleo wa Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc).

Jopo hilo linaongozwa na rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mindi Kasiga amekiri kuiona taarifa hiyo na alisema anayeweza kulizungumzia suala hilo ni Naibu Waziri.

“Tumeiona hiyo taarifa ila jaribu kumtafuta Naibu Waziri maana Waziri atakuwa nje ya nchi. Ninachofahamu baraza la usuluhishi bado linaendelea na vikao vyake. Ukimpata naibu waziri atakuwa na maelezo ya kina.”alisema Mindi.

Lakini, akihudhuria Siku ya Maji Duniani Jumatano iliyopita mjini Mangoshi, Rais Mutharika alisisitiza msimamo wa Malawi kulinda umiliki wa ziwa hilo dhidi ya watu aliowaita wavamizi.

Mutharika alisema Malawi ndiye mmiliki pekee wa Ziwa Malawi, ambalo huku linajulikana kama Ziwa Nyasa, na kuonya kuwa utawala wake hautavumilia watu watakaokuwa na nia ya kuyumbisha taarifa za umiliki.

“Hebu tulilinde ziwa letu. Hili ni ziwa letu na ninaposema ziwa letu namaanisha ziwa lote. Mtu yeyote asifanye kosa la kubadili umiliki ambao umekuwepo kwa miaka 124 iliyopita,” alisema Mutharika akikaririwa na tovuti ya Nyasa Times ya Malawi juzi wakati wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Nkopola Lakeshore mjini Mangochi.

“Tunathamini ziwa letu na tutahakikisha tunachukua hatua za kulilinda kwa gharama zozote,” alisema.

Mutharika aliwataka wananchi kupunguza matumizi mabaya ya maji ili yapatikane kwa ajili ya kilimo na viwandani wakati wa msimu wa ukame.

Hivi karibuni, Malawi na Tanzania zimejikuta katika mzozo wa umiliki wa Ziwa Nyasa lililo kusini mwa Tanzania, mzozo ambao umesababisha kuanza kwa mazungumzo ya usuluhishi kumaliza kutokubaliana huko baada ya nchi hizo mbili kushindwa kufikia muafaka. Mzozo wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa umekuwepo tangu mwaka 1967.

Lakini, mzozo wa hivi karibuni umeibuka baada ya Malawi kuanza utafiti wa mafuta na gesi kwenye ziwa hilo.

Hata hivyo, Mutharika alisema uchimbaji mafuta utaendelea katika ziwa hilo licha ya wanaharakati wa mazingira kuitaka Malawi iache mpango huo.

“Wale wanaohofia kuhusu mipango yetu ya kutafuta na kuchimba mafuta hawana sababu ya kuhofia. Kama tutaamua kuchimba mafuta katika ziwa, tutahakikisha tunatumia teknolojia safi,” alisema akikaririwa na Nyasa Times.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Saturday, March 25, 2017

CHADEMA Kuwasha Moto Bungeni


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema matukio yaliyotokea hivi karibuni likiwamo la aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kutolewa bastola, yanaweza kubadili upepo wa Bunge linalotarajiwa kuketi siku chache zijazo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, aliwaambia hayo waandishi wa habari jana waliotaka kufahamu mipango ya chama hicho katika kutumia mhimili wa Bunge kutokana na uwepo wa matukio ya uvunjaji wa sheria.

Katika hilo, Mnyika alisema Watanzania watarajie Bunge lijalo la Bajeti kuwaka moto.

“Sisi ndio tunaongoza Kambi Rasmi ya Upinzani na ambacho ninaweza kuwaambia Watanzania ni kwamba watarajie Bunge la Bajeti kuwaka moto juu ya utendaji wa Serikali. Sasa kuwaka moto namna gani na kuhusu nani ni masuala ambayo yataonekana katika hatua ya baadaye. Naamini safari hii haitakuwa wabunge wa Chadema, Ukawa pekee, naamini Bunge litakuwa kitu kimoja katika kuchukua hatua,” alisema Mnyika.

Chadema Yanunua Ugomvi wa Nape
Katika hatua nyingine chama hicho kimemtaka Rais Dk. John Magufuli ajitokeze waziwazi na kusema sababu za kumwondoa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Pamoja na hilo, kimetaka Rais Dk. Magufuli aseme iwapo alitoa maelekezo kwa vyombo vya usalama waliovamia ofisi za Clouds Media Group na yule aliyemtolea bastola Nape alipokuwa akizuia asizungumze na vyombo vya habari juzi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, aliyezungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuhusu ajenda mbili zilizozungumzwa katika kikao cha Kamati Kuu Maalumu ya chama hicho kilichoketi Machi 22 na 23, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Ni vyema Rais akaeleza kwa kuwa taarifa za Ikulu hazikufafanua kwanini amemwondoa Nape. Aeleze waziwazi sababu za kumwondoa Waziri katika kipindi ambacho taarifa ya kamati iliyoundwa imetolewa ambayo imeeleza wazi makosa yaliyofanywa na mteule wa rais katika siku chache tu baada ya kumkingia kifua.

“Imeonekana matumizi mabaya ya wazi ya watumishi wa vyombo vya usalama ikiwamo waliovamia kituo cha Clouds kwa bunduki, aliyemtolea Nape bastola, rais ndiye msimamizi wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, awaeleze Watanzania iwapo askari na wanausalama hao wamefanya kazi kwa maelekezo yake,” alisema Mnyika.

Alisema kama sivyo ni hatua zipi ameelekeza zichukuliwe kwa wahusika wa mambo hayo.

Mnyika alisema chama hicho kinapinga mwenendo wa matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kulindwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na matukio ya hivi karibuni yanayogusa uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo kuvamiwa kwa kituo cha Clouds Media Group pamoja na kitendo cha Nape kutolewa bastola.

“Uamuzi wa kumlinda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa gharama hata ya kumwondoa Waziri wake ni wazi ni matumizi mabaya ya madaraka. Na matumizi haya mabaya ya madaraka yamejipenyeza sasa hayamhusu Rais tu pekee bali pia watendaji wake na vyombo mbalimbali,” alisema Mnyika.

Alisema nchi imeanza kuwa ya kipolisi na matumizi ya vyombo vya dola katika masuala ambayo havipaswi kutumika.

“Tunatoa pole kwa wanahabari kwa mambo hayo pamoja na Nape kwa haya yanayomkuta,” alisema Mnyika.

Alisema haki inapovunjwa mahali popote na kwa raia yeyote, wao kama chama hawasiti kutoa kauli ya kukemea.

Mnyika aliwataka Watanzania kuungana kupinga mabaya yanayofanywa na Serikali ili kulinusuru Taifa na hatari zinazoikumba na zitakazoendelea.

“Taarifa nilizonazo kutoka vyanzo vyangu serikalini ni kwamba, Rais ameamua kumlinda RC kwa sababu eti Chadema kupitia kwa Mwenyekiti Mbowe ilitoa msimamo wa kumtaka amchukulie hatua. Watu ndani ya Serikali wanasema kama atamchukulia hatua eti Rais ataonekana amekidhi matakwa ya Chadema,” alisema Mnyika.

Alisema chama chao kina wajibu wa kuikosoa Serikali iwapo haifanyi kazi sawa sawa na Rais anawajibika kwa wananchi na si Chadema.

Mnyika alikumbusha kuwa wakati walipotangaza Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta), waligusia kauli kuwa; anapoonewa yeyote, unapokuwa kimya, haki inapovunjwa kwa mtu mmoja ukadhani kwamba haikuhusu, ikaenda kuvunjwa kwa mtu mwingine ukanyamaza kimya ukadhani kwamba haikuhusu, ipo siku jambo litakukuta mwenyewe na hakutakuwa na mtu wa kupaza sauti kwa niaba yako.

Alisema kauli hii ilionekana kuwahusu upinzani pekee lakini hivi sasa imejidhihirisha tofauti kutokana na athari zinazojitokeza kwa raia, vyombo vya habari na baadhi ya wanaCCM.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Kauli ya Waziri Dkt Mwanyekembe kuhusu madai ya RC Makonda kuvamia Clouds


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, jana baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam, amekiri kuwa anafahamu kuhusu tukio la uvamizi lililofanyika katika ofisi za Clouds Media Group.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mwakyembe aliyechukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alisema kuwa yeye kwa sasa hawezi kulizungumzia tukio hilo wala kutoa uamuzi wowote kwa kuwa hajapata ushahidi unaojitegemea.

“Ninachokijua kuhusu hilo tukio kinatokana na taarifa za vyombo vya habari, taarifa za magazeti, za redio, za televisheni, na sidhani kama taarifa hizo zinatosha kwa mimi kutoa uamuzi wowote.”

Ameongeza kuwa bado suala hilo ni la kuchunguzwa zaidi kwani picha inayotolewa ni ya upande mmoja.

“Mlalamikaji hapa ni Clouds, anayetupa taarifa kuhusu suala hili zima ni Clouds na wenzake. Kwa hivyo naipata picha hii kwa upande mmoja…”

Aidha kwa mujibu wa ripoti iliyokuwa imetolewa na kamati iliyoundwa na aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ilisema kuwa wamesikiliza upande wa mlalamikaji (Clouds Media Group).

Lakini walipokwenda kwa ajili ya kuusikiliza upande wa mlalamikiwa (RC Paul Makonda) hawakufanikiwa kumpata. 
Hii ni baada ya wao kusubirishwa kwa muda mrefu  nje ya ofisi yake na baadae kuambiwa kuwa Makonda ameondoka na hatoweza kurudi kwa siku hiyo. Jambo hili liliwafanya wajumbe hao kujiaminisha kuwa Makonda hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo na aliamua kuwatoroka.

Hata hivyo ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ili aifikishe katika mamlaka husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Friday, March 24, 2017

Download Audio: Lady Jaydee & H Art The Band – Rosella [Club version]



 
 
https://my.notjustok.com/track/download/id/197897/by/PGj2XDRZfw
 
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

VIDEO: Rais Magufuli Katoa ONYO Kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Wakati akiwaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi, Ikulu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John P. Magufuli, leo amewaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi pamoja na mabalozi kadhaa Ikulu Jijini Dar.
Mwakyembe ameapishwa kuwa Waziri mpya wa habari, Profesa Kabudi kaapishwa kaapishwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria.
==>Haya ni mambo machache aliyoyasema Rais Magufuli Leo
1.Kuna wengine walisema Kinana leo angezungumza na waandishi, wakati nimemtuma India ambapo atakuwa kwa zaidi ya siku 10
2.Tunataka kuitoa nchi katika hali ya mazoea kuipeleka katika mstari ambao ni sahihi

3.Ukiangalia siku iliyofuata baada ya Rais wa Benki ya Dunia kuja, magazeti yote yaliandika habari nyingine tofauti-

4.Niwatake waandishi wa habari muwe wazalendo, Tanzania ikiharibika na nyie pamoja na wanaowatuma muandike wote mtaharibikiwa

5.Hata magazeti ya leo yana picha ya mtu mmoja ambaye amefanya kosa moja, utadhani kosa ni linaungwa mkono na serikali

6.Niwatake wamiliki wa vyombo vya habari muwe waangalifu, kama mnadhani mna uhuru wa namna hiyo, kuweni makini sana

7.Kuna vyombo vingine vya habari sehemu yenye ugomvi ndio wanapeleka kamera na habari hizo zinapewa muda mrefu, 'watch out'

8.Vyombo vingine haviandiki mazuri ya mtu, lakini wakipata mabaya yake ndiyo yanajaza kurasa
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Wednesday, March 22, 2017

new music mp3 wanginja ryder i wann tell tz



       
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Madaktari Kenya Wawaonya Madaktari wa Tanzania Wanaotaka Kwenda Kenya


Chama cha Madaktari wa Kenya (KMPDU), kimewataka wenzao wa Tanzania wasikubali kusaini mkataba wowote wa kwenda Kenya kabla mgogoro wao na Serikali haujatatuliwa.

Taarifa ya KMPDU  inasema haina tatizo na uwezo ama mafunzo ya madaktari wa Tanzania na protokali ya leseni za madaktari inayotambulika na Baraza na Bodi za nchi za Afrika Mashariki.

“Lakini tunapenda kuwataarifu kwamba kwa miaka miwili iliyopita, madaktari wa Kenya wamekuwa wakihangaika na Serikali ya Kenya kuhusu idadi yetu na kukataliwa kwa kile Serikali na Wizara ya Afya ilichosema ni ukomo wa bajeti jambo ambalo lilikuwa likichochea mgomo uliokwisha wiki moja iliyopita.

“Tunawashukuru kwa kutuunga mkono wakati wa mgomo wetu uliodumu kwa siku 100.

“Tumeona makubaliano ya Serikali ya Kenya na Tanzania wa kuleta madaktari 500 ili kuleta uwiano (ration) kati ya wagonjwa na madaktari kwenye pengo lililopo nchini kwa sasa.

“Hadi kufikia Mei 2017, kutakuwa na madaktari wanaokadiriwa kufikia 1,400 ambao hawajaajiriwa na Serikali ya Kenya,” ilisema taarifa hiyo.

Wakati huo huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema madaktari 159 nchini wametuma maombi ya kazi kwenda kufanya kazi nchini Kenya hadi sasa, tangu Serikali ilipotoa tangazo Machi 18, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ummy aliwatoa hofu madaktari kuhusu usalama wao wawapo nchini Kenya kutekeleza majukumu yao.

 “Rais Uhuru Kenyata ambaye ni mwenyeji wetu, amemuhakikishia Rais Dk. John Magufuli, kwamba tutakuwa salama,” alisema.

Ili kukamilisha suala hilo, alisema tayari wizara yake imeandaa rasimu ya makubaliano ambayo itaeleza mambo yote kimaandishi, likiwamo suala la usalama na masilahi yao waliyoahidiwa.

Alisema madaktari hao watakapoajiriwa nchini humo watalipwa mshahara sawa na madaktari wengine wa huko.

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari, alisema kabla ya uamuzi huo kutolewa na kukubaliwa na nchi zote mbili, ulijadiliwa kwa kina faida na athari zitakazojitokeza.

“Kenya ilituhakikishia usalama wa madaktari wetu, mshahara mzuri pamoja na makazi ya uhakika, hivyo Serikali ilijiridhisha ni fursa nzuri ya ajira kwa madaktari wetu,” alisema Profesa Mohamed.

Msimamo wa MAT
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kimepinga uamuzi wa Serikali kuipatia madaktari 500 Kenya hadi hapo nchi hiyo itakapoanza kutekeleza makubaliano kati yake na madaktari wake ambao hivi karibuni waligoma kwa takribani miezi mitatu.

Taarifa ya MAT iliyotolewa juzi na Mwenyekiti wake, Dk. Obadia Nyogole, ilisema: “Kumekuwepo na maoni tofauti juu ya madaktari wa Tanzania kwenda Kenya, na zaidi ya asilimia 60 ya madaktari wa nchi hiyo wamepinga suala hilo na kutaka wazawa kwanza ndiyo waajiriwe."
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

TEF yamtangaza Makonda adui wa uhuru wa habari


Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) leo  limevitaka vyombo vya habari nchini kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam, Paul Makonda.

TEF wameyasema hayo leo katika  taarifa yao na kulaani vikali kitendo cha Makonda cha kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds usiku wa Machi 17 akiwa na askari wenye silaha.

“Kwa mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul Makonda kuwa ni Adui wa Uhuru wa Habari, na yeyote yule atakayeshirikiana naye katika kukandamiza uhuru wa habari nchini,” ilisema taarifa hiyo ya TEF iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Theophil Makunga.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

TANZANIA YAPATA MKOPO WA BILIONI 109 KUJENGA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA


1
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB), (kulia), akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Kuwait Bw. Hamad Al-Omar (katikati), baada ya kubadilishana Hati ya Mkopo wa Sh. Bilioni 109.69 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyahua- Chaya yenye urefu wa Kilometa 84.5 kwa kiwango cha lami, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
2
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mipango (MB), (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Kuwait Bw. Hamad Al-Omar (kushoto), wakisaini mkataba wa makubaliano ya mkopo wa wa riba nafuu wa Sh. Bilioni 109.69 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyahua- Chaya yenye urefu wa Kilometa 84.5 kwa kiwango cha lami, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam..
3
Baadhi ya wajumbe walioongozana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Kuwait Bw. Hamad Al-Omar (hayupo pichani) wakishuhudia utiwaji saini wa mkataba wa makubaliano ya mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. Bilioni 109.69 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyahua- Chaya yenye urefu wa Kilometa 84.5 kwa kiwango cha lami, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
4
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mipango (MB), (mbele kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa barabara ya Nyahua-Chaya, itakayojengwa kwa kiwango cha lami baada ya kupata fedha kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Kuwait.
5
Wajumbe kutoka Tanzania wakishuhudia utiwaji saini wa mkataba wa makubaliano ya mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. Bilioni 109.69 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa Kilometa 84.5 kwa kiwango cha lami, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
6
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mipango (MB), (wa tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Kuwait Bw. Hamad Al-Omar (wa tano kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Maafisa wa Serikali ya Kuwait, baada ya kusainiwa kwa mkataba wa mkopo wenye riba nafuu wa  Sh. Bilioni 109.69 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya, yenye urefu wa Kilometa 84.5 kwa kiwango cha lami, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
7
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mipango (MB), (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Uchumi wa Kuwait Bw. Hamad Al-Omar (wa pili kushoto) wakiondoka baada kusainiwa kwa mkataba wa mkopo wenye riba nafuu wa Sh. Bilioni 109.69 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa Kilometa 84.5 kwa kiwango cha lami, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
8
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mipango (MB), (kulia) na wajumbe kutoka Kuwait wakijadili jambo baada ya kusainiwa kwa mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa  Sh. Bilioni 109.69 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya, yenye urefu wa Kilometa 84.5 kwa kiwango cha lami, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Tuesday, March 21, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 22


Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Serikali yafuta Usajili wa Vibali vya Uzalishaji na Uingizaji wa Pombe za Viroba.



Na: LilianLundo – MAELEZO
Serikali imefuta usajili wa vibali vya uzalishaji na Uingizaji wa aina 20 ya pombe kali za viroba zilizokuwa zimesajiliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam kuhusu usitishaji wa uzalishaji na uingizaji, uuzaji na matumizi ya pombe zilizofungwa katika mifuko ya plastiki (Viroba).

“Tumefuta usajili wa vibali vya uzalishaji na uingizaji kutoka nje, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika mifuko ya plastiki (viroba) chini ya ujazo wa milimita 200,” alifafanua Ummy Mwalimu.

Aliendelea kwa kusema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa tamko la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilotoa Februari 02, 2017 la kusitisha uzalishaji, uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe hiyo kali kuanzia Machi 01, 2017.

Ummy amesema kuwa usitishaji huo unazingatia kanuni za kukataza uzalishaji, uingizaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki kufungashia pombe kali za mwaka 2017 (The Environmental Management (Prohibition of Manufacturing, Important and Use of Plastic Sachets for Packakging Distilled and other alcoholic beverages) Regulations 2017) imekatazwa kutumia vifungashio vya plastiki kufungashia pombe kali. Badala yake wazalishaji watapaswa kufungasha pombe kali hizo katika chupa zenye ujazo usiopungua mililita 200.

Aidha amesema kuwa uamuzi wa kupiga marufuku matumizi ya pombe za aina hiyo unatokana na athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kiafya na kijamii. Matumizi mabaya ya pombe hizo yamesababisha ajali nyingi, vifo, ulemavu na mzigo mkubwa kwa Serikali wa kutoa huduma kwa wahanga wa pombe hizo na ongezeko la makosa ya jinai.

Ummy amesema kwamba Viroba vilivyokamatwa na kuzuiwa vinasubiri maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu namna ya kuviteketeza
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

Serikali Yakana Kumshikilia Yusuf Manji


Sakata la kushikiliwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Yusufu Manji limeendelea kuchukua sura mpya, safari hii yakiibuka mabishano Mahakama Kuu baada ya Serikali kukana kumshikilia.
Mabishano hayo yameibuka jana kati ya mawakili wa Serikali na mawakili wa Manji baada ya mfanyabiashara huyo kufungua maombi juma lililopita akihoji uhalali wa kushikiliwa na Uhamiaji.
Manji aliyefungua maombi hayo mahakamani hapo kupitia Wakili wake Hudson Ndusyepo, anaiomba mahakama iiagize Uhamiaji afikishwe mahakamani ili mahakama iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kisha iamuru aachiwe huru.
Kutokana na maombi hayo, Jaji Ama-Isario Munisi, aliwaamuru wajibu maombi kuwasilisha hati zao za kiapo kinzani dhidi ya maombi hayo na kupanga kuyasikiliza jana mchana.
Wajibu maombi ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.
Hata hivyo jana Serikali katika majibu yake kupitia  hati ya kiapo kinzani cha Ofisa Uhamiaji, Anorld Munuo, ilikana kumshikilia mfanyabiashara huyo. Mbali na kiapo hicho, Wakili Mkuu wa Serikali, Oswald Tibabyekoma, alisisitiza kuwa mfanyabiashara huyo hashikiliwi na yuko huru.
Maelezo hayo ya Serikali yalipingwa vikali na mawakili wa Manji, Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo, ambao kwa nyakati tofauti walisisitiza kuwa hadi jana mfanyabiashara huyo alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, kwa matibabu, akiwa chini ya ulinzi wa maafisa Uhamiaji
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.